Kwanini ni vigumu sana kupata "A" katika vyuo vyetu? Tunawahujumu wanafunzi wetu?

sasa wewe unakuta mwalimu anatunga mtihani kwa ajili ya kukomoa na kukamata watu, halafu unakuta anajisifu kwenye somo langu hakuna mwanafunzi anapata A sasa we unategemea nini!?
 
Watoto wanashinda kwenye @twitter na Facebook unafikiri watapata A vipi?

Google imemaliza kabisa uwezo wa watoto wa vyuo wa Kitanzania - Inawezekana ni mkakati mahususi wa CIA

On the serious note : Either amepata "A" or "C" kutoka chuo chochote hapa Tz, ninachelea kusema uwezo wao wote wawili upo sawasawa tu!!!
 
si kwel wanopata A na C wawe sawa mara zte ingawa kias flan hujtokeza!mi nilichokiona pa1 na utashi we2 na kusoma kwa bidii kupungua kias kutokana na utandawaz BADO mfumo wa elimu ya juu unatakiwa uhusianshwe na mazngra/changamoto zlizopo kwny jamii!
 
Kidogo angalau saiv wanafunzi wanao ingia chuo ni wale walio faulu na kupata point 4.5 ili kujiunga na chuo.nimeshudia wanafunzi wengi wali ingia chuo bila hzo point lakin Tcu wakawa wakali wote wametimuliwa hadi warudie mithian na kufikisha point inayo takiwa .hii imeanza mwaka juzi. Pia hata wale wanao pata nafas ya ku soma chuo bado wana feli kwa sababu wengi wanasoma course walzo chagulwa na serekali na sio walzo chagua .au wanazo zipenda hii ndio issue kubwa hapa bongo.wat wana soma ili wawe na digri na sio wawe na taluma
 
Utakuwa umedesa sana vibuti na nondo nyingine kama si uongo tutajie somo ulilopata A kama sio la ngwini na tupe hesabu kama haujaegemea kuti kavu ndo nyie mmeambiwa mkiulizwa swali after exam mmeshasahau.

Sasa naona hizo ni dharau zilizopitwa na wakati za kuitana NGWINI, mimi kudesa ninadesa tena sanaa tu, najua kilichonileta chuo ni nini. Masomo niliyopata ni AY100 na AY105
(ukatafute majina yake but najua utakuwa unayajua), Mimi nasoma B.A.Archaeology na ninaipenda sana ndio maana sikubali kuishindwa, kuna cource na cource ni kweli mfano watu wa injiania japokuwa kuna ambao wanaoipata. Vichwa havifanani.:yell:
 
Watoto wanashinda kwenye @twitter na Facebook unafikiri watapata A vipi?

Google imemaliza kabisa uwezo wa watoto wa vyuo wa Kitanzania - Inawezekana ni mkakati mahususi wa CIA

On the serious note : Either amepata "A" or "C" kutoka chuo chochote hapa Tz, ninachelea kusema uwezo wao wote wawili upo sawasawa tu!!!

Hoja yako imetulia.
 
Unalazimisha kusikika kwa courtesy of bright colours?
 
Matokeo ya Mwaka wa nne Mlimani
1. Kwa shahada ya kwanza pale Mlimani gredi zenyewe zimekaa hivi (kama hazijabadilika) A: 75-100, B+: 70-74, B: 60-69, C: 50-59, D: 45-49 na E: 0-44 2. Gredi za hapa Marekani (kutoka katika silabasi yangu katika darasa la Language and African Society) zimekaa hivi: A: 93-100, A-: 90-92, B+: 87-89, B: 83-86, B-: 80-82, C+: 77-79, C: 73-76, C-: 70-72, D+: 67-69, D: 63-66, D-: 60-62, E: 0– 59. Japo profesa unaweza kujipendekezea gredi zako mwenyewe, mfumo huu wa alama ndio umependekezwa na chuo kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza. 3. Hali ilivyo kule nyumbani (kama bado haijabadilika)

