Kwanini nimekua mtu wa kutokujali sana kwenye mahusiano na jamii yangu?

Ototo

JF-Expert Member
Jun 26, 2016
1,107
2,000
Habari za jukwaa la MMU bosses.

Sisi kama binadamu tumetofautiana kwa mambo mengi sana. Kimtazamo, jinsi tunavyoyachukulia mambo na lifestyle kiujumla.

Huwezi amini naweza nikamaliza week sijampigia mpenzi wangu simu lakini nikaona ni jambo la kawaida sana, lakini yeye lazima atalalamika na mimi nashindwa kujua kosa langu hapo ni lipi.

Mpaka yeye ndio huwa ananipigia au kama hana salio atanitumia message ya kuomba nimpigie. Na si kwa mpenzi wangu tu hata kwa jamaa na ndugu hali ni hiyo hiyo. Kwa mfano nikienda chuo naweza kumaliza semester nzima sijampigia ndugu yangu yoyote simu kujuliana hali.

Na ikitokea mtu akawa ananicare sana huwa sijisikii comfortable sana. Napenda tuwasiliane lakini isiwe kupita kiasi. Tofauti na wenzangu ambao wanaweza kuwapigia simu wapenzi wao zaidi ya mara nne kwa siku au kuongea na marafiki mara kwa mara kwenye simu.

Wakati mimi ikitokea mtu kanipigia leo tukaongea akimaliza siku mbili akipiga tena kama hana ishu zaidi ya kusalimiana tu huwa naona kama ananichosha.

Hivi hili linaweza kuwa tatizo au ni kawaida tu? Maana nalalamikiwa sana kwenye suala kama hilo.
 
Mkwanzania

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
280
500
Ni suala la kawaida sana wala usipate taabu. Ni LAZIMA wanadamu tutambue kila mtu ana hulka tofauti. Watu wengine kama wewe na mimi ni introvert, tunaamini zaidi katika kuwasiliana na hisia zetu badala ya hisia za watu wengine. Mimi pia kama najua au conscience zangu zinaniambia watu wangu wako salama na hakuna tatizo huwa sioni sababu ya kuwapigia pigia simu.

Lakini hii haimaanishi kwamba huwezi kujifunza kidogo kuboresha mawasiliano yako, unaweza kuanza kujitahidi kwa kupanga muda hili uwasiliane na watu wako wa karibu sana kama wazazi na mpenzi sababu kwa vyovyote vile unahitaji au wanahitaji kuwasiliana na wewe kihisia zaidi kuliko watu wengine ili kuwaonesha kuwa unajali. Sio kazi rahisi najua lakini jitahidi.
 
abrhms

Member
Nov 13, 2015
15
45
Usijari mkuu..haupo peke yako. Nami nipo kama wewe...labda cha kuongezea ni kwamba mie sipendi kabisa kutembelewa labda mie niamue kutembelewa/kumtembelea mtu. Pia nipo vzr sana katika uhusiano wa ana kwa ana..lakini tukipeana mgongo ndo kwaheri (out of site, out of mind). Ila mie niliwahi kushare na ndugu zangu tatizo langu na kuwaambia ikitokea sijawasiliana nao wasione kama nimewatupa...in short nawapenda sana...ila kiasi wewe umenizidi semister nzima...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
themanhimself176

JF-Expert Member
Dec 28, 2016
1,701
2,000
sio wewe mkuu ata mie pia kisanga icho niko nacho napiga simu kwa mama yangu tu na wadogo zangu kwa jamaa wengine sijawa fanya ivyo na ni lawama usiseme kila siku maneno ila siwezi kbsaaaaa...............

kwa demu wangu ndo kisanga kwanza mimi sio mpenzi wa kuongea na simu saaaaana ila napendelea txt message nikimeet nae ni kumla mambo ya outing sijui nini atamtoa baba ake na sio mimi
 
Daxx Shado

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
381
1,000
Tupo wengi, na nakubaliana na alieongelea kuhusu introverts. Mimi binafsi si tu kwamba sipigi simu au kuwasiliana na ndugu na jamaa mara kwa mara lakini pia nikiwa na tatizo ni mgumu sana kumwambia yeyote.

