Kwanini nina shauku ya kuacha kazi ya serikali? Hii roho inanifuatilia sana

goodfool

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
1,664
993
Hamjambo.

Goodfool nimerudi tena.

Goodfool ,mim mi mwajiriwa wa serikali idara ya elimu kama mwalimu. Nimekua nikipenda mada mbalimbali na kila kitu kwangu ni sawa katika kujifunza thats why I called myself a Goodfool.

Kwa kipindi kirefu, nime kuwa na shauku ya kuacha kazi ninayofanya sasa,

Toka niajiriwe mwaka 2012
Miezi sita tu nikawa na shauku hii kwa mawazo yanayonijia kama haya:

1. Niache kazi nipate muda mpana nivumbue jambo lolote litakafanya mchango wangu uonekane katika jamii.

2. Niache kazi, nibobee katika kilimo na ufugaji au tuseme ujasiria mali.

3. Niache kazi nisomee mambo ya mazingira na wanyama (wild life) , niaNzishe campaign ,nijitolee katika taifa na jamii

4. Niache kazi nifanye kilichomo kwenye shauku(B) ukiacha taaluma yangu.

5. Nifanye fursa nnazoziona hazitumiwi vjjn kama uokaji wa mikate, utengenezaji sabuni , ufugaji sungura, pig, bata, punda n.k

kuna mda mawazo haya yananiteka sana.

Si kama siridhiki na kipato changu. Ni kama nahisi nabanwa na duties za serikali, mda mwingine mpaka nakosana na wakuu wangu katika kazi.

Mnaweza sema labda vyuma vimekaza, ila mbali na gvt salary, nina ki-pharmacy kijijini, duka la mahtaj ya nyumbani, ninalima kidogo pamba na choroko.
Na hata natamani kumiliki small scale sisal plantation.
labda mnaweza sema vipato kidogo vya nje binanipa kibri , hapana, ila ninashauku ya kuwa mkubwa mwenye mafanikio zaidi (sio tajiri no)

Ninapoanza kufikiria jinsi ninavyotaman kuwa mtu huru huwa nakosa usingizi na ninalala masaa 2!, HUKU YALIYOBAKI NIKIKESHA KWENYE MEDIA KUSOMA MAKALA MBALIMBAL ZA UVUMBUZI, UJASIRIA MALI, KILIMO, UFUGAJI, NAKESHA YOUTUBE , JF.

LEO nimeona alichofanya SUMRY huko Rukwa, nimekuwa inspired vibaya.
Napenda kuwasikiliza akina Moe, Eric Shigongo billie get, mark zuckerbag, hoja za nmna ya kufanikiwa katika mambo mbalimbl, na kusoma m,akala zenu hapa jf zenye muelekeo huo. (Japo zingine pia humu nasoma)
Navutiwa na watu waliochukua m@muzi magumu katika maisha, mchana na usiku nawaza kugundua kitu kitakacho irahisishia jamii maisha.

Nahisi kazi (ajira) inanipa uvivu fulani wa kimawazo(kifikra)

MAMBO YANAYONIWIA VIGUMU KUACHA KAZI.

1. Katika familia mimi na baba yangu pekee ndo w@jiriwa wa serikali, kaka ni wafanyabiashara wadogo huku wadogo zangu wakiwa benchi mpaka sasa, ajira. hivi uamuzi wangu watauchukuliaje?

2. Mama yangu ndo kabisa hataki kusikia anasema shetani ananifatilia, nimshike yesu.

3. Ukoo wote waajiriwa serikalini ni wachache -12), na jinsi ndugu wanavyopenda kunisihi sihi ("usichezee kazi")

4. Hali ilivyo alafu ni -declare kuacha kazi, ajira ngumu, si wataniona mwehu? Kama ndoa nataman kutoka wengine wanataman kuingia .

Natamani kuwa independent kufanya yaliyo katika shauku yangu ya moyoni.

Sijatawaliwa na woga ila napata wakti mgumu kutokana na nilivyoeleza.

