Kwanini ni vigumu sana kupata "A" katika vyuo vyetu? Tunawahujumu wanafunzi wetu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini ni vigumu sana kupata "A" katika vyuo vyetu? Tunawahujumu wanafunzi wetu?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Yo Yo, Feb 17, 2012.

 1. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Matokeo ya Mwaka wa nne Mlimani
  1. Kwa shahada ya kwanza pale Mlimani gredi zenyewe zimekaa hivi (kama hazijabadilika) A: 75-100, B+: 70-74, B: 60-69, C: 50-59, D: 45-49 na E: 0-44 2. Gredi za hapa Marekani (kutoka katika silabasi yangu katika darasa la Language and African Society) zimekaa hivi: A: 93-100, A-: 90-92, B+: 87-89, B: 83-86, B-: 80-82, C+: 77-79, C: 73-76, C-: 70-72, D+: 67-69, D: 63-66, D-: 60-62, E: 0– 59. Japo profesa unaweza kujipendekezea gredi zako mwenyewe, mfumo huu wa alama ndio umependekezwa na chuo kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza. 3. Hali ilivyo kule nyumbani (kama bado haijabadilika)

  • Utakuta darasa lina wanafunzi 100, na kati ya wanafunzi hawa pengine wawili, watatu na hata mmoja tu ndiyo atapata "A". Hata madarasa makubwa yenye wanafunzi 300, eti wanafunzi wanne au watano tu ndiyo wanapata "A". Kwa nini? Ni kwa sababu masomo ni magumu sana? Wanafunzi hawajisomei sawasawa (Na kama hawajisomei ni kwa nini?), maprofesa hawafundishi vizuri kiasi kwamba wanafunzi hawawaelewi? Au maprofesa wanatunga mitihani migumu kupindukia? Au pengine wanafunzi wa vyuo vikuu vyetu ni mbumbumbu na hawana uwezo wa kupata A?

  • Ninacholalamikia hapa siyo kila mwanafunzi kupata A bali ule ugumu uliopo wa kupata alama hizi kwani siamini kama kweli eti katika darasa la wanafunzi 300, ni wanafunzi watatu au wanne tu ndiyo wana uwezo wa kufaulu vizuri. Kama hivi ni kweli basi ni wazi kuna tatizo kubwa katika mfumo wetu wa elimu.
  4. Hali ilivyo hapa Marekani

  • Hapa kupata A ni jambo la kawaida na maprofesa na wanafunzi wanalijua hili. Mahusiano kati ya wanafunzi na maprofesa ni ya wazi na wanafunzi wanaweza kuuliza maswali na kujadili masuala ya gredi watakazozipata na maprofesa wao kwa uwazi. Hali hii inasababisha matatizo fulani na haya nitayaongelea siku nyingine.

  • Kwa wanafunzi wanaotegemea kuendelea na shahada za uzamili na uzamivu ni lazima wahakikishe kwamba wanapata A kwa sababu ushindani wa kupata ufadhili ni mkubwa sana na vyuo vingi vinataka wanafunzi ambao ni bora kabisa. Kwa ujumla alama za B, na hata B+ na pengine A- hazimsaidii sana mwanafunzi kuweza kujiunga na vyuo vikuu vyenye hadhi kama Harvard, Yale, Columbia, UCLA, Stanford, Berkeley na vinginevyo
  5. Uzoefu Wangu

  • Nina uzoefu na uteuzi wa wanafunzi wa shahada za uzamili na uzamivu hapa Marekani na huwa nashangaa sana kugundua kwamba kwa kawaida waombaji kutoka Afrika huwa na alama za chini sana hasa ikilinganishwa na waombaji kutoka sehemu zingine duniani kama China, Korea, Ulaya, Amerika ya Kusini na hata nchi za Uarabuni. Maprofesa hapa huwa wanajiuliza inawezekanaje mwanafunzi mwenye azma na ari ya kujisomea ashindwe kupata A (75) ambayo hapa ni C? Na kama hakuna profesa wa kuwafahamisha wanakamati wenzie wanaofanya uteuzi kuhusu mambo yalivyo, mara nyingi maombi ya wanafunzi kutoka Afrika huwa hafifu sana na huishia kutupiliwa mbali. Ndiyo maana nahoji hapa kwamba pengine tunawahujumu vijana wetu kwa kuwapa alama za chini na kuishia kuwakosesha ufadhili ambao ungewawezesha kusomeshwa bure. Na sijui mfumo huu unamsaidia nani.
  6. Ilivyokuwa Kwangu

  • Mwaka 1997 nilipata nafasi ya ufadhili wa kusoma shahada za uzamili na uzamivu katika Idara ya Isimu pale UCLA ambapo pia nilitakiwa kufanya kazi kama mwalimu msaidizi wa Kiswahili. Barua ya mwanzo niliyopata ilikuwa na masharti mawili yaliyonichanganya na kuninyima usingizi. Sharti la kwanza lilisema kwamba ilikuwa ni lazima nipate "first class" katika shahada yangu ya kwanza na la pili ni kufanya mtihani korofi wa GRE.

