Kwanini ofisi ya DPP wanatuona Watanzania ni wajinga na Vilaza? Huyo mwizi kaibaje computer kwenye ulinzi wa CCTV na jeshi lenye SMG & AK47

WATANZANIA SIO WAJINGA KIASI HIKI

Leo vyombo vya habari vimeripoti kwamba Computer za ofisi ya DPP tena zenye nyaraka za kumbukumbu za waliolipa fedha za uhujumu uchumi na nyaraka nyingine zikiwemo za mienendo ya mashtaka ya kesi za uhujumu zimeibwa. Huu ni zaidi ya ukoo wa panya. Huwezi kumpata asiye mwizi katika ukoo wa panya, kuanzia Babu, Bibi, Baba, Mama, watoto, wajukuu, vitukuu, vilembwe na vilembwekeza wote ni wezi tu.

Swali ni nani huyo anayeweza kuiba ndani ya ofisi ya DPP?

Ofisi ya DPP imesheheni ulinzi kabambe wa walinzi waliojihami kwa silaha nzito za kivita ikiwemo SMG, AK47 n.k. Huyo aliyeiba hizo computer tena zote alipita wapi bila kuonekana na huu ulinzi? Alipitaje na hilo furushi la computer bila walinzi kumhoji. Au alizimeza hizo computer ili akishatoka akanywe dawa ya kuhara ili aziharishe?

Ofisi za DPP zinalindwa na mifumo ya kisasa ya CCTV camera. Je CCTV hizo ndani na nje ya jengo la ofisi hiyo hazikuweza kuwanasa hao wezi? Au tuseme nazo ziliondolewa kama zile za kule Dodoma aliposhambuliwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu? Au mnataka tuamini kwamba CCTV hizo ni kama zile zilizokuwepo collesium hotel kule alipotekwa MO DEWJI zikashindwa kunasa na kuonesha watekaji hadi leo?

Kwa nini hizo laptops and desktops zisiibwe kabla ya Ofisi ya DPP kuanza kukusanya mabilioni kwa mbwembwe huku yakitangazwa hadharani?

Kwa nini hao wezi waibe computer zenye kumbukumbu za malipo ya wahujumu uchumi na nyaraka za mienendo ya kesi zao tu na waache computer zenye kumbukumbu na nyaraka za watuhumiwa wengine kama wale Masheikh wa Uamsho kutoka nchini Zanzibar? Au nao nyaraka zao zimeibwa? Hao wezi walijuaje kwamba computer hizi zina nyaraka fulani na hizi hazina? Watakuwa wana akili nyingi na uwezo mkubwa sana wa michezo ya betting hasa ikizingatiwa kuwa computer hizo pengine zilikuwa zimezimwa na zina password complicated sana.

Ofisi ya DPP inajua kuwa utaratibu salama ni Fedha kulipwa Benki na mlipaji kuwasilisha stakabadhi za malipo. Swali ni kwa nini DPP akijua hayo yote aliamua kukusanya mabilioni hayo kwa vikapu, maboksi, sandarusi na magunia? Ofisi ya DPP ni Benki? Ofisi ya DPP ni hazina?

Kwa nini haikufunguliwa account maalumu ya kukusanya hicho kinachoitwa wahujumu uchumi kutubu na kurejesha fedha na watu wakalipa kwenye account hiyo? Hata kama computer zingeibwa si fedha zingekuwa salama na nyaraka za malipo ingekuwa ni rahisi tu kuzi trace kwenye Benki husika?

Hii haiingii akilini hata kidogo. Kwamba loss report tu ya kadi ya gari na simu, bill za maji, bill za umeme, ada ya watoto wa shule, fomu za kuomba chuo na mikopo, ada ya cheti cha kuzaliwa cha Mtoto na hata malipo ya gharama ya shilingi elfu 1 tu unapewa lipa bill control number au account ya Benki ulipe kwa simu au Benki halafu upeleke slip for payment au nambari ya muamala lakini kwa DPP mabilioni yanalipwa kwenye sandarusi alafu leo mnatuletea hekaya za Abunuwasi, Esopo na hadithi za Alufu Lela Ulela hapa kuwa computer na nyaraka za malipo zimeibwa. Nonsense! Kwamba mnataka kuwa suspect waliolipa kuwa ndio watuhumiwa ili muwashike walipe tena au mnataka Watanganyika wadanganyike na kuamini kuwa nyaraka zimepotea na pesa zimepotea hivyo tumuachie Mungu mwenyewe tu ashughulike na wezi?

