Franco Zetta
JF-Expert Member
- Nov 3, 2014
- 1,661
- 843
Waungwana mpaka nina leta kwenu hoja yangu ni baada ya kutafakari sana na nilipo kosa jibu nikaona niwa shirikishe, awali nili jiaminisha kuwa ni sababu ya uchama tu kuwa kinacho shika hatamu kina Wabunge wengi na upinzani ni wachache ila nikaona hapana ni zaidi ya hapo kwa maana kuna maswala ya kitaifa sana ambayo hayana nasaba na itikadi za kisiasa na kwa kutambua kuwa Wabunge wetu ni watu wazima na isitoshe ni wasomi na wanao jitambua kuwa wako pale kuisimamia Serikali kwa kutumwa na kuaminiwa na Watanzania, na kama ndivyo itokeeje tena yule msimamizi wa Serikali atumiwe tena kuwa kibaraka wa Serikali kupitishia matakwa yake ya kidhalimu na kuua Demokrasi na Wabunge walio wengi kuunga mkono tena kwa makofi kama vile wana manufaa binafsi na bila kujitambua kuwa wana bariki kuwanyima fursa na uhuru wananchi walio wachagua kuona na kuelewa jinsi wanavyo wakilishwa,sijui hofu yao wabunge walio wengi na Serikali inayo warubuni ni nini? ni wazi sasa nimeeleweka kuwa nina zungumzia Uhuru ulio kandamizwa wa vyombo vya habari kuonyesha live coverage Bungeni kwani hatua hii ni ishara ya mwanzo kabisa ya nini kina kuja na tuki tarajie hapo mbele,mbinu kama hizi za kulidhibiti Bunge zili tumiwa na kuinufaisha sana Serikali ya awamu ya tatu japo kulikuwa na kushtuka shtuka hapa na pale ila awamu ile ili kwama sana kwenye mhimili wa Sheria hadi kukawepo Uadui na kubaniwa fedha za bajeti, Mwalimu Nyerere ali tutahadharisha kuwa itakapo fikia mhimili wa Sheria nao ukachezewa na uka kubali basi tumekwisha, kwa Bunge hili mpaka kufikia kupandikiziwa Uongozi ni wazi kuwa Bunge hili limesha dakwa juu kwa juu tena alfajiri na mapema na Serikali haina msimamizi, Ndio ninapo uliza kwanini ni Mhimili wa Bunge tu kila wakati unao ruhusu hali hizi?.