#COVID19 Kwanini nina mashaka na Chanjo ya COVID 19

Jul 5, 2020
5
3
Katika kukabiliana na UVIKO-19, ni sawa kuanza kuyachanja haya makundi yaliyopendekezwa na kamati ya Profesa Aboud?


Simiyu, Tanzania

Mheshimiwa rais Samia alipoingia madarakani aliunda kamati ya wataalamu wa hapa nchini ili kufuatilia mwenendo wa mlipuko wa UVIKO-19 na kumshauri njia za kutumia katika kuthibiti janga hili. Rais alifanya vizuri sana kufanya hivi kwa sababu hili ni janga la kimataifa.

Lakini ni muhimu kuweka rekodi sawa katika jambo hili pamoja na uhalali na umuhimu wa kuwepo kamati.

Wakati kamati inaundwa janga la korona lilikuwa na zaidi ya mwaka katika nchi ya Tanzania, na kwa muda wote huo Tanzania ilikuwa imefaulu kwa kiasi kikubwa katika juhudi zake za kupambana na janga hili na wengi katika mataifa yaliyotuzunguka walikuwa wanatamani kuwa wananchi wa Tanzania. Pamoja na kwamba nchi za jirani na nyingine kwa mfano, Afrika Kusini, Kenya na Uganda zilifungia watu ndani, Tanzania haikuchukua uamuzi huo. Hayati Magufuli aliruhusu watu waendelee na shughuli zao kama kawaida huku wakimwomba Mungu na kuzingatia ushauri wa Wizara ya Afya.

Mpaka kampeni za uchaguzi zinaanza mwaka jana, na kufanyika kwa kipindi cha miezi miwili, shughuli ambazo zilihusisha makusanyiko ya watu, wengine wakisafiri kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine na wengine jimbo moja kwenda jimbo lingine, hakukuwepo na mabadiliko katika hali ya kiafya ya watanzania kuhusiana na janga la korona. Huku kwetu, watu waliamini kabisa korona imetoweka na wengine kwamba kama korona ilikuwepo basi haikuwa na madhara.

Kama kweli korona ilikuwepo kipindi kile cha kampeni, na ilikuwa inaenea kupitia mikusanyiko ya watu, kwa nini haikuuwa maelfu ya watu. Maana kama ingekuwa inaenea kwa kasi kupitia mikusanyiko ya watu basi watanzania wengi wangeambukizwa kipindi hicho na vifo vingi vingetokea.

Sasa kama korona iliingia Tanzania, ambalo ni ukweli, lakini yakafanyika mambo ambayo yalifanyika, kama kumuomba Mungu na kutumia tiba za asili basi mambo hayo yalisaidia hata kama hayawezi kuthibitishwa kwa formula za kisayansi.

Kwa hiyo kamati ilitakiwa ifanye marejeo katika mambo yaliyokwisha fanyika na kuifanya Tanzania kufanikiwa katika kupambana na UVIKO-19, lakini haikufanya hivyo?

Pamoja na mambo mengine ambayo kamati ilishauri ambayo yawezekana haikufanya utafiti na ufuatiliaji wa kutosha, ni kupendekeza makundi maalumu katika kutekeleza mpango wa chanjo dhidi ya UVIKO-19.

Baadhi ya makundi yaliyopendekezwa kupewa kipaumbele katika chanjo ni pamoja na wahudumu katika vituo vya afya, watu wanaolinda mipaka, viongozi wa dini, watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na watumishi walio mstari wa mbele katika sekta ya utalii na hoteli.

Sasa kama umekuwa mfuatiliaji wa mambo chanjo za UVIKO-19 zina madhara yanayoambatana nayo. Hii yaweza kuwa kwa sababu ya teknolojia iliyotumika kuzitengeza, lkn pia haijachukua muda wa kutosha kuzijaribu lkn pia haikufanyika utafiti wa kutosha kama ambayo inakuwaga kwa chanjo zingine.

Mbali na sababu hizo, yameripotiwa matukio ya watu waliothirika kutokana na chanjo na wengine kufa baada ya kuwa wamechanjwa.

