Kwanini Nyerere asomewe misa Kanisani-London??

barabaraya18

Senior Member
Sep 18, 2006
106
8
Hivi kwa nini balozi Mwanaidi anazidi kutafuta lawama?

Nyerere alikuwa baba yetu wote wakristo na wasio wakristo.Hata wakati anaombolezwa tulikuwa pamoja pale uwanja wa Taifa. Lakini leo kwa sababu ambazo anazijua mwenyewe Balozi wetu Bi Mwanaidi Mjaar kaamua kuwaba Babayetu wa Taifa Mwalimu Nyerere aombewe Kanisani lakini sio Ukumbi ambao watu wenye madhehebu mengine wangejisikia comfortable kumwombea dua Mwalimu

Hivi kwa nini wasiandae kitu kama Lecture ya kumkumbuka mwalimu na yale ambayo alitufunza kwenye ukumbi badala ya kujikita kwenye udiini usio na kichwa wala miguuu?

Kama familia ya mwalimu ingeamua kufanya hivyo in private ningeelewa lakini siyo hii ya Ubalozi na Balozi kuendelea na mchezo wao wa kibaguzi

Balozi mwanaidi hivi kwa nini unatumia back door kuwabagua watu ambao ulitakiwa uwawakilishe bila kuangalia mitazamo yao ya kidini?

Na zaidi ya hayo mbona hajafanya Juhudi za kumsomea Al haj Abeid Amani Karume hicho kisomo?

You would have thought Balzi ambaye ni lawyer by profession angejua a trade vipi kwenye mambo haya
 
Hivi Benjamin mkapa alipokuwa anaandaa futari ikulu alikuwa anawapendelea Waislamu kwa hivyo amewabagua Wakristo?

Je Wakristo wana haki ya kuuliza kwanini pesa ya kodi yao inaandaliwa Futari badala ya kununua vitabu vya shule ya msingi au dawa hospitalini?.

Hivi Mwalimu si alikuwa na dini? na alisomewa misa ya Marehemu pale Saint Joseph? Je wasiokuwa wakristo walilalmika kweli?

Nyerere alikuwa baba yetu wote wakristo na wasio wakristo.Hata wakati anaombolezwa tulikuwa pamoja pale uwanja wa Taifa. Lakini leo kwa sababu ambazo anazijua mwenyewe Balozi wetu Bi Mwanaidi Mjaar kaamua kuwaba Babayetu wa Taifa Mwalimu Nyerere aombewe Kanisani lakini sio Ukumbi ambao watu wenye madhehebu mengine wangejisikia comfortable kumwombea dua Mwalimu

Hivi kumuombea dua marehemu ni mpaka Kanisani au msikitini tu? huwezi kumuombea dua Marehemu nyumbani kwako?

Mimi ninaona cha msingi siyo wapi dua imeombewa ,Bali ni kumuombea Mwalimu dua njema na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia kiongozi mzuri kama Mwalimu .

Tuache dhana potofu Mwalimu alikuwa ni Mkiristo, kama jinsi viongozi wetu wengine walivyo waislamu, kama serikali inafanya mazishi au hitma ya viongozi wetu kuwatreat marehemu kwa mujibu wa imani zao sioni tatizo
 
Wakuu mbona nimeona futari imetayarishwa kwenye ukumbi wa Mtakatifu Ann, au?

Halafu mkuu Barabara, mbona huwa unatokea na ishu za kidini tu na Balozi Mwanaidi, vipi ishu zingine mkuu kama Buzwagi?

Halafu Balozi Mwanaidi si ni Mu-Islam, kwani hajui yote hayo mkuu au huyo mama amebadili dini baada ya kuwa balozi?
 
=gamba la nyoka;81458]Hivi Benjamin mkapa alipokuwa anaandaa futari ikulu alikuwa anawapendelea Waislamu kwa hivyo amewabagua Wakristo?

Mkapa hakulazimishwa kuandaa hizo kodi na nadhani wakristo na wasiokuwa wakristo wanayo kila haki ya kulalamika kodi zao kutumika katika masuala ya kidini wakti serikali ishasema haina dini

Je Wakristo wana haki ya kuuliza kwanini pesa ya kodi yao inaandaliwa Futari badala ya kununua vitabu vya shule ya msingi au dawa hospitalini?.