Nani anayefahamu hizi fedha zinaingizwa kwenye account ipi ya Serikali na kwa ajili ya matumizi gani na nani anapanga matumizi yake? Je zinaelekezwa BOT, hazina, Ikulu au wapi? Je Bunge linajua matumizi yake?

Hapa kwa nini tusihoji hata zile 20,000 za vitambulisho vya wajasiriamali zinapelekwa wapi? Je ni Ikulu, hazina au BOT. Je matumizi yake ni yapi na Bunge linajua matumizi hayo?

Kwamba ofisi nyeti ya DPP anataka kutuambia kuwa haina back up? Kwamba hata ingeungua basi kusingekuwa na kumbukumbu nyingine yoyote ya mienendo ya mashtaka na wahalifu? Ofisi za DPP hazina back up salama ndani ya nchi? Hazina backups za kwenye Google drive na icloud?

Je hapa hapakuwa na nia ovu? Je mpango huu ni tukio la bahati mbaya au ilikuwa ni sehemu ya kuandaa na kuhalalisha mpango huu? Kesho mtakuja kutuambia kuwa kwenye mabilioni yote mnayodai kuyakusanya baada ya wizi huu ni milioni 10 tu imebaki na zingine zilienda na computer.

Kwamba sasa hata wahujumu uchumi mnaowashikilia mnataka kusema itabidi muwaachie kwa sababu hata nyaraka muhimu za kumbukumbu za kesi zao za uhujumu uchumi nazo zimeibwa pamoja na computer. Nini kipo nyuma ya pazia?

Wakati zoezi hili linaanza niliwahi kuhoji ikiwa by any chance zoezi hili lina connection yoyote na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu 2020 kifedha?

Nashawishika kuamini kuwa kama huu sio utani msibani basi ni sinema yetu pendwa ya FUTUHI! Nchi hii haiishiwi vimbwanga! Kwamba upepo mkali wa Kisulisuli kutoka Mlima wa MOTO umepeperusha computer za DPP zenye nyaraka za malipo ya wahujumu uchumi na kama haitoshi kisulisuli hicho kikapeperusha walinzi wote wanaolinda ofisi za DPP. Basi huenda walinzi wote na CCTV zote pale ni wanaume nao walipeperushwa kuelekea Mlima wa MOTO kuwahi fursa.

_________
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Dar, Lazaro Mambosasa amesema taarifa walizipata Jumanne asubuhi na wanaendelea kufanya uchunguzi.

Amesema hadi sasa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo. Kwamba hadi sasa hakuna mshukiwa yeyote! Tafakari!

Hapa sijui nani anampeleleza nani? DPP ni Polisi, ofisi ya DPP inalindwa na Polisi, sehemu kubwa ya Watumishi wa ofisi ya DPP ni Polisi, Kamanda wa Polisi ni Polisi, upelelezi ni polisi. Je polisi wanajipeleleza wenyewe?

Je upelelezi unafanyika watu wakiwa ofisini hakuna anayejiuzulu ili kupisha upelelezi. Je huu upelelezi utakuwa HURU na HAKI bila kuingiliwa na wakubwa?

Alipopigiwa simu, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga kuulizwa kuhusu tukio hilo, alijibu kwamba yuko kwenye kikao.

Tukio hili limetokea ikiwa ofisi hiyo ya DPP iko katika mchakato wa kujadiliana na kuingia makubaliano na watuhumiwa mbalimbali wa kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha.

Miongoni mwa kesi ambazo ziko katika hatua ya makubaliano ni kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili vigogo wa IPTL, Harbinder Sethi na James Rugemalira wanaodaiwa kutakatisha zaidi ya Sh bilioni 309.

Watuhumiwa wengine ni mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera anayetuhumiwa kukwepa kodi na kutakatisha Sh milioni 173.

Mtuhumiwa mwingine ni Yusuf Ally maarufu Mpemba wa Magufuli, anayetuhumiwa kusafirisha nyara za Serikali zenye thamani zaidi ya Sh milioni 200.

Ofisi hiyo kwa wiki mbili zilizopita imeingiza zaidi ya Sh bilioni 40 ambazo kati yake zaidi ya Sh bilioni 3.6 zimepokewa na zilizobakia wahusika watalipa kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa kati yao na DPP.

Pia Serikali imetaifisha nyumba sita za washtakiwa waliokuwa wakikabiliwa na makosa ya uhujumu uchumi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ndani ya wiki moja.

Oktoba 4, mwaka huu, mshtakiwa Yasin Katera aliyekuwa akishtakiwa pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Takukuru, Godfrey Gugai alilipa faini ya Sh milioni 100 na Serikali ikataifisha nyumba moja iliyopo Nyegezi, Mwanza.

Alilipa faini hiyo baada ya kukiri kosa la kutakatisha fedha huku akijua fedha hizo ni zao la kuficha ukweli baada ya kudai ni mmiliki wa nyumba wakati nyumba ni mali ya rafiki yake, Gugai.

Wafanyabiashara Magdalena Uhwello na Halima Nsubuga walikiri makosa ya kutakatisha fedha wakahukumiwa kulipa faini ya Sh milioni 101 na fedha zao Dola za Marekani 388,000 kutaifishwa na Serikali.

Mahakama iliamuru washtakiwa wakishindwa kulipa fedha hizo wataenda jela mwaka mmoja kwa kosa la kuendesha upatu na wataenda jela miaka 20 kwa kutakatisha fedha.

Oktoba 7-11, mwaka huu, wafanyabiashara watatu, Mohammed Yusufali, Arifali Paliwalla na Sameer Khan walilipa fidia Sh 1,201,000,000 baada ya kukiri makosa yao na nyumba nne zilizopo Bagamoyo mkoani Pwani na Masaki, Dar es Salaam zilitaifishwa na kuwa mali ya Serikali.

Hukumu hiyo ilitolewa na Mahakama Kuu Kitengo cha Uhujumu Uchumi mbele ya Jaji Elinaza Luvanda. DPP aliwapunguzia mashtaka kutoka 544 na kubakia matatu.

Akisoma mashtaka hayo, Wakili wa Serikali Mkuu, Oswald Tibabyekomya alidai shtaka la kwanza na la pili yanamkabili mshtakiwa Yusufali pekee.

Kwamba katika vipindi tofauti kati ya Januari 2008 na Januari 2016 jijini Dar es Salaam, akiwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Farm Plant Limited, kwa nia ya kukwepa kodi aliwasilisha ‘retuns’ za kughushi kwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kusababisha ukwepaji kodi wa zaidi ya Sh bilioni 21.

Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa kati ya Agosti 2015 na Januari 2016, kwa vitendo kama hivyo, mshtakiwa huyo alisababisha ukwepaji kodi wa Sh 1,684,559,546.47.

Shtaka la tatu la washtakiwa wote, wanadaiwa kuwa kati ya Januari 2008 na Januari 2016, kwa vitendo vyao vya uwasilishaji wa nyaraka za uongo za ulipaji kodi, waliisababishia TRA hasara ya Sh 24,303,777,426.70.

Mahakama iliamuru mshtakiwa Yusufali alipe fidia ya hasara aliyoisababishia TRA ya zaidi ya Sh bilioni 24 na tayari alishalipa sh bilioni moja.

Wakili Tibabyekomya alisema kiasi kilichobaki kitalipwa kwa muda wa miezi 24 ambapo kila mwezi atalipa sh 970,990,726.08 pamoja na kutaifishwa kwa nyumba nne zilizo maeneo ya Masaki na Bagamoyo kuwa mali ya Serikali.

Kwa upande wa mshtakiwa wa pili, wakili huyo aliomba alipe fidia ya Sh milioni 10 ya hasara aliyoisababishia TRA ambapo tayari alishalipa sh milioni moja.

Alisema kiasi kilichobaki kitalipwa kwa kipindi cha miezi 12 kwa kila mwaka Sh 750,000.

Kwa upande wa mshtakiwa wa tatu, wakili huyo aliomba alipe fidia ya Sh milioni 300 kutokana na hasara aliyoisababishia TRA na tayari alishalipa Sh milioni 200.

Alisema kwa mujibu wa makubaliano hayo, kiasi kilichobaki kitalipwa kwa kipindi cha miezi 10 kuanzia tarehe aliyoingia makubaliano na kila mwezi atalipa Sh milioni 10.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimwachia huru Mkurugenzi Mkuu wa Benki M (Tanzania), Sanjeev Kumar (63) na kumtaka kulipa fidia ya zaidi ya Sh bilioni 6 na faini ya Sh milioni 2 baada ya kukiri.

Mshtakiwa Kumar ametakiwa kuilipa fidia hiyo ndani ya miezi 24 na tayari ameshalipa Sh milioni 690.

