Kwanini Nyerere alikataa wazungu kuchimba madini na kuwa tofauti nao kabisa?

Sideeq

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
2,422
433
Mara kwa mara tunasikia "ushujaa" wa Nyerere kuwapinga Wazungu kama vile kuwakatalia kuchimba madini kwa madai ya kuwa alikuwa akihifadhi rasilimali za nchi hii kwa vizazi vijavyo na alikuwa akipingana nao sana kutokana na uzalendo wake.
Nimeangalia upande wa pili na kupata kuelewa kuwa Nyerere hakufanya vile kutokana na kulinda rasilimali za Taifa au uzalendao bali ni chuki zake binafsi kwa Wazungu baada ya kumtumia na "kumtosa". Ikumbukwe kuwa Tanganyika ilikuwa ni kati ya nchi zinazoongoza kwa kupokea misaada mingi kutoka nchi za Magharibi mara tu baada ya Uhuru, na Nyerere alikuwa akiipokea hii misaada lakini alichokuwa hakijui ni kuwa Wazungu walikuwa wakimtumia ili kuipata Zanzibar (Muungano), mara baada ya Muungano kufungwa na wazungu kupata walichotaka Nyerere akaachwa peke yake, hawakuwa na haja naye tena.
Hii ilimuuma sana Nyerere na kuhakikisha kuwa Wazungu hawatapata dili yoyote wakati wa utawala wake na hatokubali misaada kutoka kwao ila kama kuna ulazima wa kufanya hivyo.
Mwenye kutaka ku refute anakaribishwa lakini tuondoeni jazba, ushabiki na matusi.
Pia ninamuomba mod atuachie huu uzi kwa sababu kuna controvesial nyingi sana zinazomzunguka Nyerere, hivyo huu huenda ukawa ni wakati muwafaka wakumchambua.
Nawasilisha.
 
Mara kwa mara tunasikia "ushujaa" wa Nyerere kuwapinga Wazungu kama vile kuwakatalia kuchimba madini kwa madai ya kuwa alikuwa akihifadhi rasilimali za nchi hii kwa vizazi vijavyo na alikuwa akipingana nao sana kutokana na uzalendo wake. Nimeangalia upande wa pili na kupata kuelewa kuwa Nyerere hakufanya vile kutokana na kulinda rasilimali za Taifa au uzalendao bali ni chuki zake binafsi kwa Wazungu baada ya kumtumia na "kumtosa".


Huu ni uzushi wa hali ya juu kuhusu Nyerere. Tuangalie migodi miwili mikubwa; Kahama Mining (Bulyanhulu) na Mwadui diamonds.

Mwadui Diamonds, kipindi chote cha Nyerere hiza za serikali zilikuwa 49% ,na wawekezaji 51%. Nyerere aliona hili kuwa na maslahi kwa Taifa, japo alitaka Tanzania iwe na 51%. Baada ya Nyerere kuondoka, japokuwa huu mgodi haukuwa na tatizo lolote, Mkapa akakubali Tanzania iwe na 15% na muwekezaji 85%. Angalia kwamba, kwa kipindi chote Tanzania ikiwa na hisa nyingi za 49%, muwekezaji, ambae ndiye aliendesha mgodi, aliamua kujenga uwanja wa ndege pale mgodini, ambao pia ulitumika kwa ndege za mgodi na za kibiashara (commercial flights). Mara baada tu ya muwekezaji kuchukua 85%, alitangaza kufunga uwanja wa ndege ili eneo la uwanja lichimbwe almasi. Ikaja julikana kwamba lile eneo lililokuwa uwanja wa ndege ndilo liliokuwa na utajiri mkubwa wa almasi kuliko maeneo mengine yote ya mgodi! Wenye akili tukajua tumefungwa goli la dobo.

Bulyanhulu: Waliofanya utafiti wa dhahabu walikuwa ni Placer Dome, kampuni toka Canada kama sikosei. Barrick wa sasa walikuja kununua huu mgodi baadaye kabisa. Sasa Placer Dome walipogundua wingi wa dhahabu hapa, miaka ya 1970, walitengeneza proposal ambayo share za Tanzania zingekuwa chini sana ya 50%. Nyerere akakataa katakata, akasema, sana sana, atakubali share za Tanzania ziwe 51%. Placer Dome wakakataa, wakadai basi Tanzania ichukue 49% wao ndio wawe na 51%, kwa kuwa gharama za exploration pia zilikuwa zao. Nyerere akawaambia sikilizeni, kama hamtaki Tanzania tuwe na 51% basi ondokeni, kwa sababu hiyo dhahabu huko ardhini haitaoza. Hata tusipoichmba sisi iko siku watoto wetu wataichimba, kwa sababu wakati huo nao watakuwa na utaalamu wa kufanya hivyo. Placer Dome wakaondoka wakiacha vibanda vyao vitatu pale Bulyanhulu.

Alipokuja Mkapa, akautoa Bulyanhulu kwa wawekazaji kwa Tanzania kuchukua wastani wa karibu asilimia 3% (tatu), wakati Nyerere alikataa 49%! Mkapa akasema Tanzania tutafaidika na kodi ya mauzo ya dhahabu!

Kumbuka kwamba hata Placer Dome walipoona mgodi walioufanyia utafiti unapewa mtu mwingine na serikali walienda mahakamani kudai mgodi wao, lakini kama ilivyotarajiwa na wengi, walishindwa hiyo kesi.

Sasa niambie, kosa la Nyerere hapa ni nini? Kusimamia maslahi ya Tanzania?
 
Thibitishiwa kama alitumiwa na akatupwa....wanaotumiwa si hawa wanaopewa suti na ada za watoto zao ili wagawe rasilimali za Tanzania?
 
Nyerere alikuwa mzalendo wa kweli. Hawa wengine ni wachumia tumbo tu...
 
Nyerere alikuwa mzalendo wa kweli. Hawa wengine ni wachumia tumbo tu...

Nyerere alikuwa ni kiongozi wa pekee sana, nashangaa mtoa mada anavyosema. Sasa hivi viongozi tulionao ni majizi makubwa na majambazi ya kutupwa, ila namini siku moja nitaiona tanganyika yangu kabla sijaingia kabulini.
 
Wewe ulieanzisha hebu preview then utagundua makosa yako mwenyewe, MZUNGU, NYERERE,TANGANYIKA, ZANZIBAR, MUUNGANO...TANZANIA. Hah ivi hata kidato cha pili umefika wewe?

Hebu lete conection ya Mzungu na Zanzibar waliitakia nini wakati ule na hata leo?
Ngoja nikuagizie halua na gahawa.....
 
mwalimu alitaka madini ije kuwanufaisha watu wote kwa kuwa hayaozi hakuwa haraka ya kuyahomola na kubakisha mahandaki kama sasa ilivyo maeneo mengi yenye utajiri mkubwa wa madini ni aibu hata huduma za msingi ni tatizo hatunufaiki kwa kiwango alichotarajia mwalimu.
 
Back
Top Bottom