MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

Martin Luther alishapata cheo cha , 'uaskofu' wakati huo. Dhana kwamba alifuta vitabu 7 napata shida mamlaka hayo aliyapata wapi? Mnyonge mnyonge lakini haki yake mpe
Kwa taarifa yako Biblia ya Martin Luther siyo tu ilikuwa na mapungufu ya vitabu 7 vya Agano la Kale, pia aliondoa vitabu vya Yakobo, Waebrania na kitabu cha Ufunuo.

Reformet mwenzake Calvin ndio alimzuia kuondoa vitabu hivyo vya Agano Jipya na ndipo Luther akavirejesha vitabu hivyo..
 
Sikuwahi pata good and complete Clarification za Padre Luther na je nani mwenye mamlaka ya kutoa vitabu na kupunguza mistari ya bibblia
Pili kanuni za kanisa ndizo alizipinga au bibblia?
Ahsante
Kwa kifupi Martin luther naweza kusema alikuwa ni Opportunistic...Alipata loop hole ya kuondoa vitabu vya Agano la kale, baada ya kurejea mitaguso ya Kanisa (hasa mtaguso wa trent) masahihisho yanahitajika hapa.

Wakati Kanisa Katoliki lina-compile Bible, Kuna vitabu 7 vya Agano la Kale ambavyo vilipokelewa kwa lugha ya Kigiriki...Hivyo Wayahudi(Waisrael) hawakuvitambua vitabu hivyo simply bze of language....Hivyo Luther akatumia mwanya huo kuviondoa.

Ila alishindwa kuondoa vya Agano jipya maana hivyo vilikuwa nje ya uwezo wake.....Ila ni bahati tuu, maana alisha viondoa vitabu 3... Calvin alimsihi sana kuvirudisha...

Kituko
 
Biblia na historia ya kanis
Historia ya Biblia ni kuwa ni Kitabu kilichotengenezwa na Kanisa Katoliki na kukamilika mwaka 300 Ad...Ilikamilika ilkiwa na vitabu 72/73 ila baadae Martni Luther aliondoa vitabu 7 na kubakiwa na vitabu 66.,
Hakuishia hapo, aliondoa vitabu 3 vya Agano jipya....Biblia ya Martin Luther ilikuwa na vitabu 39 vya Agano La Kale na Vitabu 24 vya Agano jipya..

Reformer mwenzake Calvin ndiye aliyemsihi kuvirudisha vitabu 3 ya Agano jipya..
 
Duh kaaazi kweli kweli hapo ndo mlipo mpa cheo binadamu mwenzenu awe mwombezi. mmesahau kwamba mariam na yeye ni binadamu kama niniyi na alishakufa anasubiri ufufuo siku ya mwisho.. sasa sijui nani kawadanganya kwamba maria yuko hai...... Au ni katika kitabu gani kimemtaja Mariam Kwamba yi hai ambapo anaweza kusikia maombi yenu
Rejea Kitabu cha Mhubiri 7:12

Nayo mwili hurudi mavumbini ulikotoka nayo Roho kumrudia Mungu aliyeitoa .....

Roho haifi kamwe...

Soma ufunuo 5:8 uone Watakatifu wanafanya kazi gani mbinguni..
 
alipazwa? lete andiko acha hizo historia za kanisa mlizo mezeshwa na zilizotungwa na watu ndio maana Luther mlishindwa kujibu hoja zake..

Haya lete andiko la kupazwa kwa Maria
Soma Ufunuo uone jinsi Yohane anapata ufunuo..

"Tazama ishara ikaonekana mbinguni, mwanamke aliyevikwa jua na mwezi chini ya miguu yake na taji ya nyota 12 juu ya kichwa chake"
 
uongo wa mchana hebu lete andiko.
maana maria ndiye aliyesema hivyo.
LUKA 1:46-48.
anasema watamwita mmbarikiwa lakini sio Mungu kusema tutamwita hivyo
Kwamba hayo aliyoyasema siyo Neno Mungu? Au tunaposema Biblia ni neno la Mungu tunamaanisha nini hasa?

Ni hatari maana mwisho wa Siku barua zote alizoandika Paulo utasema si neno la Mungu ila ni mawazo ya Paulo....
Angalia usije ingia kwenye mtego huo, kwa kujifanya mjuvi wa kupinga hata vitu halisi na wazi...
 
Kanisa katoliki wanamuhitaji Mungu kwakweli na ndio mana wengi wanaoelewa neno huwa wanakimbia, Japo sijawahi kuwa mkatoliki lakini nasikia ukifa siku ya kuzikwa padri akikuombea rehema basi unasamehewa makosa yako!

Na pia mama maria ndo anawaombea wakatoliki, pia ndo dhehebu pekee ambalo pombe imehalalishwa!! Mungu atusaidie sana
 
Mmepotea ninyi wakatoliki, kasime YOHANA MT. 14:6 then urudi hapa utuambie mmepata wapi maandiko ya kumuomba Mungu Baba kupitia kwa Bikira MARIA.
Maria ni Mtakatifu kama Watakatifu wengine...Na Watakatifu wana kazi ya kutuombea....Wao ni Kanisa Shindi huko mbinguni..

Soma Ufunuo 5:8 uone maombi ya Watakatifu na Wale wazee 24 mbele ya Kiti cha Mwana Kondoo..
 
Back
Top Bottom