Kwanini Nyerere aliongoza kugomea bidhaa za Afrika ya Kusini wakati wa makaburu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Nyerere aliongoza kugomea bidhaa za Afrika ya Kusini wakati wa makaburu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Feb 22, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Feb 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Tanzania na nyingi za kusini mwa Afrika ziligomea kufanya biashara na Afrika ya Kusini kwa muda mrefu sana. Wangeweza kupata bidhaa nyingi na za kisasa na hata wafanyakazi kutoka Afrika ya Kusini. Lakini Nyerere pamoja viongozi wengine waliongoza harakati za kukataa kununua bidhaa za Afrika ya Kusini na baadaye harakati zao zikajakuungwa mkono na mataifa ya kimagharibi. Ninajiuliza hata hivyo:

  a. Nyerere alikuwa anawaza nini kuacha wananchi wake wateseke kwa kununua bidhaa kutoka mbali na ghali wakati za Afrika ya Kusini zilikuwa karibu na rahisi?

  b. Kwanini Watanzania hawakuona tatizo kugomea kufanya biashara na Afrika ya Kusini wakati utawala wa makaburu bado uko madarakani?

  c. Je kuna lolote viongozi wetu wa sasa wanaweza kusimamia kukataa kufanya biashara na makampuni ya kifisadi?

  d. Je wananchi wa Tanzania bado wana ujasiri wa kuweza kuvumilia usumbufu wa muda au ndio tumekuwa taifa la legelege ambao hatuwezi tena kufunga mikanda? (kama mikanda yenyewe ipo).
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Labda kabla ya kuanza kujibu maswali yako, ni vema tukafahamu kwa kina ishu hii, kwamba Je Afrika ya kusini iliathirika kwa namna yoyote na Ugomeaji huo?...au labda kwa lugha ingine, Je lengo la ugomeaji la Nyerere et al lilitimia?...Did S.Africa yield?
  Tuendelee!
   
 3. l

  limited JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 300
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  nyerere alikuwa mzalendo na alikuwa hatakikuwa tegemezi(omba omba) wa kununuliwa kirahisi he was mjamaa, kuhusu viongozi wa sasa hivi hawawezi watakachokuambia ni soko huria(ambalo hawajui hata maana yake) na ubinafsi na rushwa imejaa kwa viongozi wetu.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Feb 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  absolutely; na hadi inaelekea mwishoni mwa miaka ya themaini na mwanzoni kiburi cha Afrika ya Kusini kilishindwa kuhimili kwani kampeni iliyoanzishwa mwishoni mwa miaka ya hamsini na Nyerere na wenzake ilipamba moto kwani ilikuja kuwa kampeni kubwa ya wasomi na vijana duniani. Ilichangia kuipigisha magoti Affrika ya Kusini ya makaburu.
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hapo ndipo penyewe sasa!

  Mimi binafsi nilipata kushuhudia, japo kwa muda mfupi, enzi za Uzalendo wa kweli wa wananchi wa Tanzania!
  Wakati huo serikali ilikuwa inaheshimiwa sana, maana ilikuwa ni utawala wa watu kwaajili ya watu, na hivyo amri yoyote ya serikali ilishuka chini kwa impact yote iliyotarajiwa!
  Lakini zaidi sana ni kwamba cha kushangaza, wananchi wenyewe walikuwa na roho za kujitoa sana na hapakuwa na chembe ya ulalamishi wala kinyongo(angalia mfano responce ya wananchi kwenye vita ya Uganda).
  Hivyo, kwa aina ya waTanzania wa wakati ule, walikuwa tayari kufanya lolote ili mradi nia ilikuwa kuleta usawa na haki kwenye sehemu fulani ya dunia au Taifa...na hivyo kutekeleza agizo la kugomea bidhaa za S.Africa ilikuwa ni ushujaa, na watu hawakungoja kusimamiwa kutekeleza hilo.
  Uhovyo wa serikali za sasa hivi umekwangua UZALENDO, na hatutaona tena utu wa wakati ule.
   
 6. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #6
  Feb 22, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Nyerere alikuwa principled sana; hakuwa tayari kushirikiana na dhalimu yoyote, na wala hakuwa tayari kumpigia magoti dhalimu yeyote. Mojawapo ya principle yake ambayo ninaiheshimu hata leo ni kuwa ni "afadhali uwe fukara wa mali kuliko kuwa maskini wa mawazo." Principle hiyo ilikuwa inamzuia kujikomba au kumtumikia dhalimu yoyote kwa ajili ya mali. Makaburu walikuwa dhalimu ambao yeye alitaka kuwabana hadi watoe uhuru kwa walio wengi huko bondeni. Pole pole lakini alifanikiwa ukizingatia kuwa nchi zote za kusini zimepata uhuru wako kutokana na msimamo huo wa Nyerere: kumbuka Zimbabwe, Msumbiji, Angola, Namibia na Afrika ya Kusini zote zimepata uhuru kwa mabavu hayo ya Nyerere.