Ruksa kunirekebisha/

Wasalaaam, Goodfool.
 
kuacha kazi kabla hujaliweka vizuri jambo la maana la kufanya sikushauri, inabidi uwe na uhakika na kile utakachoenda kufanya baada ya kuacha kazi. ila kama nafsi yako inakuhimiza uache kazi, acha, huenda hiyo sio talanta yako, sharti ya kazi yoyote ile ni kuipenda kutoka moyoni
 
Ndo maana naipenda jf, thaanks
 
Mkuu Mimi sio mwajiriwa ni mpiga dili tu ila nakushauri usiache kazi kwanza tengeneza mazingira mazuri ya kufikia baada ya kuacha kazi ndipo uache,na msela wangu aliacha kazi kichwa kichwa saa hivi anaonekana kujuta so tengeneza mazingira mazuri ya hizo plan zako za kibiashara ndipo uache
 
sikiliza nafsi yako kumbuka kuna mstari mwembamba sana kati ya utajiri na umaskini ambao huko kwenye fikra za mhusika
Ni somo zuri, Japo unaonyesha unahitaji msaada na wakati huohuo umegusa watu wengi humu ambao wako kwenye Ukinzani wa mawazo kama ulivyoainisha Kisanifu sana,

Ngoja nikupe Majibu ya Kukusaidia kwenye maamuzi yako:
Kama viashiria hivi vifuatavyo vinakusukuma, basi tambua kazi unayofanya aidha umeajiriwa itakutesa na kukuumiza hata kama inakupa Mshahara mzuri na unakidhi haja zako kadhaa!

1.Angalia Moyoni mwako, je unapata satisfaction, kama hakuna utoshelezi wa moyoni unapofanya hiyo kazi, basi usisubiri kuuliza kama hapo siyo mahali sahihi! Moyo wako utaumia na kuteseka na utakuwa mlalamishi, maana satisfaction siyo fedha au utajiri ni divine connection ya mtu na kazi yake halisi aliyoumbiwa kuifanya. Ndo maana utashangaa mtu anaacha kazi ya Upolisi kwa mfano aliyokuwa analipwa 500,000 kwa mwezi kwa mfano anaenda kuanza Kilimo cha vitunguu, anakaa miaka 3 anasotea kupata hata 200,000 kwa mwezi hapati, LAKINI anakuwa na satisfaction kwenye nafsi yake..Na hatimaye baada ya miaka 5 anapata faida kubwa inayomtambulisha huko duniani kuwa kuna mkulima mkubwa wa vitunguu huko morogoro !!
Unachokitamani anza kukifanya hata kama ni Kidogokidogo, hicho ndicho kitakacho kutoa maana kiko ndani yako na kinakupa satisfaction, usiogope kuanza, maana hakuna kazi au kitu kisicho na mwanzo,

2. Raha nafsini mwako, Hii ni raha inayotokana na kazi unayofanya, unajisikia raha kuifanya hata kama haikupi faida lakini imejaa ndani ya kilindi chako cha moyo, inakupa raha kuifanya. Si unaona mtu anaajiriwa kuwa Mwalimu wa Pr. School anjisikia raha na anafurahia kazi yake ya kufundisha watoto wa darasa la kwanza, wakati mwingine hataki hata kusikia habari ya ualimu lakini huyu anajisikia kukaa na watoto na kupiga story za 'A' , E, I, O, U....anaona raha...Huyo anaweza kuanzisha shule ya Chekechea na shule ikaenda na kufanikiwa, maana iko raha nafsini mwake kufundisha...SASA kama mkulima akaanzisha shule ya chekechea unadhani atakuwa na nini? zaidi ya kukumbuka faida ndiyo impe raha ya kufungua shule hiyo....raha nafsini mwako itakuvuta kufanya kazi uliyotakiwa uifanye...

3. Uhuru wa Maamuzi ( Freedom of mind)...unakuwa huru kwenye decision making, unajua wapi unatakiwa na muda upi, uko huru haufungwi, ukiamua ulale masaa ya mchana na usiku uchape kazi ni sawa tu, ukiamua usafiri kwa ndege ni wewe tu! ukiamua usile siku nzima ili kubana matumizi...Ukiona kazi uifanyayo haikupi uhuru wa kutumia Nafasi yako ujue uko kifungoni, Tafuta uhuru wako...Kama ni mbunifu basi kimbilia huko anza kubuni kidogokidogo...utafanikiwa tu...

......Nitaendelea....Ngoja nimalizie majukumu mengine,....

Joune, Ndaga,
Kyala Nnunu.
 
