kwanini njia za kupata wabunge wa EALA (BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI) ZIsibadilishwe ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kwanini njia za kupata wabunge wa EALA (BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI) ZIsibadilishwe ?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EL MAGNIFICAL, Jul 12, 2012.

 1. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Habari zenu wakuu ni imani yangu mko salama salimini !
  Wadau ktk kipindi kile cha uchaguzi wa Eala sikupendezewa sana na rushwa zilizokuwa zinaendelea chini kwa chini.....!

  Pia aina ya washiriki waliokuwepo, bila kusahau kutokuwepo usawa baina ya chama tawala na upinzani,
  Sasa basi hivi ni kwanini wabunge wa bunge la afrika mashariki wasiwe wanatoka ndani ya bunge letu na wabunge hao wawe wale ambao ni machachali kwa kutetea maslahi ya taifa inshort wabunge wote ambao huwa makini pindi wazungumzapo ili kuweka safu nzito kwa majilani zetu wanapokuwa ktk bunge hilo.

  Na pia wabunge watakao toka kutuwakilisha chama kitakachokuwa kimetoa mbunge wake kitachukua jukumu jingine la kumuweka mtu mwingine ili kumfidia mbunge wa chama chao bungeni ?

  Nawasilisha.

  Ntashukuru nikipata mawazo yako karibuni.
   
 2. kiagata

  kiagata Senior Member

  #2
  Jul 12, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 192
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mchakato wa ubunge ni mzito siku zote hata hivyo siku moja mambo yatabadirika na wale wabunge machachali katika majimbo yao tutawaona wakitutetea kupitia EALA.

  Hata hivyo kampeni za chama tawala zinawaminya upinzani kutoa kichwa ktk kinyangany'iro hicho.Mf mkumbuke MH.Mbere Marando katika chaguzi iliyopita alikuwa wembe.Hata hivyo muda ukifika mambo yatakuwa shwari.
   
 3. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Mimi ningeshauri kwakuwa wabunge wa EALA ni wabunge wanawakilisha wananchi wote irrespective of their party affiliation, wananchi wote watakaowania nafasi hizo waombe hizo nafasi kwa TAASISI YA BUNGE badala ya kupitia kwenye vyama vyao ambako wanafanyiwa mizengwe ya kutowapitisha watu wenye uwezo ili mradi hawawataki!! Bunge ndio lifanye mchujo toka awali na sio vyama vya siasa.
   
Loading...