Kwanini ni vyema Magari yenye kasi yanafungwa kidhibiti mwendo.

H.T.P

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,169
1,298
Wataalamu wa mambo ya usafirishaji wanashauri magari yote hasa yale yanayosafiri umbali mrefu huku yakiwa na abiria yafungwe speed governor, lengo ni kuhakikisha kwamba hata dereva atakapojisahau akakanyaga sana mafuta kuwe kuna kikomo kuepusha madhara yawezayo kusababishwa na ajali itokanayo mwendo kasi.

Nadhani sasa imefika wakati speed governor inahitaji kwa hawa watu tuliowaajiri kwa kura zetu, maana wakiachwa waendeshe tu kama vichwa vyao vinavyowatuma watatuangamiza wote.
 
Speed governor ni bunge, sasa angalia hilo bunge sasa linavyokuwa butu, hata meno halina, watanzania wasipoamka kutoka usingizini, maendeleo ya takuwa hivi hivi mwendo wa kinyonga, watanzania tuamke jamani, la sivyo tusubiri yale yale ya kudanganywa na kusema nchi yetu ni ya amani kumbe siyo amani ukweli ni kwamba ni ya waoga.
 
Hatuna haja na speed governor manake awali walipoleta hayo mambo; ilikuwa ni mradi wa wajanja wachache na wala hakusaidia.

Speed governor ni moja tu! Ipitishwe sheria, kama basi linaendeshwa kwa kasi sana; traffic analipiga mkono kisha abiria watu wazima wote wanakula bakora sita sita kisha safari inaendelea. Kama Traffic aliwaotea Mlandege lakini mlipofika Chalinze traffic mwingine akawaotea gari yenu ipo speed sana; hapo tena mnapigwa mkono kisha mnakula six zenu baada ya hapo kiroho safi safari yenu ya kwenda Tunduma inaendelea!

Nadhani hadi mkishaingia Tunduma tu, mnakaguliwa makalio na yakionekana yana malengelenge afande anafahamu kwamba hili basi lilibeba abiria wapumbavu kwahiyo mnaishia selo; kwenu hadi kesho asubuhi. Yaani hapo mtakuwa mnaenda kwenu wakati mshakula angalau six times four vinginevyo sioni adhabu inayowafaa watu wazima zaidi ya 30 wanaomwacha dereva mmoja awapelekeshe anavyotaka huku wakisubiri awamwage kwenye daraja ili wale wataosalimika watupigie kelele eti dereva alikuwa anaendesha kwa mwendo wa kasi.

Tutatafuta dawa ya ku-deal na traffic watakaoshindwa kutekeleza wajibu wao huu.
 
Back
Top Bottom