  • Utakuta darasa lina wanafunzi 100, na kati ya wanafunzi hawa pengine wawili, watatu na hata mmoja tu ndiyo atapata "A". Hata madarasa makubwa yenye wanafunzi 300, eti wanafunzi wanne au watano tu ndiyo wanapata "A". Kwa nini? Ni kwa sababu masomo ni magumu sana? Wanafunzi hawajisomei sawasawa (Na kama hawajisomei ni kwa nini?), maprofesa hawafundishi vizuri kiasi kwamba wanafunzi hawawaelewi? Au maprofesa wanatunga mitihani migumu kupindukia? Au pengine wanafunzi wa vyuo vikuu vyetu ni mbumbumbu na hawana uwezo wa kupata A?

  • Ninacholalamikia hapa siyo kila mwanafunzi kupata A bali ule ugumu uliopo wa kupata alama hizi kwani siamini kama kweli eti katika darasa la wanafunzi 300, ni wanafunzi watatu au wanne tu ndiyo wana uwezo wa kufaulu vizuri. Kama hivi ni kweli basi ni wazi kuna tatizo kubwa katika mfumo wetu wa elimu.
4. Hali ilivyo hapa Marekani

  • Hapa kupata A ni jambo la kawaida na maprofesa na wanafunzi wanalijua hili. Mahusiano kati ya wanafunzi na maprofesa ni ya wazi na wanafunzi wanaweza kuuliza maswali na kujadili masuala ya gredi watakazozipata na maprofesa wao kwa uwazi. Hali hii inasababisha matatizo fulani na haya nitayaongelea siku nyingine.

  • Kwa wanafunzi wanaotegemea kuendelea na shahada za uzamili na uzamivu ni lazima wahakikishe kwamba wanapata A kwa sababu ushindani wa kupata ufadhili ni mkubwa sana na vyuo vingi vinataka wanafunzi ambao ni bora kabisa. Kwa ujumla alama za B, na hata B+ na pengine A- hazimsaidii sana mwanafunzi kuweza kujiunga na vyuo vikuu vyenye hadhi kama Harvard, Yale, Columbia, UCLA, Stanford, Berkeley na vinginevyo
5. Uzoefu Wangu

  • Nina uzoefu na uteuzi wa wanafunzi wa shahada za uzamili na uzamivu hapa Marekani na huwa nashangaa sana kugundua kwamba kwa kawaida waombaji kutoka Afrika huwa na alama za chini sana hasa ikilinganishwa na waombaji kutoka sehemu zingine duniani kama China, Korea, Ulaya, Amerika ya Kusini na hata nchi za Uarabuni. Maprofesa hapa huwa wanajiuliza inawezekanaje mwanafunzi mwenye azma na ari ya kujisomea ashindwe kupata A (75) ambayo hapa ni C? Na kama hakuna profesa wa kuwafahamisha wanakamati wenzie wanaofanya uteuzi kuhusu mambo yalivyo, mara nyingi maombi ya wanafunzi kutoka Afrika huwa hafifu sana na huishia kutupiliwa mbali. Ndiyo maana nahoji hapa kwamba pengine tunawahujumu vijana wetu kwa kuwapa alama za chini na kuishia kuwakosesha ufadhili ambao ungewawezesha kusomeshwa bure. Na sijui mfumo huu unamsaidia nani.
6. Ilivyokuwa Kwangu

  • Mwaka 1997 nilipata nafasi ya ufadhili wa kusoma shahada za uzamili na uzamivu katika Idara ya Isimu pale UCLA ambapo pia nilitakiwa kufanya kazi kama mwalimu msaidizi wa Kiswahili. Barua ya mwanzo niliyopata ilikuwa na masharti mawili yaliyonichanganya na kuninyima usingizi. Sharti la kwanza lilisema kwamba ilikuwa ni lazima nipate "first class" katika shahada yangu ya kwanza na la pili ni kufanya mtihani korofi wa GRE.

  • Sharti la kwanza liliwashtua watu wengi sana na niliambiwa kwamba kwa muda mrefu kulikuwa hakujawa na mtu aliyepata hiyo "first class". Niliambiwa kwamba pengine hawa jamaa wa UCLA walikuwa hawataki niende na niliambiwa kuachana nao kwani walichokuwa wananiomba kufanya kilikuwa hakiwezekani. Kilichonishangaza ni kwamba kulingana na matokeo yangu ya miaka mitatu iliyopita, ningeweza kupata hiyo first class kama ningepata angalau A nne tu katika mitihani yangu ya mwisho ya mwaka wa nne. Na kupata A nne katika masomo 10 niliyokuwa nikisoma eti ilikuwa haiwezekani. Sikukubali!
7. Nilichokifanya na Matokeo Yake

  • Sijawahi kusoma kwa nguvu zaidi, ari zaidi na kasi zaidi kama katika kipindi kile katika maisha yangu yote mpaka nikapachikwa majina ya "Librarian", mkazi wa "Special Reserve", "Aliyetumwa na kijiji" na mengineyo. Sikujali!

  • Matokeo ya mwaka wa nne yalipotoka nilikuwa nimepata A tisa, B+ moja na B moja. Nilikuwa nimeipata hiyo "first class!" tena nzuri. Haraka haraka niliyatuma matokeo hayo UCLA na msimamizi wangu (ambaye anafahamu ugumu wa kupata first class) alifurahishwa sana kiasi kwamba aliiomba kamati ya ufadhili kufuta sharti la mimi kufanya mtihani wa GRE. Habari hizi kuhusu GRE hata hivyo zilikuwa zimechelewa kwani tayari nilikuwa nimeshaanza maandalizi na nilikuwa nimeshalipia ada (dola 120). Niliufanya mtihani huu ili kujipima nguvu tu lakini first class tayari ilikuwa imesharekebisha mambo. Na hivi ndivyo nilivyoweza kusomeshwa UCLA kwa miaka sita (mitatu shahada ya uzamili na mitatu shahada ya uzamivu) huku nikilipiwa karibu dola 30,000 kwa mwaka.
Risti ya malipo ya GRE

  • Ati, kwa nini ni vigumu sana kupata A na hatimaye "first class" katika vyuo vikuu vyetu? Tatizo hasa ni nini? Ni mfumo wa elimu tuliorithi kutoka kwa Waingereza? Pengine inabidi tulifikirie jambo hili kwani inawezekana tukawa tunawahujumu wanafunzi wetu kwa kuwapotezea nafasi za ufadhili katika mashirika mbalimbali vikiwemo vyuo vikuu, jambo ambalo si jema hasa katika kipindi hiki ambapo kusema kweli mambo yako wazi sana kuhusu masuala ya ufadhili wa kimataifa.
Source:MATONDO: KWA NINI NI VIGUMU SANA KUPATA "A" KATIKA VYUO VYETU? TUNAWAHUJUMU WANAFUNZI WETU ???
Daaah hii avatar yako nikimwachia laptop mama watoto akiiona hii naweza kuta screen imekuwa chenga tuuu,coz hata akiona sisimizi lazima amfukuze kwa kitambaa!!!Sasa huyu si atamtafutia nyundo kabisa!!!
 
Elimu ya bongo matatzo tu,nakumbuka kipindi niko first year udsm,kuna ticha alikuja akatuambia eti mwaka huo tulikua wengi mno so lazima ashike watu idadi ya shato 10,na kweli alifanya hivo.
 
walimu wengine kuwafelisha wanafunzi mavyuoni ni sifa hivyo hufanya hivyo kusudi.
nilipopkuwa chuoni siku moja darasa lilimuuliza mwalimu kwa nini ni vigumu sana kupata A na hali masomo si magumu kiasi hiki katika cozi hiyo?
mwalimu alijibu kama mnatafuta A hamtakaa mzipate ila nyinyi someni muelewe itawasaidia maishani kwani cheti ni karatasi tu haitakuwa na maana endapo utaambiwa uthibitishe kile kilichopo katika cheti ukashindwa. cheti hiki hakina maana.
hivyo kutopata A si maana kama hawana akili vyuoni huko ila tu uvivu wa kusahihisha kwa umakini, au kutotoa A hizi kwa makusudi. akupe A ili uvunje rekodi zake?
 