  Kwa wanaokumbuka mwaka 1965, baada ya muungano, Ujerumani Magharibi ilimwambia Nyerere awaondoe Ujerumani Mashariki kutoka Zanzibar ambapo walikuwa wamealikwa na Babu. Nyerere alipokataa wakamtishia kuwa watamnyima misaada, siku hiyo hiyo akawambia fungeni misaada yenu muondoke; na kweli Ujerumani magharibi walibomoa barabara walizokuwa wameshajenga pale Dar, akawaambia wachukue hata sindano zao, wakaondoka. Mwaka 1965, kulikuwa na jamaa mmoja aliyekuwa afisa wa ubalozi wa Marekani anaitwa Caruci, ambaye alikuwa ameshiriki kumwua Lumumba, aligunduliwa kuwa na njama za kutaka kumwua Babu au kumchonganisha Babu na Karume; njama hizo zilipogundulika ubalozi wa marekani ukafungwa. kwa muda mrefu chini ya utawala wa Nyerere hatukuwa na ubalozi wa Marekani na Ujerumani Magharibi.

  Baada ya kumjua kuwa ni mtu principled, walikuwa wakiongea naye kwa uangalifu na kwa adabu. Hata kule kukataa masharti ya IMF miaka ya sabini hadi themanini kulitokana na jeuri hiyo hiyo. It is possible kuwa kulikuwa na madhara yake kwa wanachi lakini bado ninaona kuwa ilikuwa ni vizuri kwa Taifa kuwa na identity yake badala ya kuendeshwa na watu wa nje kwa ajili ya mali.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Feb 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kichuguu, vizuri sana kutukumbusha huko nyuma. Nyerere alikuja kuheshimika sana na akawa sauti ya reason katika bara la Afrika hata nje. Wazungu (kama watu wengine walivyo) wanakawaida ya kumheshimu mtu mwenye msimamo na msimamo unaoongozwa na dhamira. Lakini hawawezi kumheshimu hadi pale watakapomjaribisha kuona anaweza kuhimili au vipi.

  Nilikuwa napitia makala yake ya kwenye Observer ya London (1959) akielezea msimamo wake huo ambao alitoa ile famous quote "to vote South Africa in, is to vote us out".. Na matokeo yake Afrika ya Kusini ikajitoa kuomba uanachama wa Jumuiya ya Madola.
   
 8. Companero

  Companero Platinum Member

  #8
  Feb 22, 2011
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkuu lakini bado alifanya biashara ya almasi na De Beers pale Mwadui pengine ndicho viongozi wetu wa leo walichojifunza kwake!
   
 9. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #9
  Feb 22, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu ila haya mawili bila kubadili attitude ya wabongo its practically impossible!
   
 10. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #10
  Feb 22, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Ndiyo, pressure ilisaidia sana South Africa kutengwa na ulimwengu. Kaburu akasalimu amri.
  Nyerere alipinga msimamo wa Israel dhidi ya wapalestina, Waisrael walikokuwa wanatusaidia wakasitisha misaada yao. Moja ya miradi walioyukuwa wanataka kuianzisha ni huu wa kuvuta maji toka Victoria hadi Dodoma.
  Hata pale tulipotoka kwenye vita na mpaka wetu kuwa umefungwa na Kenya, msimamo wa Nyerere ulikuwa ule ule,afadhali imperial soap itoke europe kuliko Kenya. Tukaanzisha mashirika yetu ya ndege,reli, bandari n.k. Hii ndiyo inatupa kiburi hadi leo ndani ya EAC kuwa tunaweza bila msaada au kumtegemea mtu.
  Somo: Kiongozi msafi anachukua maamuzi magumu kwa manufaa ya taifa lake. Kiongozi hapati heshima kwa kunyenyekea matajiri bali umma uliomwamini. Kwamba pesa itanunua kila kitu isipokuwa utu na heshima ya mtu.
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Feb 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  ur probably right lakini bidhaa ilikuwa ni yetu... nlisema alisusia bidhaa za Afrika ya Kusini.
   
 12. popiexo

  popiexo JF-Expert Member

  #12
  Feb 22, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 743
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Msimamo wa Nyerere ulikuwa thabiti, na hakuweza kumnyenyekea mtu kwa sababu ya nguvu au utajiri wake ila kwa hekima na busara, hiki ndio viongozi wa leo walipaswa kukiiga. Kipengele C ktika hoja yako na sema kwa sasa hatuna kiongozi anayeweza kusimama na kwepingana na watu wenye nguvu au utajiri/mafisadi. Viongozi wetu sasa wamewekwa mifukoni mwa mafisadi, either kutokana na tamaa na ubinafsi or kukosa uzalendo kwa nchi yetu.
   
 13. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #13
  Feb 22, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nadhani pia umefika wakati serikali yetu ikatae kufanya biashara na nchi zinazouza bidhaa fake kama Uchina. Ninaamini huu nao ni ufisadi uliokomaa kwani unaongeza umasikini kwa Watanzania ambao tayari ni maskini.
   
