Katika hali ya kawaida ungekuwa wewe ungetaifisha kwa mfano jengo au shule ambayo ipo ndani ya mazingira ya nyumba ya ibada? Kibasila secondary ya dsm ilikuwa ikiitwa st xavery... Ilitaifishwa na kulikuwa hostel ya kiume pale shule na za kike zilikuwa kule kanisani... Kwa hostel ilichukuliwa ile ya kiume tu ile ya kike sababu ilikuwa pale kanisani chang'ombe ikaachwa....Ukiyaangalia mazingira hayo utapata jibu.Kufuatia Azimio la Arusha serikali ilitaifisha taasisi ikiwemo hospitali, vyuo,majengo n.k. vya watu binafsi na mashirika ya kidini. Lakini shule za seminari za Kikatoliki hazikuguswa nini sababu hasa?mwenye kujua naomba msaada.
NB:
Ieleweke si kila shule inayomilikiwa na katoliki ni Seminari (mfano; St. Francis High School = sasa Pugu Sec. hii haikuwa seminari per se).
Chemsheni bongo msitoe majibu laini laini kama kawaida ya watanzania, hii sio kipima joto cha ITV kubwabwaja utumbo hapa ni "pweinti" tu zinatakiwa.