Kwanini Mwalimu Nyerere aling'oa reli ya Dar-Lindi, Mtwara, Nachingwea?

Reli ilijengwa mpaka Masasi(sio Tunduru) kwa jili ya mradi wa kilimo cha Karanga ili kutengeneza Mafuta ya kula Uingereza

Ni kweli reli iliyojengwa ilikuwa kwa ajili ya mradi wa kilimo cha karanga ambacho wakati huo ulikuwa muhim sana kwa ajili ya mafuta ya kula kama ambavyo safari_ ni_ safari alivyosema, lakini ilikuwa ni kutoka Mtwara hadi Nachingwea ambapo nyakati hizo Nachingwea ilikuwa kituo kikubwa cha kilimo na biashara nyingine za wanyama pori
 
Labda "kila mtu" ana ugomvi na mimi! Inabidi nianze kutafuta marafiki maana maadui nilio nao wanatosha kubakia maisha yangu yote.




To tell you the truth haijalishi nani anakuja; walioondoka waliletwa na serikali ya CCM na wanaokuja wataletwa na serikali hiyo hiyo sasa hatuna ujanja isipokuwa kuibana serikali hii hii. Au wewe huoni kuwa ni suala la serikali ya CCM na sera zake ndio vinahusika na hii reli?


Saa zingine si haba ukawa na marafiki wengi kuliko maadui...afterall the fewer enemies you have the better ndio siri za maisha hizo mkulu

sasa ukitazama sera za the alternative party hawanajipya zaidi ya copy and paste sera hiyo hiyo ya CCM maana hata mentality zao ni kama za CCM kwa sababu wametokea huko huko CCM .

kisha wanajiuliza iweje watu hawana interest na siasa...its simple siasa ndio inafanya watu kuwa bize zaidi JF kuliko chochote kile
 
_MG_0094.JPG


_MG_0225.JPG
Ha ha haa! Mzee, imekuchukua zaidi ya miezi miwili kurudi na hizi pics!!! Hivi haiwezekani ukabadilisha hiyo heading? Au ni sawa kutumia uongo kumlaumu mtu? Reli Dar - Lindi???
 
Tatizo leno Chadema whatever Nyerere did was right, whatever Mkapa did was right lakini Kikwete na Mwinyi hapana. Kwenye hesabu zamani tulikuwa tunaziita step function

Its high time Chadema muanze kuamua moja kama mna attack CCM kama chama mshambulie chama au kama mna attack Personalities basi mjue chama chenu kitakufa maana tomorrow there is no Kikwete but CCM will be there!!!!
Hivi hizi Chadema ziko ngapi??? Chadema hawahawa wanaomtaja Mkapa kwenye kundi la mafisadi ndio haohao wanaoona whatever Mkapa did was right au kuna wengine???
 
Reli hii iliyozinduliwa mwaka 1953 haikufika Masasi, ilitoka Mtwara hadi Nachingwea Mkoa wa Lindi katika mashamba ya Karanga ya wakoloni. Mashamba haya hayakuzalisha kama ilivyokusudiwa yakatelekezwa na wazungu wakakimbia katika kukaribia uhuru. Plale Nachingwea kulikuwa na mashamba makubwa yanajulikana kama "Farm One (1) hadi Farm Seventeen(17). Kwa wale waliofuatilia historia ya ukombozi wa Afrika, Kambi ya wapigania ukombozi kama vile FRELIMO, ZIPA walikuwa pale Farm 17.
 
Wanajamii, hapajawahi kutokea reali kati ya Dar mpaka Mtwara. Hata wale wanaosema kuwa reli ilitoka Mtwara mpaka Masasi sio kweli. Ukweli ni kuwa Reli ilitoka Mtwara kupitia Masasi mpaka Nachingwea. Dhumuni kubwa la mkoloni ambaye aliijenga reli hii ni kutokana na mpango wao wakoloni wa Mradi wa kilimo cha Karanga kule maeneo ya Ruponda, Nachingwea. Kwa bahati mbaya, kilimo hicho hakikufanikiwa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyosababisha kilimo cha karanga kutokubali kama walivyopanga. Hata hivyo walionyesha nia ya kuitumia reli hiyo kwa ajili ya kusafirisha zao la korosho lakini mipango yao iliingiliwa na harakati za uhuru, hivyo walisitisha rasmi mradi huo mwanzoni mwa mwaka 1961. Sasa baada ya nchi kupata uhuru, ndio serikali ya awamu ya kwanza iliposhindwa kuendeleza pale walipoishia wakoloni, badala yake ikang'oa hiyo reli na kwenda kuunganisha katika kipande cha reli ya kati mkoani Tanga. Kwahiyo kama viongozi wangeona mbali, hakukuwa na haja ya kung'oa nhiyo reli sababu umuhimu wa reli unaenda sambamba na barabara na leo tunaona umuhimu wa kuwa na reli kule kusini. Kwa wasiofika hawajui ninachosema lakini waliofika watanielewa. Hiyo niyo habari kamili.
 
Safari umenena!!! Hakujawahi kuwa na reli kati ya NTWARA na DAR!!! Na hiyo ya Mtwara Masasi iling'olewa namkoloni kwa kukosa TIJA..Haikulipa (tukitumia kiswahili cha biashara ya kimtaa)
 
Picha hizo kwa Ihsani ya issamichuzi.blogspot.com la taarih 26 May 2011.

Kuna Mdau hapo imeweka picha hizo kuonyesha mpaka leo mataruma ya hiyo Reli yapo.

WaTanganyika mnangoja nini kufufua reli hiyo?
 

Attachments

  • _MG_0225.JPG
    _MG_0225.JPG
    548.4 KB · Views: 106
  • _MG_0094.JPG
    _MG_0094.JPG
    407.7 KB · Views: 78
resize_image.php


Hili ni jambo ambalo ukimuuliza Nyerereist yoyote hatokupa jibu

Mindhali humu kuna GREAT THINKERS naamini tutapata data tuu kwa nini the so called baba wa taifa alimua hii reli ingolewe

Nawasilisha

Kwanini toka Kikwete ameingia madarakani, shirika la Reli linaelekea kufa?
Kwanini toka mwaka 2006 , hakuna treni zinazokwenda Kilimanjaro/ Arusha?
Kwanini wakati wa Kikwete shirika la ATCL alilikuta na ndege kadhaa ,sasa halina hata moja?
Kwanini wakati wa JK Bandari zetu zinatetereka na upakuzi mizigo umepungua kwa kasi?

Ukijibu haya maswali , tutakujibu hilo lako....
 
resize_image.php


Hili ni jambo ambalo ukimuuliza Nyerereist yoyote hatokupa jibu

Mindhali humu kuna GREAT THINKERS naamini tutapata data tuu kwa nini the so called baba wa taifa alimua hii reli ingolewe

Nawasilisha

Sasa hii ramani ni ushaidi wa kuwepo reli na kung'olewa? Weka ramani ambayo inaonesha kuwepo kwa reli hiyo!
 
Reli ilikuwa inatoka Mtwara kwenda Masasi,nadhani wewe unaelimu ya madrasa its better ungeenda kupata elimu dunia ili uweze kupambanunua vitu
 
Nadhani hakukuwa na mjadala wowote kuhusu uwepo wa "reli Mtwara".. mjadala ulikuwa kwenye reli iliyong'olewa na ushahidi wa hizi picha unaonesha kuwa reli haziikung'olewa bado zipo. Swali ni kwanini Serikali ya CCM haijatengeneza hizi reli na kuunganisha Mtwara na Dar-es-Salaam?

SR, inabidi tuwabane hawa watu watoe majibu maana kati ya masuluhisho ya kuunganisha kusini na Kaskazini ni ujenzi wa reli hiyo.. ila sijui inaweza kupita wapi sijaangalia topografia na jiografia ya eneo hili.

Hapana MM!
Reli imeng'olewa na madaraja yamebomoka pia (sehemu ambazo kulikuwa kunapita mito midogo) kama vipo basi ni vipande vifupi tu..nimeshawahi kusafiri kwa gari kati ya Mtwara-Masasi na Lindi-Nachingwea mara kadhaa,kwa hiyo ninachosema nakifahamu,sehemu kubwa ilipopita hiyo reli nimepita kwa gari,nikiri kuwa sijapita sehemu yote...Ila kama ulivyosema ni muhimu hiyo reli kurudishwa na hatimaye kuunganisha kusini na kaskazini kwa maendeleo ya nchi yetu,tunaidai serikali kwa hilo.
 
Nimewahi kusikia kuwa kabla ya uhuru wa Tanganyika kusini mwa Tanzania Mkoa wa Mtwara kuliwahi na Railway line iliokua inaunganisha Mtwara na Wilaya ya Nachingwea. Aiadha mara baada ya uhuru wa Tanganyika serikali ya Mwalimu ikaamua kung'oa reli hiyo na kwenda kujenga reli ya Dar/Moshi.

Kwa ufahamu wangu naamini kuwa wazungu (wakoloni) walioamua kujenga reli hiyo walikua na madhumuni yao kwa mikoa ya kusini mwa Tanganyika.

Lakini mpaka hivi sasa sijui kwa nini Wazungu waliamua kujenga Reli kusini na Kwa nini serikali ya Mwalimu iliamua kung'oa reli hiyo?........Naomba wan jf kwa yeyote ambae ana ufhamu mzuri kuhus hili basi anifahamishe na mimi niongeze ufahamu wangu.....nawakilisha.
TRAIN-NACHINGWEA_site.jpg
 
Tanganyika 1, naomba nikuweke hili dokezo nilizonami, kisha linganisha na unachokijua...... then utaangali mwennyeweeeeee

1.1 Construction History
The history of the railways in Tanzania dates back to the German colonial era, when in the early 1880s' the first ever railway line in East Africa was built by the Germans from Tanga. The line reached Mombo in 1904 and finally reached Moshi and Arusha in 1911 and 1929 respectively. The branch line to connect with Kenya reached Taveta in 1924.

The Central Line started to be laid at Dar es Salaam in 1905, reaching Morogoro in 1907 and finally reaching Mwanza in 1926. The branch from Tabora to Kigoma was laid in 1912, reaching Kigoma in 1914. The Central line was connected to Tanga line in 1963.

The Chinese built 1860 km Cape Gauge (1067mm) TAZARA was constructed in a record time of 5 years from the port of Dar es Salaam to New Kapiri Mposhi, in Zambia between 1970 and 1975.
 
Tanganyika 1, naomba nikuweke hili dokezo nilizonami, kisha linganisha na unachokijua...... then utaangali mwennyeweeeeee

1.1 Construction History
The history of the railways in Tanzania dates back to the German colonial era, when in the early 1880s’ the first ever railway line in East Africa was built by the Germans from Tanga. The line reached Mombo in 1904 and finally reached Moshi and Arusha in 1911 and 1929 respectively. The branch line to connect with Kenya reached Taveta in 1924.
The Central Line started to be laid at Dar es Salaam in 1905, reaching Morogoro in 1907 and finally reaching Mwanza in 1926. The branch from Tabora to Kigoma was laid in 1912, reaching Kigoma in 1914. The Central line was connected to Tanga line in 1963.
The Chinese built 1860 km Cape Gauge (1067mm) TAZARA was constructed in a record time of 5 years from the port of Dar es Salaam to New Kapiri Mposhi, in Zambia between 1970 and 1975.
Well said mkuu!suala la kubomolewa kwa reli lilikuwa haliniingii akilini hata kidogo!
 
Back
Top Bottom