  • Sharti la kwanza liliwashtua watu wengi sana na niliambiwa kwamba kwa muda mrefu kulikuwa hakujawa na mtu aliyepata hiyo "first class". Niliambiwa kwamba pengine hawa jamaa wa UCLA walikuwa hawataki niende na niliambiwa kuachana nao kwani walichokuwa wananiomba kufanya kilikuwa hakiwezekani. Kilichonishangaza ni kwamba kulingana na matokeo yangu ya miaka mitatu iliyopita, ningeweza kupata hiyo first class kama ningepata angalau A nne tu katika mitihani yangu ya mwisho ya mwaka wa nne. Na kupata A nne katika masomo 10 niliyokuwa nikisoma eti ilikuwa haiwezekani. Sikukubali!
  7. Nilichokifanya na Matokeo Yake

  • Sijawahi kusoma kwa nguvu zaidi, ari zaidi na kasi zaidi kama katika kipindi kile katika maisha yangu yote mpaka nikapachikwa majina ya "Librarian", mkazi wa "Special Reserve", "Aliyetumwa na kijiji" na mengineyo. Sikujali!

  • Matokeo ya mwaka wa nne yalipotoka nilikuwa nimepata A tisa, B+ moja na B moja. Nilikuwa nimeipata hiyo "first class!" tena nzuri. Haraka haraka niliyatuma matokeo hayo UCLA na msimamizi wangu (ambaye anafahamu ugumu wa kupata first class) alifurahishwa sana kiasi kwamba aliiomba kamati ya ufadhili kufuta sharti la mimi kufanya mtihani wa GRE. Habari hizi kuhusu GRE hata hivyo zilikuwa zimechelewa kwani tayari nilikuwa nimeshaanza maandalizi na nilikuwa nimeshalipia ada (dola 120). Niliufanya mtihani huu ili kujipima nguvu tu lakini first class tayari ilikuwa imesharekebisha mambo. Na hivi ndivyo nilivyoweza kusomeshwa UCLA kwa miaka sita (mitatu shahada ya uzamili na mitatu shahada ya uzamivu) huku nikilipiwa karibu dola 30,000 kwa mwaka.
  [​IMG] Risti ya malipo ya GRE

  • Ati, kwa nini ni vigumu sana kupata A na hatimaye "first class" katika vyuo vikuu vyetu? Tatizo hasa ni nini? Ni mfumo wa elimu tuliorithi kutoka kwa Waingereza? Pengine inabidi tulifikirie jambo hili kwani inawezekana tukawa tunawahujumu wanafunzi wetu kwa kuwapotezea nafasi za ufadhili katika mashirika mbalimbali vikiwemo vyuo vikuu, jambo ambalo si jema hasa katika kipindi hiki ambapo kusema kweli mambo yako wazi sana kuhusu masuala ya ufadhili wa kimataifa.
  Source:MATONDO: KWA NINI NI VIGUMU SANA KUPATA "A" KATIKA VYUO VYETU? TUNAWAHUJUMU WANAFUNZI WETU ???
   
 2. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2012
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Omba kazi ya ufundishaji, halafu kifike kipindi cha usahihishaji, hapo ndipo utakapojua kuwa ni kwanini A hazipatikani kwa wingi. I bet wewe unaweza usitoe hata B+ kwa aina ya wanafunzi waliopo vyuoni leo.
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  A college za bongo zinapatikana sana!
   
 4. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Tatizo nini? hawana akili au? inawezekana kuwa wanafunzi wa tz wasiwe na akili zaidi ya wa nchi nyingine?? na ni kwanini hawana akili kama ndio sababu.....
  mfumo wetu wa elimu unajenga wanafunzi wasome na waelewe mwisho wa siku wapate A?
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Feb 17, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,336
  Likes Received: 1,803
  Trophy Points: 280
  Wale walimu wamepata ile kazi kwa msuli kweli kweli...they like to see few reach where they reached...the GPA of above 3.8 in the past
   
 6. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2012
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hebu fikiria mchapo huu, ni jana tu nilikuwa naongea na mwanafunzi mmoja wa Mwalimu Nyerere Memorial University, nikamuuliza vipi matokeo yako ya mwaka wa kwanza? Akasema ni mazuri ana GPA ya 4.1 ambayo kiukweli ni matokeo mazuri sana yenye A kibao, yeye anasema ni mwanafunzi wa Economics of Development, nikamwambia aniambie kwa kifupi tu course yake inahusu nini, chali hakujibu lolote, nikamwuuliza achague eneo lolote katika course yake (topic) ambayo yeye yuko mahiri zaidi, akachagua micro economics, nikamuuliza ni ma-author gani ambao ni nguli katika uwanda huo? Chali, hakuweza kumention hata mmoja, na cha kusikitisha zaidi I'm telling truth aliuliza ma-authors ndio kina nani? Sasa that's it, sio kwamba A hazipatikani, no zinapatikana katika vyuo flaniflani kirahisi tu pengine, lakini jee hao ni A students? Jibu utakuwa nalo mwenyewe.
   