Hili nalikubali kabisa si wakristo tuu bali hata wasio na dini wanayo haki hiyo
Hivi Mwalimu si alikuwa na dini? na alisomewa misa ya Marehemu pale Saint Joseph? Je wasiokuwa wakristo walilalmika kweli?

Ishu siyo kusomewa misa kanisani bali ishu ni pale chombo cha kiserikali kama ubalozi na balozi ambaye alitakiwa awawakilishe waTanzania wote bila kujali dini au imani zao anapokuwa mstari wa mbele kuonyesha udini katika mamabo haya ya kitaifa

MIEZI KADHAA ILIYOPITA ALIFANYA MISA YA KUOMBEA TAIFA KWENYE KANISA LA WESTMINSTER...SWALI KWA NINI HAKUFANYA KWENYE TOWN HALL ? SAFARI HII NAYO YUKO STARI WA MBELE KWENYE HILI LA MISA NYINGINE KANISANI...hebu niambie huoni kama hapo kuna swali la kuuliza?

Hivi kumuombea dua marehemu ni mpaka Kanisani au msikitini tu? huwezi kumuombea dua Marehemu nyumbani kwako?

Kuomba dua mtu unaweza kuomba kutokana na imani yako ndio maana nikasema kuwa kama shughuli ingekuwa ni PRIVATE YA KIFAMILIA huko makanisani sina ugomvi nayo.

Vile vile nikasema kuwa kama shughuli inagharamiwa na SERIKALI na PUBLIC FIGURE kama balozi anapokuwa mstari wa mbele na hiii misa then kuna tatizo katika kuangalia sensitivity za alimia kubwa ya watanzania waliopo UK ambao wengi ni waislam na haswa toka visiwani ambao wangependa kushiriki katisha shughuli hizo lakini wanakuwa wanasita kutokana na udini ulioekwa mbele na Balozi Majaar

Mimi ninaona cha msingi siyo wapi dua imeombewa ,Bali ni kumuombea Mwalimu dua njema na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia kiongozi mzuri kama Mwalimu .

Nakuunga mkono kwenye hili ila siungi mkono serikali kuingiza udini kwenye shughuoi kama hii ya BABA YETU WA TAIFA

Tuache dhana potofu Mwalimu alikuwa ni Mkiristo, kama jinsi viongozi wetu wengine walivyo waislamu, kama serikali inafanya mazishi au hitma ya viongozi wetu kuwatreat marehemu kwa mujibu wa imani zao sioni tatizo

Kwa hiyo kwa maneno hayo hapo juuu kusema Mwalimu alikuwa Mkristo ni dhana Potofu?

Serikali ilitakiwa ifanye inalolijua sikuzote nalo ni kutawala na mamabo ya dini kuwaachia wananchi.Serikali inapoanza kuwa biased na kutulazimisha kuattend shughuli za kidini nadhani ni kinyume na katiba sasa watu kama nying=yi leo hamwezi kutaka marekeshisho ya katiba kwa ku pick and chose.

Mambo ya kuchomana moto,kuzika, kukhitimisha,kusoma misa, ubatizo are not of Governments business

Huyu Balozi angekuwa yuko karibu na watu basi angejua kuwa alitakiwa aandae LECTURE ya kumuenzi Mwalimu kwenye kumbi mbali mbali zilizotapakaa London na kuwaita watu kama Dr SAS au Warioba au wasomi kama akina Hraoub Othman waje kumwaga vitu kuhusu Mwalimu na legacy yake na siyo haya mamabo ya misa makanisani ambayo nadhani ni private na ya kifamilia zaidi

Kesho hao mauditors wa Fofreign wakienda kukagua mahesabu ya Ubalozi wataambiwa nini kuhusu Ubalozi kuandaa misa makanisani kila kukicha?

[=Field Marshall ES;81459]Wakuu mbona nimeona futari imetayarishwa kwenye ukumbi wa Mtakatifu Ann, au?

kama unazungumzia futari ya akina Saidi John na Aly Sungura iliyofanyika kanisa la St Ann basi hilo naweza kukufahamisha kuwa sikuona Tangazo au Mkono wa Balozi kwenye hilo hivyo na swaumi niliyonayo nitakuwa napata dhambi na nitakuwa namsingizia.

Lakini nayo haiondoi ukweli jinsi gani haoa akiana Ali Sungura walivyokuwa out of touch na waislam wa London kwani wapo akina shikh Ayubu, Ustadhi Mohammed Hassan na wengineo ambao wangewa consult ili kupata ushauri zaidi badala ya kufanya mambo kama walivyofanya

Halafu mkuu Barabara, mbona huwa unatokea na ishu za kidini tu na Balozi Mwanaidi, vipi ishu zingine mkuu kama Buzwagi?

Mkuu uzuri wa JF kila mmoj ana ishu zake. Wengine hawatoki kwenye mamabo ya Lugha, wengine wako kwenye michezo, wengine wako kwenye siasa na kadhalika. mimi siwezi kusema niko upande gani ila nadhani upande wangu ni ule unaona walakini katika mamabo mbali mbali na kama waona mie ni upande wa udini basi sawa kwani sidhani kama ni dhambi kulijadili hilo
Halafu Balozi Mwanaidi si ni Mu-Islam, kwani hajui yote hayo mkuu au huyo mama amebadili dini baada ya kuwa balozi?

Naam ni muislam lakini anaweza akawani ni KAFETERIA MUSLIM sasa mamabo ya majina yasikutishe mkuu wangu kwani hata huyo JENERALI ULIMWENGU naye ni musilam vile vile na uliona alivyokuwa nawatukana waislam enzi zake pale Rai?

majina yasikutishe bosi.
 
kama unazungumzia futari ya akina Saidi John na Aly Sungura iliyofanyika kanisa la St Ann basi hilo naweza kukufahamisha kuwa sikuona Tangazo au Mkono wa Balozi kwenye hilo hivyo na swaumi niliyonayo nitakuwa napata dhambi na nitakuwa namsingizia.

Lakini nayo haiondoi ukweli jinsi gani haoa akiana Ali Sungura walivyokuwa out of touch na waislam wa London kwani wapo akina shikh Ayubu, Ustadhi Mohammed Hassan na wengineo ambao wangewa consult ili kupata ushauri zaidi badala ya kufanya mambo kama walivyofanya

Mkuu hii futari imetangzwa karibu wiki nzima kule Michuzi Line, na mpaka imefanyika bila tatizo, I mean kama ninakuelewa vizuri hao kina Ayub na Mohamed ndio wa-Islam haswa huko London, wengine wote sio, maana ni mpaka hao waiunge mkono ishu ya dini hiyo huko ndio itakuwa sawa, wengine wote na wale tuliowaona kwenye picha wanakula futari ni makafiri?

Mkuu huenda una point muhimu katika malalamiko yako, isipokuwa so far labda sijaiona au sielewi, kwa hiyo nitakaa pembeni na hii ishu!
 
=Field Marshall ES;81464]
Mkuu hii futari imetangzwa karibu wiki nzima kule Michuzi Line, na mpaka imefanyika bila tatizo,

Kama unazungumzia tari ya akina saidi John ndio hiyo ilitangazwa kwenye Michuzi na ndio hiyo iliyotapakaa mapicha leo kwenye michuzi blog

Issue siyo tatizo na wala hakuna aliyesema kuwa kufuturisha kuna tatizo

I mean kama ninakuelewa vizuri hao kina Ayub na Mohamed ndio wa-Islam haswa huko London, wengine wote sio, maana ni mpaka hao waiunge mkono ishu ya dini hiyo huko ndio itakuwa sawa, wengine wote na wale tuliowaona kwenye picha wanakula futari ni makafiri?

hakuna sehemu hata moja niliyosema kuwa:

SHEIKH AYUBU na SHEIKH MOHAMMED HASSAN ni waislam haswa London

wala sehemu niliyotaja au sema neno MAKAFIRI

Hivyo naomba urekebishe hapo

Kuhusu hao ma shekhe niliyowataja hapo juu ni watu ambao kutokana na elimu yao pamoja na hekima wanapewa nafasi zaidi katika kutoa ushauri au consultation katika jumuiya ya waislam hapa London na UK kwa ujumla...bila kumsahau of course SHEIKH ISSA

Sasa kama nilivyosema hapo awali issue siyo kufuturu lakini kuna mambo ya watu hawakuuulizwa kuhusu utaratibu ulivyofanyika kuanzania kufuturisha mpaka ukumbi au sehemu yenyewe haswa ukizingatia kumbi ziko nyingi tuuu sasa kwa nini ufuturishe Kanisani wakati Council wanaweza kukupa Ukumbi Bure haswa kwa shughuli kama hizi?