Kazi ya chanjo ni kuwakinga watu na ugonjwa. Kama watu wanakufa baada ya kuwa wamechanjwa, hata hata ni sehemu ndogo ya waliochanjwa basi hiyo chanjo sio salama.

Sasa kama kifo kinaweza kumpata mtu aliyechanjwa, kamati haikuona hayo makundi ambayo ni muhimu sana katika taifa yakichanjwa, na madhara yakawapata, watoa huduma katika sekta hizo watatoka wapi??

Kama kweli hii kamati ikuwa na uzalendo na taifa na wananchi wa Tanzania, ilishindwa kuonyesha madhara ya chanjo yaliyowapata wananchi wa nchi nyingine na kushauri namna ya kufanya...?


Sikuwa nimezingatia sana kauli za askofu Gwajima, lakini nilipoangalia tena ripoti ya kamati na mapendezo yao hususani makundi yanayotakiwa kupewa kipaumbele,nikaona hii kamati inabidi ipitie mapendekezo yake upya!!!

Kamati inataka kumwambia Mhe rais Samia kwamba madaktari wote na wauguzi waanze kuchanjwa? Wakipata madhara itakuwaje?

Kamati inataka kumwambia Mhe rais kwamba polisi na majeshi yote wachanjwe? Wakipata madhara itakuwaje?

Kamati inataka kuwambia Mhe rais kwamba watu wa uhamiaji waanze kuchanjwa? Wakipata madhara itakuwaje?


Je, kamati hii imetokea wapi? Watu hawa hawakuwepo wakati korona inaanza mwaka jana? Njia zilizotumika kukabiliana na korona mwaka jana hapa Tanzania hazifai? Kweli?

Profesa Aboud na kamati yake inabidi wajitafakari upya...


Hamisi Mzalendo
hamis@rocketmail.com
Simiyu
 
Umesha Ambiwa Abiria chunga mzigo wako! (Chanjo ni Hiyari)
Kama unajiona unayo kinga ya mwili ya kutosha achana nayo!
Chanjo ni short and long term strategy!
Ref; ufumbuzi uliopatikana ktk chanjo ya ndui!
 
Hii hoja ni dhaifu sana (hitimisho)! Kama Covid-19 inaambukiza kupitia hewa na kwa hiyo walio kwenye mikusanyiko mikubwa ni more susceptible to contract Covid-19, huwezi kuhitimisha kwamba kwa vile kulikuwa na mikusanyiko mikubwa na watu wengi hawajaathiriwa, then Covid-19 haipo au haiambukizi watu wanapokusanyika wengi.

Wote tunajua sumu inaua na huwa inatokea watu waliokula chakula au kunywa kinywaji chenye sumu baadhi wanapoteza maisha na baadhi wanapona. Kwa vile baadhi wamepona, huwezi kuhitimisha kwa kusema kwamba kula chakula au kunywa kinywaji chenye sumu hakiwezi kukudhuru.

Unafahamu pia kwamba Tanzania ni moja ya nchi zenye mbu wanaombukiza malaria na unajua pia kuna dozi mbalimbali za malaria ambazo watu wakipata malaria huwa wanatumia. Baadhi wanapoteza maisha hata baada ya kutumia dawa na baadhi wanapona. Ni irrelevant kuhitimisha kwamba kwa vile baadhi wamefariki, then dozi zinazotolewa za malaria hazifai.

Mfano mwingine ni kwamba kuna wakati tuliambiwa wananchi wanaokaa kando ya Ziwa Victoria na kutumia maji ya ziwa kuna uwezekanao mkubwa wa kupata ugonjwa wa kichocho. Na mimi ni mkazi wa mikoa ya kanda ya ziwa na nimetumia hayo maji karibu maisha yangu yote ya ujana. Nikipimwa nikakutwa sina ugonjwa wa kichocho, huwezi kusema ni kwa sababu nimekuwa nikitumia maji yenye vijidudu vya kichocho. Mambo haya ya kitafiti/kisayansi yana logic yake tofauti na unayotaka ifanye kazi kwa chanjo na maambukizi ya Covid-19.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom