manwest1
JF-Expert Member
- Apr 25, 2014
- 225
- 134
Nilikuwa katika ajira kwa muda wa miezi 17. Katika muda huo wote nilikuwa nachangia mfuko wa NSSF kwa mujibu wa sheria. Mwezi wa tatu mwaka huu tulipunguzwa kazi kutokana na Covid 19.
Nilijaza fomu za NSSF ili niweze kupata hela yangu iliyopo huko nianze biashara. Niliambiwa kwakuwa nimefanya kazi miezi 17 nitaanza kwakulipwa asilimia 50 (50%) ya hela iliyopo NSSF. Nililipwa hiyo asilimia 50.
TATIZO ni kwamba kila nikifuatilia kiasi kilichobaki nakipataje naambiwa HICHO SITAWEZA KUKIPATA MPAKA UTARATIBU MPYA UTAKAPO TOLEWA. Nilienda ofisi nyingine nikaambiwa SIWEZI KULIPWA HICHO KILICHOBAKIA.
Fikiria ni asilimia 50 yaani nusu unalipwa nusu hulipwi. Naambiwa hata wale waliovuka miezi 18 katika ajira, baada ya kulipwa hizo asilimia 30 kwa miezi 6. Hulipwi tena kiasi kilichobaki. Huu ni utaratibu gani jamani. Si uonevu huu. Naomba wajuzi wa haya mambo wanisaidie.
Nifanye nini?