Mkuu huenda una point muhimu katika malalamiko yako, isipokuwa so far labda sijaiona au sielewi, kwa hiyo nitakaa pembeni na hii ishu!

Sasa mkuu hebu rejea katika hiyo thread ya MWALIMU KUFANYIKA MISA KANISANI NA UBALOZI kwani hiyo ndiyo issue iliopo in hand

serikali ishasema haina dini sasa kwa nini inapenda kujishulisha mambo ya kidini? tena kwa kutumia pesa za walipa kodi?

na kama kumbu kumbu mbona hatuoni al Marhum Alhajj Abeid Amani Karume akifanyiwa haya mashughuli?
 
Kwanza naona tumepata kamusi mpya ya kiswahili kuna neno moja linalotumiwa na member moja wa JF kwenye maandishi yake kila mahali. I mean hili neno lina maana gani 'mamabo' mwanzo nilifikiri ni key board na kukosea kuandika lakini naona kila wakati mamabo inajitokeza.

BTW Sasa jibu la swali kwa nini................................blah blah blah............. hivi ulitaka waende kumwombea nyumbani kwako? Haya maneno ya baba yetu wote na porojo nyingine hazina mkia wewe inaonekana una beef na Mama balozi kwa sababu aidha amekata mrija uliokuwa unautumia hapo London ubalozini au unatafuta cheo upewe maana kila wakati huishi kulialia kama mtoto mdogo. Oh mama balozi hivi oh mama balozi vile na mambo lukuki ambayo hayana faida kwa WTZ.

Sasa kama wewe una ushahidi weka hapa facts ni pesa kiasi gani ya walipa kodi ametumia kwa hii shughuli? Halafu wewe andaa hiyo misa/ibada ya kumsomea Karume maana unataka kumlinganisha na Nyerere wakati yeye hakuwa hata rais wa Tanzania, The best he did ni kuwa makamu wa rais.
 
Kwa kweli mimi sijaelewa mheshimiwa analeta au anajaribu kuleta hoja gani hapa forum.Ningeomba ufafanue hapa ni nini hoja na vigezo vyako kuonekana unapinga suala hili.

Kama una maana waislamu hawatakuwa "confortable" kuingia kanisani, mbona hata dada yake yake marehemu Dodi Al Fayed aliingia kanisani kuwaombea marehemu pamoja na Diana Spencer ambao walikuwa wapenzi kabla ya kifo?. Aliingia pale kanisani na yeye ni muislamu ingawa utasema kwamba ile ilikuwa ni "level" ingine.

Licha tu ya kuingia kanisani mle pale Guards Chapel, dada yule aitwae Camilla, pia alisoma vitabu vya "hymns" na kushiriki kusali na wakristo kwa "standard" yake. Pia kanisani mle mlikuwamo waislamu wengine kama Proffesor Sir Magdi Yacoub ambae ni Mmisri na ni muislamu. Proffesor Yacoub ni daktari bingwa wa magonjwa na moyo na mapafu pale chuo cha Imperial.

Sasa tukirudi kwa suala la hayati Mwalimu Nyerere, yeye anafahamika sana hapa Uingereza na sehemu zingine duniani. Kuna watu wengi tu huku Ulaya na hasa UK ambao walikuwa wakifaidi mijadala mbalimbali nae, mijadala ambayo mingine watanzania wenyewe hawakuwahi kufanya nae zaidi ya hotuba za kitaifa,mikutano na waandishi habari na pale mlimani na wasomi.

Halafu hayati mwalimu alianza kuja huku majuu hasa hapa Uingereza tokea kabla ya uhuru mwaka 1952 tu ndio alimaliza shule pale chuo kikuu cha Edinburgh. Hayati mwalimu Nyerere ana marafiki lukuki wakiwamo wanaujamaa wenzie wanaojiita "Fabian thinking".