Mkuu Mimi sio mwajiriwa ni mpiga dili tu ila nakushauri usiache kazi kwanza tengeneza mazingira mazuri ya kufikia baada ya kuacha kazi ndipo uache,na msela wangu aliacha kazi kichwa kichwa saa hivi anaonekana kujuta so tengeneza mazingira mazuri ya hizo plan zako za kibiashara ndipo uache
Ubarikiwe mkuu. You're so sincere too, my task is just filtering
 
Hizo ni dalili za mwanzo za kuanza kujitambua .....( mimi ni nani ) nataka nini katika maisha yangu/ ndoto zangu ni zipi, ....hiki ninachokifanya kitatimiza ndoto zangu......etc
" Hongera sana" ni stage ambayo binadamu wengi waliofanikiwa waliipitia ,

Mafanikio yoyote huanza na ndoto baadae utatakiwa kuzifanyia kazi ndoto zako (following the dream) na mwisho utatakiwa kuondoka katika huo utumwa huru( ajira)

Haya mambo si ya kukurupuka, kwani ujasiriamali ni mzuri sana kuuona kwa nje ndani kuna complications na changamoto nyingi you need to be strong

Kwa haraka unaonekana ni bado kijana - 30 .... ningekushauri endelea kukamatia hicho kibarua huku ukijipanga vizuri mpaka nafsi yako itakaporidhika kuwa unaweza kimbia mwenyewe .
 
Ni somo zuri, Japo unaonyesha unahitaji msaada na wakati huohuo umegusa watu wengi humu ambao wako kwenye Ukinzani wa mawazo kama ulivyoainisha Kisanifu sana,

Ngoja nikupe Majibu ya Kukusaidia kwenye maamuzi yako:
Kama viashiria hivi vifuatavyo vinakusukuma, basi tambua kazi unayofanya aidha umeajiriwa itakutesa na kukuumiza hata kama inakupa Mshahara mzuri na unakidhi haja zako kadhaa!

1.Angalia Moyoni mwako, je unapata satisfaction, kama hakuna utoshelezi wa moyoni unapofanya hiyo kazi, basi usisubiri kuuliza kama hapo siyo mahali sahihi! Moyo wako utaumia na kuteseka na utakuwa mlalamishi, maana satisfaction siyo fedha au utajiri ni divine connection ya mtu na kazi yake halisi aliyoumbiwa kuifanya. Ndo maana utashangaa mtu anaacha kazi ya Upolisi kwa mfano aliyokuwa analipwa 500,000 kwa mwezi kwa mfano anaenda kuanza Kilimo cha vitunguu, anakaa miaka 3 anasotea kupata hata 200,000 kwa mwezi hapati, LAKINI anakuwa na satisfaction kwenye nafsi yake..Na hatimaye baada ya miaka 5 anapata faida kubwa inayomtambulisha huko duniani kuwa kuna mkulima mkubwa wa vitunguu huko morogoro !!
Unachokitamani anza kukifanya hata kama ni Kidogokidogo, hicho ndicho kitakacho kutoa maana kiko ndani yako na kinakupa satisfaction, usiogope kuanza, maana hakuna kazi au kitu kisicho na mwanzo,

2. Raha nafsini mwako, Hii ni raha inayotokana na kazi unayofanya, unajisikia raha kuifanya hata kama haikupi faida lakini imejaa ndani ya kilindi chako cha moyo, inakupa raha kuifanya. Si unaona mtu anaajiriwa kuwa Mwalimu wa Pr. School anjisikia raha na anafurahia kazi yake ya kufundisha watoto wa darasa la kwanza, wakati mwingine hataki hata kusikia habari ya ualimu lakini huyu anajisikia kukaa na watoto na kupiga story za 'A' , E, I, O, U....anaona raha...Huyo anaweza kuanzisha shule ya Chekechea na shule ikaenda na kufanikiwa, maana iko raha nafsini mwake kufundisha...SASA kama mkulima akaanzisha shule ya chekechea unadhani atakuwa na nini? zaidi ya kukumbuka faida ndiyo impe raha ya kufungua shule hiyo....raha nafsini mwako itakuvuta kufanya kazi uliyotakiwa uifanye...

3. Uhuru wa Maamuzi ( Freedom of mind)...unakuwa huru kwenye decision making, unajua wapi unatakiwa na muda upi, uko huru haufungwi, ukiamua ulale masaa ya mchana na usiku uchape kazi ni sawa tu, ukiamua usafiri kwa ndege ni wewe tu! ukiamua usile siku nzima ili kubana matumizi...Ukiona kazi uifanyayo haikupi uhuru wa kutumia Nafasi yako ujue uko kifungoni, Tafuta uhuru wako...Kama ni mbunifu basi kimbilia huko anza kubuni kidogokidogo...utafanikiwa tu...

......Nitaendelea....Ngoja nimalizie majukumu mengine,....

Joune, Ndaga,
Kyala Nnunu.
Loooh!!! What the great consult!!!!, asante I have understood you well mkuu
 
Kama una wadogo zako wasio kua na ajira, ndugu zako wenye vibihashara vidogo vidogo basi jua kabisa wewe sio mbunifu na ukiacha kazi utakufa masikini. Nasema hivi kwa kua kama ungekua na mawazo na mipangilio chanya basi tulitegemea uanze kui implement kwa ndugu zako ili kupitia mitaji yao hiyo midogo waweze kukua kupitia mawazo yako.

