khalta
Member
- Oct 21, 2017
- 66
- 123
Habari zenu wapendwa,
Sielewi nimepatwa na nini hata, kuna hali huwa inanijia mfano nikipita barabarani nikaona wale watoto wanaombaomba jamani napata na huruma sana moyo unaniuma hadi nalia.
Nikipishana tu na mtu mzima sana labda kiwete au mgonjwa au nikiona tu huyu mtu kajichokea jamani sielewi hii hali inatokea wapi nabadilika ghafla najikuta mnyonge sana.
Kuna mahali nilipita nikanunua kitu basi yule kijana akaniambia "Ahsante sana dada yangu Ahsanteeee kwa kuniungisha" huku akiiweka mikono yake kifuani kwake daaah aisee nilijikuta natokwa na chozi na huzuni ghafla.
Huwa nikimuangalia mtu ambaye najua anahitaji msaada kwa muda huo alafu hakuna uvumbuzi kwakweli naumia kabisa hadi naanza kuhisi hivi isije ikawa ni ugonjwa maana huzuni mara kwa mara nisaidieni hata siielewi hii hali kwanini inanitokea.