 14. zaratustra

  zaratustra JF-Expert Member

  #14
  Feb 22, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 849
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Mkuu serikali haifanyi biashara fake na Uchina, ndo maana tuna vifaa vingi vya kichina vinatumiwa na Jeshi letu la Ulinzi (TPDF). Wanaofanya biashara fake ni wamachinga wa kichina na wajasiriamali wetu, ambao wananunua bidhaa za bei rahisi ambazo kama nilivyosema vinatengenezwa na wamachinga wa kichina (LABDA kwetu tungesema SIDO)! Kumbuka hata mmarekani ana-muhara mchina kwa ubora wa bidhaa zake! Kitu (bidhaa) cha kichina ambacho hapa bongo unaweza kukipata kwa sh. 2,000/- hadi 5,000/- Ulaya au Marekani kinauzwa bei zaidi ya hiyo (kwa kulinganisha), maana kule zinapelekwa bidhaa ambazo ni First Category! Kwetu zinaletwa..............! I stand to be corrected and criticized!!
   
 15. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #15
  Feb 22, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Kwanini Watanzania hawakuona tatizo kugomea kufanya biashara na Afrika ya Kusini wakati utawala wa makaburu bado uko madarakani?

  Among other things nafikiri hii - APARTHEID ndo ilikua kubwa zaidi....... Viongozi wa sasa hawa akina JK, RA, EL, AC etc..... they represent the true corrupt, opportunistic, egoist, etc leaders who are there their personal/group interests rather than more than 40mil Tanzanians. Wanajulikana kwa njia wanazoingia madarakani, wapambe wao, etc.....

  Uhitaji wa uamsho wa Watanzania ni mkubwa sana..... ona AR last week wanasema waanze na kusambaza katiba.... nearly 50 years of independence, more than 70% of Tanzanians live in rural areas with less access to basic social services and needs and so hata katiba yao hawaijui....... Kimsingi kama wanajua ni haki yao kupata hizi huduma, with this ICT, the playing field is getting flattened than thought. Think of what happened in the last general election.. last October...... Hatuhitaji kutumia nguvu nyingi sana, kufanya walichofanya our Brothas in Tunisia, Egypt etc.... People are tired, we're really tired... and the indicators are so clear that changes are bound to come, come what may.....
   
 16. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #16
  Feb 22, 2011
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  "If you don't stand for something, you will fall for anything"
   
 17. F

  Felister JF-Expert Member

  #17
  Feb 22, 2011
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Attitude ya watanzania inasikitisha; mafanikio ya mtu hayapimwi tena kwa uadilifu wake bali pongezi zinaenda kwa wale wanaoweza kukwepa sheria na kutumia mabega ya wengine kufikia malengo yao hata kama itamaanisha kumwaga damu .....Sad! Hakuna incentive ya kuwa mwadilifu Tanzania; maana waadilifu wote ni maskini, wasio na sauti na wasio na majina makubwa yenye kupewa heshima. Wakizungumza hakuna anaewatazama na wanaonekana wamepitwa na wakati maana tuko kwenye siasa ya ubeberu maana hata ubepari unaheshimu rule of law.

  Asante MM kutuletea topic inayotuwezesha tuweze ku reflect back na kuona ni wapi tunaenda.
   
 18. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #18
  Feb 22, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Na si hivyo tu, bali ni kwamba ule mktaba wa De Beers ulisainiwa miaka mingi kabla ya uhuru.
   
 19. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #19
  Feb 22, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Kwa viongozi tulionao hawawezi wakasema jambo na ukawaamini.

  Nyerere alijenga kuaminika ndani ya jamii yake na ndio maana watu walimfuata kila alipotoa msimamo fulani.
  Sasa leo kiongozi kama JK akisema serikali haina uwezo wa kutoa huduma kwa kina mama wajawazito nani atamwamini wakati analisema hilo ni jana yake tumemwona kwenye bembea Jamaica?

  Hata vyama vya upinzani, ukiondoa maandamano ya Jan 5, 2011 mjini Arusha ni maandamano yapi yaliyoitishwa na viongozi wa vyama na ukawaona wako front line wakipigwa mabomu. Nani atawaamini tena kesho???

  Kina Nyerere na wenzake walikuwa na DIRA na MAONO ya Tanzania waitakayo hata kama hawakufikia malengo kwa 100%.

  Kama kiongozi hajui kwa nini nchi yake ni maskini kwa nini umtarajie KUUONDOA huo UMASKINI?
   
 20. T

  Topical JF-Expert Member

  #20
  Feb 22, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wewe na Nyerere bana? haikutosha kumfanya mtakatifu mkuu?

  Principle bila akili ni ugonjwa...

  Nyerere principle zake zinatusaidia nini sisi watu wa chini? au ndio tukose sabuni ili kupata umaarufu...? hana lolote

  Nyerere ni mkuu wa jukwaa ukimpa jukwaa anaweza kupendezasha hadhira yake lakini utekelezaji ..nil.
   
Loading...