Inawezekana wakawa ni watu hawahawa ambao labda wameomba wafadhili shughuli hio ama vingine mimi na wewe hatujui kwa kuonesha mshikamano wao kwa kiongozi yule waliemheshimu kwa kile kichwa chake chenye uwezo wa kuona mbali.

Nimalizie tu kwa kusema kwamba hayati Nyerere alifariki akiwa hospitalini London, kwa hio ikiwa hivo basi nafikiri mama balozi yuko "right" kujaribu kuwakutanisha watanzania na raia wengine wawe wazungu au waasia au waafrika bila kujali rangi au dini na yeye mwenyewe akiwa kiongozi kwa kushiriki ndani ya kanisa.

Halafu ndugu, usijaribu saana kuleta suala la imani unapozungumzia dini kwani ni jambo la hatari. Nakushauri uwe unakuwa muangalifu unapojaribu kuleta mijadala kama hii labda unge-"rephrase" hii mada yako.

Kwa hio mimi nafikiri waislamu na watu wa madhehebu mengine wanaweza kwenda katika shughuli hio iwe kanisani au mahala pengine.

Pia watu wa London na miji mingine wanapewa nafasi ya kuhudhuria shughuli hio ingawa mara nyingi tunakuwa "busy" lakini tutajitahidi tuhudhurie.

Kwa nyumbani Tanzania shughuli inaweza kufanyika pale uwanja wa Taifa na labda viongozi wa serikali ya awamu ya nne,wakahutubia na kukiri wamefanya makosa kukumbatia mafisadi na waendekeza rushwa, na hata kutoa tamko rasmi kama la mika ya 80 la kupiga vita wahujumu uchumi lililotolewa na hayati shujaa Edward Moringe Sokoine mpaka kukawa na mtafutano.

Naomba kutoa hoja.
 
A.A. Karume na Mwalimu Nyerere wapi na wapi? ndiyo yale yale ya kufananisha kichuguu na Mlima. Sioni tatizo lolote la misa ya kumuombea Marehemu mpendwa Baba wa Taifa (mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi), kanisani. Kuingia kanisani hakumfanyi mwislamu yeyote kuwa mkristo au kupata dhambi kwa kufanya hivyo. Nimeshawaona waislamu wengi wanaingia kanisani wakati wa ndoa za kikristo au mazishi.
 
...labda kwakuwa alikuwa mkristo na amefariki mkristo, misa itafaa zaidi ikifanyikia kanisani (jumba la ibada)!
 
watu wengine wako kwa ajili ya kupinga kila kitu even if kitafanywa na Mungu...kama waona dini yako ya thamani mno..hujalazimishwa kwenda kaa nyumbani wengine wamuombee...its very bad ku mix udini na siasa..
 
hivin hii misa waislamu tumekatazwa kwenda? mbona futari tuliwaalika na wakristo?
tuache kulalamika kwa mambo yatakayozidi kututenganisha.
 
Hivi kwa nini balozi Mwanaidi anazidi kutafuta lawama?

Nyerere alikuwa baba yetu wote wakristo na wasio wakristo.Hata wakati anaombolezwa tulikuwa pamoja pale uwanja wa Taifa. Lakini leo kwa sababu ambazo anazijua mwenyewe Balozi wetu Bi Mwanaidi Mjaar kaamua kuwaba Babayetu wa Taifa Mwalimu Nyerere aombewe Kanisani lakini sio Ukumbi ambao watu wenye madhehebu mengine wangejisikia comfortable kumwombea dua Mwalimu

Hivi kwa nini wasiandae kitu kama Lecture ya kumkumbuka mwalimu na yale ambayo alitufunza kwenye ukumbi badala ya kujikita kwenye udiini usio na kichwa wala miguuu?

Kama familia ya mwalimu ingeamua kufanya hivyo in private ningeelewa lakini siyo hii ya Ubalozi na Balozi kuendelea na mchezo wao wa kibaguzi

Balozi mwanaidi hivi kwa nini unatumia back door kuwabagua watu ambao ulitakiwa uwawakilishe bila kuangalia mitazamo yao ya kidini?

Na zaidi ya hayo mbona hajafanya Juhudi za kumsomea Al haj Abeid Amani Karume hicho kisomo?

You would have thought Balzi ambaye ni lawyer by profession angejua a trade vipi kwenye mambo haya
Asomewee kwenuuu
 
Back
Top Bottom