Habari za jukwaa la MMU bosses.
Sisi kama binadamu tumetofautiana kwa mambo mengi sana. Kimtazamo, jinsi tunavyoyachukulia mambo na lifestyle kiujumla.
Huwezi amini naweza nikamaliza week sijampigia mpenzi wangu simu lakini nikaona ni jambo la kawaida sana, lakini yeye lazima atalalamika na mimi nashindwa kujua kosa langu hapo ni lipi.
Mpaka yeye ndio huwa ananipigia au kama hana salio atanitumia message ya kuomba nimpigie. Na si kwa mpenzi wangu tu hata kwa jamaa na ndugu hali ni hiyo hiyo. Kwa mfano nikienda chuo naweza kumaliza semester nzima sijampigia ndugu yangu yoyote simu kujuliana hali.
Na ikitokea mtu akawa ananicare sana huwa sijisikii comfortable sana. Napenda tuwasiliane lakini isiwe kupita kiasi. Tofauti na wenzangu ambao wanaweza kuwapigia simu wapenzi wao zaidi ya mara nne kwa siku au kuongea na marafiki mara kwa mara kwenye simu.
Wakati mimi ikitokea mtu kanipigia leo tukaongea akimaliza siku mbili akipiga tena kama hana ishu zaidi ya kusalimiana tu huwa naona kama ananichosha.
Hivi hili linaweza kuwa tatizo au ni kawaida tu? Maana nalalamikiwa sana kwenye suala kama hilo.