Watoto wanashinda kwenye @twitter na Facebook unafikiri watapata A vipi?

Google imemaliza kabisa uwezo wa watoto wa vyuo wa Kitanzania - Inawezekana ni mkakati mahususi wa CIA

On the serious note : Either amepata "A" or "C" kutoka chuo chochote hapa Tz, ninachelea kusema uwezo wao wote wawili upo sawasawa tu!!!

nani kakwambia vyuo vya nje wanafunzi wake hawatumii google kujisomea, huitumia sana na huwasaidia sana kwa hiyo google sio sababu ya kufeli kama unachukua material zisizoeleweka kutoka google ni shauri yako ila vitabu kabisa vipo huko na hutumiwa sana kuwasaidia wanafunzi kuelewa na kufaulu mitihani yao.
 
wengi tuna A za zima moto..wiki moja kabla ya pepa unchukua list ya maswali unaingia maktaba..mwisho wa siku unapata A.. Baada ya pepa hujui kitu.

hili ni tatizo la kimfumo ikiwa kuna utaratibu wa kupima uelewa utungwaji wa maswali ungekuwa kwa kusudi la kujua uwezo wa uelewa wa wanafunzi sio kukariri. watunga maswali wenyewe huyatunga kwa kudesa yalivyokuwa yametungwa awali ama miaka iliyopita,hawatungi swali jipya na endapo litatungwa wengi hufeli kwani huwa bado hawajapitia walimu wamekuwa wavivu ama sio WABUNIFU kabisa katika kuaandaa wanafunzi wa kuelewa wao ndio chanzo cha kukariri mwanzo mwisho. kwa nini kusingekuwa na oral final presentations,writing exams na vitu vingine ambavyo vingepima uelewa zaidi wa wanafunzi.sio kuzalisha empty heads soon after their final exams.
 
Sithan kama hizo ndio grade ambazo tunazitumia hapa UD. Nadhani sasa hivi wamebadilisha. Ninakataa. Ila mbona kupata A inawezekana tu ukiamua? Ukiingia na coursewrk ya maana UE mbona unapata tu. Mbona mimi kuna masomo nimeipata?

inategemea umesoma course ipi ?
 
ikiwa mwalimu mwenye somo kila siku anawaambia wanafunzi wake lazima mpungue humu tupate hewa mmejaa sana nawahakikishia mtapita 70 kati ya 120 hivi tu unategemea kupata A?
 
Nafikiri kupata A kwa wanafunzi ni Vyuo maana vipo vyuo hapa tz wanafunzi wanapata A za kutosha tu hata kama wanafunzi wake hawastahili. nimesikia wakati mwingine hupewa wakiwa hawajafikisha hizo alama ili chuo kionekane kinafaulisha hivyo kipate wateja wengi ,ila kuna vyuo A utaihangaikia utasoma wewe na hadi uipate ni shughuli kubwa. na vipo vyuo sio tu ni ngumu kuipata A ila pia walimu baadhi hubania tu yani wanajisikia tu kufanya maisha kuwa magumu hata kama umestahili kuipata hupewi.
 
Si kulikuwa na raia mmoja alikuwa anatusumbua sana chuo hasa hizi A na B+ zilikuwa za kugusa tu..Kuna siku alifanya presentation hatukuamini aliishia kuongea ka sekunde 45, aliganda ka dk 4 kila akijaribu kuongea anashindwa, hadi tunamaliza chuo alikuwa anazikimbia presentation.
Ila tulichokuja kugundua alikuwa mtu wa kumeza sana vitini (notes), kwa hy pepa ikija mulemule mtamkoma na ikipindishwa kidogo kilio.
Ninachotaka kusema elimu yetu ipo zaidi kwenye kumeza 'notes' tukishamaliza mitihani tunasahau kila kitu.
 
Back
Top Bottom