 7. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #7
  Feb 17, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Mfumo wa University/College kwa hapa bongo ni mbovu sana!! mwalimu wako wa darasani ndiye atakayesahisha mtihani wako wa semester na kukukabidhi GPA...this is very big prob by the way
   
 8. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,378
  Trophy Points: 280
  Sithan kama hizo ndio grade ambazo tunazitumia hapa UD. Nadhani sasa hivi wamebadilisha. Ninakataa. Ila mbona kupata A inawezekana tu ukiamua? Ukiingia na coursewrk ya maana UE mbona unapata tu. Mbona mimi kuna masomo nimeipata?
   
 9. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Same way jana niliongea na dent wa mwaka wa kwanza Mwalimu Nyerere College....same nae anasomea Economics Development...na mada ambayo lecturer wake ana boa ni ile ya macro-economics..nilivyomuuliza kuhusu matokeo akasema anatarajia suppl 2 na results bado haijatoka!! Bt she is somehow empty kwa anavyojieleza!!
   
 10. CHIEF MP

  CHIEF MP JF-Expert Member

  #10
  Feb 17, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 1,569
  Likes Received: 344
  Trophy Points: 180
  Mkuu nmefurahshwa xana na ufafanuz wko thabiti!Mi ni undergraduate ktk chuo kikuu kimoja hapa tz!Ukwel ni kwamba TATIZO NI MFUMO 2lorith toka kwa wakolon!Istoshe PYRAMID SYSTEM ndo kinachotuua African states as some lecturers feel hppy wen FEW reach ze top
   
 11. Lyceum

  Lyceum JF-Expert Member

  #11
  Feb 17, 2012
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  Kutana na mwenye A then mwambie aitafsiri kwa vitendo utalia. Mara nyinigi nimekutana na wenye PASS field wapo fit kwa vitendo kuliko hayo ma A. Nadhani hata mwanafunzi anapotamani A ajiulize kama ataweza kuitetea kibaruani. A zimetuumbua wengi
   
 12. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo kwa maelezo yako tatizo ni wanafunzi wenyewe? hivi kweli unataka kusema ni woote maana kuna baadhi ya fani hakuna first class kabisa miaka zaidi ya mi5....hiki kizazi ni vipi? na kama huyo kwa maelezo yako kapata GPA hiyo lakini ianonekana ni bonge la kilaza....je tatizo ni yeye mkuu?????? tafakari..

  wow.....unasomea kozi gani mkuu?
   
 13. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #13
  Feb 17, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  mkuu kwanini mtu upate A na ushindwe kuitetea kibaruani?? tatizo nani? mwanafunzi au mwalimu au nini? au CCM arifu?
   
 14. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #14
  Feb 17, 2012
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  You see? Picha inakuja yenyewe
   
 15. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #15
  Feb 17, 2012
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Good observation, na mimi binti yule nilimueleza awe tayari kuprove, kwa watu makazini ama kokote atakapo pata nafasi, kivitendo na kwa uelewa kwamba kweli ni wa alama hizo. Sababu ukiwa na Cheti chenye A kibao na watu watakua wanakuexpect kudeliver ki-A-A tu.
   
 16. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #16
  Feb 17, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  post zenu ni coincidence....
  au ni sawa kama alivyosema Prof matondo..
   
 17. CHIEF MP

  CHIEF MP JF-Expert Member

  #17
  Feb 17, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 1,569
  Likes Received: 344
  Trophy Points: 180
  Mi nasoma shahada ya biashara ktk menejiment ya utalii na ukarim!Ninachokiona ni kuwa wapo wachache wanaopata A's ambapo weng wao hawabahatish pa1 na kwamba few ktk hao wanababaisha!kwan elim ya chuo ka unajua unajua tu ukisubir kubahatisha inakula kwako!
   
 18. Josephine03

  Josephine03 JF-Expert Member

  #18
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 752
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Utakuwa umedesa sana vibuti na nondo nyingine kama si uongo tutajie somo ulilopata A kama sio la ngwini na tupe hesabu kama haujaegemea kuti kavu ndo nyie mmeambiwa mkiulizwa swali after exam mmeshasahau.
   
 19. obsesd

  obsesd JF-Expert Member

  #19
  Feb 17, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 1,226
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  sijui kwakweli, labda nwdays hatuna akili,
  lakini kule bcom kule kuna walimu wanajua kukomoa sijaona?? anatunga mtihani mgumu majibu yake mwenyewe hana hadi aende kudownload kitabu tena unalipia uko uko online!
  ss maisha gan hayo, wengi wao pia wanakomoa watu wawaogope kwa idadi ya sup!
   
 20. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #20
  Feb 17, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,255
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Mwalimu Nyerere Memorial Academy wako shallow sana, sasa we ulikuwa unategemea nini!?
   
Loading...