Mara nyingi najikuta napambana na hali yangu wakati msaada upo, tatizo ni kuwa huwa napata shida sana kumwambia mtu.Huwa naona bora nipambane mwenyewe mpaka ni-solve kuliko kuomba msaada kwa mtu.

Nimejitahidi kubadilika bila mafanikio. Imefika mahali nimeikubali tabia yangu, naenda nayo hivyo hivyo japo lawama toka kwa watu wa karibu ni nyingi sana... lakini naona nao wameanza kunizoea hivyo hivyo.

Nitafurahi kusikia mwenye maoni tofauti ambayo yanaweza kuwa suluhisho.

[HASHTAG]#stayhungry[/HASHTAG] [HASHTAG]#stayfoolish[/HASHTAG]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nwaigwe

JF-Expert Member
Jul 9, 2009
1,029
2,000
Kwa wakristo ebu mkasome Kitabu cha Wagalatia. ...siku za mwisho watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe. ..wasiopenda wa kwao. ....n.k roho wa Mungu hutuongoza kujali na kupenda wanaotupenda. Kama wewe ni mkristo muombe roho Mt. Akae ndani yako akufundishe kupenda na kujali wengine
 
abrhms

Member
Nov 13, 2015
15
45
Kumbe tupo wengi...haijapita mwezi nimebreak-up na mpenzi..shida ni mawasiliano..nipo kimya sana..huwa nanunua vifurushi kwa ajili ya internet tu...dakika sina shida nazo. Nakumbuka chuo nilikuwa nawashangaa watu walikuwa wanapiga simu ovyo ili tu vifurushi vyao visiishe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
salito

JF-Expert Member
Dec 29, 2011
1,409
2,000
Na mimi nilikuwa kama mtoa mada lakini nilipata mabadiliko makubwa sana baada ya kupata mtoto,Hasa alipofikisha mwaka na nusu na kuanza kuibia maneno na nilichanganyikiwa siku aliponiita baba kwa mara ya kwanza,huwezi amini nilimnunulia dogo simu akiwa na umri huo na nikawa napiga kutwa kuongea nae,mpaka leo huo ndio utamaduni nilionao.
Labda na wewe unaweza kubadilika ukipata atakae yagusa hasa maisha yako.
 
Ototo

JF-Expert Member
Jun 26, 2016
1,107
2,000
Ni suala la kawaida sana wala usipate taabu. Ni LAZIMA wanadamu tutambue kila mtu ana hulka tofauti. Watu wengine kama wewe na mimi ni introvert, tunaamini zaidi katika kuwasiliana na hisia zetu badala ya hisia za watu wengine. Mimi pia kama najua au conscience zangu zinaniambia watu wangu wako salama na hakuna tatizo huwa sioni sababu ya kuwapigia pigia simu.

Lakini hii haimaanishi kwamba huwezi kujifunza kidogo kuboresha mawasiliano yako, unaweza kuanza kujitahidi kwa kupanga muda hili uwasiliane na watu wako wa karibu sana kama wazazi na mpenzi sababu kwa vyovyote vile unahitaji au wanahitaji kuwasiliana na wewe kihisia zaidi kuliko watu wengine ili kuwaonesha kuwa unajali. Sio kazi rahisi najua lakini jitahidi.
Kweli mkuu najitahidi sana na mimi Kuwa mtu wa kupiga simu mara kwa mara
 
Ototo

JF-Expert Member
Jun 26, 2016
1,107
2,000
sio wewe mkuu ata mie pia kisanga icho niko nacho napiga simu kwa mama yangu tu na wadogo zangu kwa jamaa wengine sijawa fanya ivyo na ni lawama usiseme kila siku maneno ila siwezi kbsaaaaa...............

kwa demu wangu ndo kisanga kwanza mimi sio mpenzi wa kuongea na simu saaaaana ila napendelea txt message nikimeet nae ni kumla mambo ya outing sijui nini atamtoa baba ake na sio mimi
Mim huwa nikihisi kuwamiss ndugu zangu huwa naenda nyumbani tunaonana naridhika Lakin sio kupiga simu ase.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom