Kwanini OCD wa Hai na RPC wa Kilimanjaro wasishtakiwa kwa kukaa kimya wakati Ole Sabaya anatekeleza uhalifu akiwa DC wa Hai?

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
2,051
2,000
Wadau nawasalimu

Nadhani wote tunayajua aliyoyatenda general Ole Sabaya DC wa Hai akiwa madarakani.

Dc Sabaya alitenda uhalifu mkubwa na leo tunashuhudia akiwa mahakamani tayari kahukumiwa kesi moja na nyingine zinaendelea. Najiuliza wakati dc sabaya anatenda uhalifu huo kulikuwa na ocd wa hai na rpc wa kilimanjaro ambao ni wajumbe wa kamati za ulinzi na usalama za wilaya na mkoa je viongozi hawa hawakuujua uhalifu huo?

Je kwanini hawakumchukulia hatua?

Au walikuwa washirika wake?

Je, kutomchukulia hatua kwanini kusitafsiriwe kuwa walishindwa kuwajibika katika nafasi zao?

Binafsi sidhani kama ni sahihi kutowachukulia hatua kwani walimuacha sabaya atende uhalifu huku wakimwona.
 

Tardy

JF-Expert Member
Oct 31, 2021
820
1,000
Wanaodai katiba wana hoja ya msingi itakayojibu moja ya maswali yako hayo.
Kwa ufupi elewa hivi
RPC NA OCD siyo wateule wa Rais.
General Sabaya alikuwa mteule wa Rais.
RPC/OCD ni makatibu wa ulinzi,wenyeviti ni RC/DC.
 

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
5,327
2,000
Wanaodai katiba wana hoja ya msingi itakayojibu moja ya maswali yako hayo.
Kwa ufupi elewa hivi
RPC NA OCD siyo wateule wa Rais.
General Sabaya alikuwa mteule wa Rais.
RPC/OCD ni makatibu wa ulinzi,wenyeviti ni RC/DC.

35C252DD-1221-4685-A1E7-F96A312D041F.gif
 

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
11,843
2,000
Sabaya ashasema alitumwa na Magufuli. Sasa ulitegemea OCD na RPC wampinge rais ?

Katiba hii inampa mamlaka makubwa sana rais. Anaweza kuwaua wasukuma wote na bado asishitakiwe popote.
 

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
2,051
2,000
Wanaodai katiba wana hoja ya msingi itakayojibu moja ya maswali yako hayo.
Kwa ufupi elewa hivi
RPC NA OCD siyo wateule wa Rais.
General 7baya alikuwa mteule wa Rais.
RPC/OCD ni makatibu wa ulinzi,wenyeviti ni RC/DC.
Nauliza Tu
Kwa Hiyo MTEULE wa RAIS Akifanya UHALIFU hakamatwi au inakuwaje mkuu?
 

Tardy

JF-Expert Member
Oct 31, 2021
820
1,000
Sabaya ashasema alitumwa na Magufuli. Sasa ulitegemea OCD na RPC wampinge rais ?

Katiba hii inampa mamlaka amakubwa sana rais. Anaweza kuwaua wasukuma wote na bado asishitakiwe popote.
Mfano wako wakichokozi,kwanini asiwaue wapemba au wamasai
 

Tardy

JF-Expert Member
Oct 31, 2021
820
1,000
Nauliza Tu
Kwa Hiyo MTEULE wa RAIS Akifanya UHALIFU hakamatwi au inakuwaje mkuu?
Ndio maana nimesema wanaodai katiba wanahoja.

1.Nani wakumkamata kama Amiri jeshi amemuamuru afanye hivyo.

2.Anaye amuru hashitakiwi popote.

3.Uliyeteuliwa uliapa kuwa utamtii.

NB.
Viapo hufanyika kwa kushika vitabu vya Mungu huku miongozo ipo kwenye katiba.

Mungu huwa nishahidi kuwa mtamwinua mteule wenu bila sababu.
 

Kalunya

JF-Expert Member
Oct 5, 2021
3,732
2,000
Sabaya ashasema alitumwa na Magufuli. Sasa ulitegemea OCD na RPC wampinge rais ?

Katiba hii inampa mamlaka amakubwa sana rais. Anaweza kuwaua wasukuma wote na bado asishitakiwe popote.
Kama alitumwa mbona wamemtosa
 

Kb Nigger

Member
Nov 22, 2021
55
125
Ndugu,uliwahi kusikia hata sauti ya PDF,zaidi zaidi alikuwa muda wote kwenye msafara wa Jiwe.
hata ,Jaji mkuu IGP
Ungewahurumia hao uliowataja.NENO MHIMILI ULIOJICHIMBIA.Nouma xana.
Mahakama zipo zinajifaragua tu.Kiufupi inatakiwa KATIBA MPYA,Japo hata iliyopo sijawahi kupata mda wa kuisoma.Sababu ni maisha magumu,tunaongozwa kwa matamko ya wanasiasa na si ya viongozi.

JIWE APUMZIKE KWA TAABU TU.hakuna namna.
 

Kalunya

JF-Expert Member
Oct 5, 2021
3,732
2,000
Wanalindwa na Pgo kwa mujibu wa wao wenyewe.
Kazi ya police ni kupokea maagizo ya wanasiasa bila kuhoji."OCD kamata huyu weka ndani" na police atakamata bila kuhoji,nchi zingine upuuzi huu hakuna police wapo huru,wanafata sheria na sio maagizo.

Zama zile Mungu alipotuacha vibaraka wake waliwaumiza Sana Watanzania wakiwemo wapinzani Ili kumfurahisha shetani.
 

Kalunya

JF-Expert Member
Oct 5, 2021
3,732
2,000
OCD akikamatwa RPC wa makonda nae aponi alikuwa wapi bashite akiyatenda hayo.

Sema ccm inawalinda wahalifu ni vigumu hao makada wanaoisaidia ccm kuiba kura kukamatwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom