Kwanini nyimbo nyingi za siku hizi ni sex song na sio love song?

Mndengereko

JF-Expert Member
Mar 24, 2011
7,280
3,345
Wakuu heshima yenu,

Nowdays kumekuwa na tabia kubwa sana ya wasanii wa kileo wa Bongoflavour nyimbo zao nyingi wanazotoa ni sex song na sio love songs,nyimbo nyingi zinazungumzia jinsi ya kufanya mapenzi,(how to make love-love making) na hazizungumzii love in general.

Kwa uchache mfano wa nyimbo za sex songs ni Iokote, Gusanisha, Nicome ya Weusi, Jibebe, Tetema, nyimbo za Lulu Diva, za Mbosso nk.

Kwa haraka haraka nizitaje hizo wakati nyimbo nyingi hasa za zamani kama vile Yalaiti, Subal khery, za Ray C za zamani, Q Chief, TID na Alikiba za zaman na za wasanii kama Ben Pol, Aslay na Jux isipokuwa nyimbo yake ya Sumaku aliyoifanya na Diamond, zilizobaki nyingi kama sio zote ni love songs.

Kwa mtazamo wangu sex songs nyingi zinawagawa mashabiki wa msanii husika, kwani zinapoteza mashabiki ambao umri umeenda kwani zinakosa maadili somehow, na hvyo msanii husika kubaki na mashabiki vijana tu.

Nionavyo mimi ni vyema wasanii wakabadilika na kutunga nyimbo ambazo ni love songs ili msanii kuwa na kundi kubwa la wasanii vijana kwa wazee, akina mama na watoto.

Nawasilisha karibuni kwa mjadala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli mkuu! Nyimbo nyingi siku huzi ni matusi ya nguoni, huwezi kusikiliza mbele ya familia yako.
 
Mbona jibu ni rahisi sana ndio zinazopendwa kwasasa hivi, Kama zingekuwa aziuzi wange acha kuimba hizo nyimbo na nyimbo zote ulizotajwa hapo juu ndio zimefanya vizuri sasa. Mbona ma fk fk yanapigwa huko kwenye TV na mnaona kawaida.
 
Aisee kuna nyimbo zikipigwa mbele ya mtu mnayeheshimiana unaweza ukaingia chini ya meza

Mfano:Kata ya Ommy Dimpoz ft Nandy..full porno audio..nandy anasema,"come on nikupe burudani,i wanna give you my sweet punani"..mara anataka tango vimemkifu vibamia"..Yaani hizi nyimbo sio za kupigwa kwenye radio/Tv stations kabisa at day time
 
Sex sells...pvssy sells...

Sex ina stimulate dopamine ubongoni ya hatari sana

Ndio maana wanadamu wanapenda sex sana,au video games au internet au TV,etc
Mbona zamani hakukuwa na wingi wa nyimbo hizi mkuu..kitu gani kimebadilika kwa sasa??..Zamani watu walikuwa hawapendi sex??

Kisa watu wanapenda sex basi mitaani tuwe na mabanda ya kutosha ya kuonyesha pornograph sio??
 
Washabiki wa sasa ndo wanapenda hizo lakini sio za kudumu, miaka hiyo tutauendelea vizuri na mtoto iddi, mzee wa busara, mwokozi nitoe roho au chemsha bongo na nyingine kama hizo! Suala la muda tu
 
Mbona zamani hakukuwa na wingi wa nyimbo hizi mkuu..kitu gani kimebadilika kwa sasa??..Zamani watu walikuwa hawapendi sex??

Kisa watu wanapenda sex basi mitaani tuwe na mabanda ya kutosha ya kuonyesha pornograph sio??

Nyimbo zilikuepo

Sex ilikuepo

Dopamine imegunduliwa juzi na jinsi ya kuiamsha

Ndio maana facebook na instagram ni additive kwasababu ni engineered to trigger dopamine kwa makusudi!

Go figure!
 
Back
Top Bottom