Akisoma adhabu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi alisema kuwa katika mashtaka hayo mawili, mshtakiwa atatakiwa kulipa faini ya Sh milioni moja kwa kila kosa.

Alisema pia mshtakiwa atatakiwa kulipa fidia ya Sh 6,039,103,579 ambazo atalipa kwa miezi 24, kwa kila mwezi Sh milioni 222.8.

Kigogo wa Michezo, Michael Wambura alikiri makosa ya kujipatia jumla ya Sh milioni 100.9 na wakakubaliana na DPP kurejesha fedha hizo kwa awamu tano na tayari Oktoba 7 alirejesha Sh 20,249,531.

Wakili maarufu, Dk. Ringo Tenga na wakurugenzi wenzake wa Kampuni ya Six Telecoms, wameachiwa huru baada ya kuingia makubaliano na DPP ya kulipa Dola za Marekani 3,748,751.19, ndani ya miezi sita, kuiachia Serikali nyumba iliyopo Mikocheni na mshtakiwa wa sita kulipa Sh milioni 30.

Wakurugenzi hao; Dk. Tenga, Hafidh Shamte na Peter Noni na Noel Chacha ambaye ni Ofisa Mkuu wa Fedha, wanatakiwa kulipa zaidi ya Sh bilioni 3 na Frank Mwalongo anatakiwa kulipa Sh milioni 30.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi alisema makubaliano mengine ambayo mahakama inatakiwa kuzingatia ni kwamba washtakiwa wamelipa Sh milioni 150, Dola za Marekani 150,000 na Dola 3,585,115 zilizobakia washtakiwa kuanzia wa kwanza hadi watano watalipa ndani ya miezi sita kuanzia Oktoba 7.

Mshtakiwa Mwalongo alilipa Sh milioni 35 alizokubali kulipa kama fidia na faini.

Nasisitiza tena Watanzania sio wajinga kiasi hiki. Waliomteka MO DEWJI tuliambiwa ni wazungu wanaoongea lafudhi ya kizulu (Afrika Kusini) sasa msije kutuambia walioiba hapa kwa DPP ni wazungu wanaozungumza lafudhi ya Kisukuma. Swali ni Je, nani huyo anayeweza kuiba ndani ya ofisi ya DPP?

Remmy Cameroon
Sauti ya wasio na sauti
Hamchoki na ndoto za mchana mkiamini ndio uhalisia wa mambo! Tanzania inabadilika nyie bado mnaishi Kitanganyika kabla ya uhuu ambapo Mzungu aliheshimika kama Mungu Mtu. Poleni!!!!
 
Wacha waibe kwani si ziko humuhumu tu.vibaya kupeleka uswiss
Na wewe iba utujengeee vivuli vya magorofa masaki.umetumikia weeee kafiri amekutosa. huna mgao unalialia nini?
 
Wadau habar za majukumu
Tetesi nilizo zipata ni kuwa kile tulicho ambiwa kuwa ktk ofisi ya DPP kumeibiwa Compyuta ni changa la Macho.

Habari zinadai kuwa wajanja wamelamba MABILIONI kadhaa yaliyokuwa yamehifadhiwa ktk ofisi hiyo yaliyokuwa yakirejeshwa na wanaodaiwa wahujumu uchumi waliokiri makosa yao.

Nashawishika kuamini tetesi hizi kwa kujiuliza maswali magumu haya.

1. Ni mtu gani mwenye uwezo wa kuvunja ofisi ya DPP na kuiba kompyuta halafu akafungue kamera za ulinzi ili iwe nini?

Anapata wapi ujasiri wa kufungua camera za ulinzi na kwa nini afungue camera?

Kompyuta zina faida gani mpka mtu aziibe na ahangaike mpaka kufungua camera za ulinzi? Je ofisi muhimu kama hii haina walinzi ukiacha hizo kamera?

Inavyo onekana walio fanya hilo tukio sio watu wachovu. Wanafanana na wale walio fungua kamera za ulinzi ktk tukio la kushambuliwa kwa Tundu Antipas Lissu. Tukio hilo limeratibiwa kimkakati na mafisadi wa Awamu hii na watu hao hawata kamatwa wala kuonekana. Hawa ndio wanao jiita wazalendo kupita kiasi.

Mataga endeleeni kuimba mapambio ya kuabudu na Kusifu awamu ya majambazi wazalendo.
CC. Meko
CC. Lumumba buku7
 
Back
Top Bottom