Kwanini NSSF isiwe na tawi la bank kusaidia wateja wake?

ZALEMDA

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
1,647
1,885
Mikopo ya bank muda mwingi haisaidii sana watumishi wa umma au sekta binafsi kwa sababu ya riba kubwa.

Sasa kwa sababu watumishi huwa ni wateja wa kudumu wa mfuko huu na kila mwezi wanachangia fedha nyingi, kwa nini NSSF isiwe na bank ambayo itatumika kuwapa mikopo wateja wake kwa riba ndogo sana ili kuboresha kipato cha wateja wake?

Asanteni
 
Hakuna kischowezekana kama mipango ingekua hivyo ila kila chombo kina majukumu yake. Pension funds wana wajibu na kazi zao na banks wana wajibu na kazi zao.
Hizo bank Nyengine watawakopesha wafanyabishara na watu wengine lakini Bank ya NSSF ni kwa wafanyakazi tu. Nakwambia wakifanya hivi Maisha ya wafanyakazi yataboreka vizuri sana.
 
Jukumu Lao ni lipi sasa kama hawawezi kuboresha Maisha ya wateja wake na kukuza uchumi wa nchi kwa kutoa mikopo nafuu kwa wateja wake?
Kama ni kutoa mikopo hata hizo bank zinaweza kutengenezewa mfumo nimefanya hicho mtoa maada anachotamani. Ni swala la maboresho kwa maendeleo tuu
 
Hizo bank Nyengine watawakopesha wafanyabishara na watu wengine.lakini Bank ya Nssf ni kwa wafanyakazi tu.nakwambia wakifanya hivi Maisha ya wafanyakazi yataboreka vizuri sana
Nadhani kuwa na product ya watumishi wenye pension nssf kwenye bank ni rahisi pia kuliko kufungua bank mpya ya nssf
 
We
Kama ni kutoa mikopo hata hizo bank zinaweza kutengenezewa mfumo nimefanya hicho mtoa maada anachotamani. Ni swala la maboresho kwa maendeleo tuu
Wewe unafikiri bank hizi za biashara zina moyo huo wa kuwarumia wafanyakazi kwa kuwapa mikopo nafuu wafanyakazi?

Nikupe mfano mzuri wa NHIF,wanakopesha madawa na vifaa kwa hospitali .nakwambia riba yap ndogo sana kiasi kwamba unajisikia raha mstarehe.
 
Kwa hoja yako ni kwamba hiyo NSSF ikifungua benki yake kuwasaidia haitakata makato standard kama ya benki zingine?

Una wazimu nini wewe?

Yaani ajenge benki eti halafu akusamehe costs za kibenki?Halafu benki aendeshe kwa mkojo wako?

Haya Matanzania yanayokaa kila siku kutaka misaada kama hivi ni upumbavu,maana wewe unataka upewe huduma bure bila makato,hayo makato alipie nani?

Inatakiwa viongozi wetu na mashule yetu yafundishe watu kufuta hii notion ya utegemezi na kupenda vya bure on expense on others.

Halafu NSSF ni shirika la bima,biashara ni bima,eti unataka kuipa kazi ya benki tena as if hakuna mabenki special kwa ajili ya kazi za kibenki?

Halafu jitu kama hili linakuja kua kiongozi au mbunge na thinking mbovu namna hii
Sidhani kama umenielewa nilichokiandika .kabla ya kuropoka ulitakiwa usome kwanza.

Nimesema bank hiyo ingeweza kutoa mikopo nafuu kwa wateja wake.sijasema mikopo bure.tumia akili kujibu hoja
 
Back
Top Bottom