Nakushauri usiache kazi kwani bado hakuna uliloweza kulifanikisha kwa kutumia mazingira uliyonayo kwa sasa. Endelea tu kusoma story za akina Bill Gates.
 
Na
Hamjambo.

Goodfool nimerudi tena.

Goodfool ,mim mi mwajiriwa wa serikali idara ya elimu kama mwalimu. Nimekua nikipenda mada mbalimbali na kila kitu kwangu ni sawa katika kujifunza thats why I called myself a Goodfool.

Kwa kipindi kirefu, nime kuwa na shauku ya kuacha kazi ninayofanya sasa,

Toka niajiriwe mwaka 2012
Miezi sita tu nikawa na shauku hii kwa mawazo yanayonijia kama haya:

1. Niache kazi nipate muda mpana nivumbue jambo lolote litakafanya mchango wangu uonekane katika jamii.

2. Niache kazi, nibobee katika kilimo na ufugaji au tuseme ujasiria mali.

3. Niache kazi nisomee mambo ya mazingira na wanyama (wild life) , niaNzishe campaign ,nijitolee katika taifa na jamii

4. Niache kazi nifanye kilichomo kwenye shauku(B) ukiacha taaluma yangu.

5. Nifanye fursa nnazoziona hazitumiwi vjjn kama uokaji wa mikate, utengenezaji sabuni , ufugaji sungura, pig, bata, punda n.k

kuna mda mawazo haya yananiteka sana.

Si kama siridhiki na kipato changu. Ni kama nahisi nabanwa na duties za serikali, mda mwingine mpaka nakosana na wakuu wangu katika kazi.

Mnaweza sema labda vyuma vimekaza, ila mbali na gvt salary, nina ki-pharmacy kijijini, duka la mahtaj ya nyumbani, ninalima kidogo pamba na choroko.
Na hata natamani kumiliki small scale sisal plantation.
labda mnaweza sema vipato kidogo vya nje binanipa kibri , hapana, ila ninashauku ya kuwa mkubwa mwenye mafanikio zaidi (sio tajiri no)

Ninapoanza kufikiria jinsi ninavyotaman kuwa mtu huru huwa nakosa usingizi na ninalala masaa 2!, HUKU YALIYOBAKI NIKIKESHA KWENYE MEDIA KUSOMA MAKALA MBALIMBAL ZA UVUMBUZI, UJASIRIA MALI, KILIMO, UFUGAJI, NAKESHA YOUTUBE , JF.

LEO nimeona alichofanya SUMRY huko Rukwa, nimekuwa inspired vibaya.
Napenda kuwasikiliza akina Moe, Eric Shigongo billie get, mark zuckerbag, hoja za nmna ya kufanikiwa katika mambo mbalimbl, na kusoma m,akala zenu hapa jf zenye muelekeo huo. (Japo zingine pia humu nasoma)
Navutiwa na watu waliochukua m@muzi magumu katika maisha, mchana na usiku nawaza kugundua kitu kitakacho irahisishia jamii maisha.

Nahisi kazi (ajira) inanipa uvivu fulani wa kimawazo(kifikra)

MAMBO YANAYONIWIA VIGUMU KUACHA KAZI.

1. Katika familia mimi na baba yangu pekee ndo w@jiriwa wa serikali, kaka ni wafanyabiashara wadogo huku wadogo zangu wakiwa benchi mpaka sasa, ajira. hivi uamuzi wangu watauchukuliaje?

2. Mama yangu ndo kabisa hataki kusikia anasema shetani ananifatilia, nimshike yesu.

3. Ukoo wote waajiriwa serikalini ni wachache -12), na jinsi ndugu wanavyopenda kunisihi sihi ("usichezee kazi")

4. Hali ilivyo alafu ni -declare kuacha kazi, ajira ngumu, si wataniona mwehu? Kama ndoa nataman kutoka wengine wanataman kuingia .

Natamani kuwa independent kufanya yaliyo katika shauku yangu ya moyoni.

Sijatawaliwa na woga ila napata wakti mgumu kutokana na nilivyoeleza.

Ruksa kunirekebisha/

Wasalaaam, Goodfool.
Matajiri wangekuwa wanasita sita hivi unadhan wangefika? Unaona ualimu unakupa kajina fulan just stay there....ili uendelee kukupa heshima mbaya zaidi hauupendi.......
 
Back
Top Bottom