Kwanini ni vigumu sana kufurahia matokeo hata kama umeshinda? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini ni vigumu sana kufurahia matokeo hata kama umeshinda?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Profesa, Nov 7, 2010.

 1. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Total Population in Tanzania: about 35 M
  Eligible population for voting: estimates from NBS projections 47% of the population about 16 Million above the age of 18.
  Those who registered for voting: About 20 Million (NEC, 2010)! (against NBS projections on eligibel voters, those who are above 18 years of age)
  Voted: About 9M
  The elected president votes: About 5 M = 25% of all registered voters
  = 32% of all eligible voters

  Source: Own calculations from NEC website: The National Electrol Commission of Tanzania - Homepage [online] and from the NBS Tanzania
  [online]

  Hipothesis: Watu wengi hawaendi kupiga kura kwa sababu:
  1. Miundo mbinu ya upigaji kura imevurugwa a. haifikiki, b. haieleweki c. jina langu halipo
  2. Hawakupata msaada wowote kutokana na matatizo yaliyokuwa yanawazuia kuweza kupiga kura
  2. Hawana imani na chama tawala
  3. Hawana imani na chama chochote
  4. Hawakuona mabadiliko yeyote katika maisha yao tangu waanze kupiga kura
  5. Uchaguzi haukuelewaka
  6. Vyama havikueleweka
   
 2. D

  DENYO JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Huwezi kufurahia ushindi wa wizi -anafurahia ushindi ni yule aliyepata ushindi wa kweli, hawa wamechakachua sasa wafurahia nini -hutuitaki tume watoke
   
 3. P

  Patrick New Member

  #3
  Nov 7, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Siwezi kukupinga kwa sababu ni ntazamo wako, Ila mimi nina mtazamo tofauti kidogo na wewe. Mimi naamini kuna watu zaidi ya milioni nane waliojiandikisha kupiga kura na ambao hawakupenda kutopiga kula ila walikuwa nje ya makazi yao siku ya kupiga kura. kwa mfano mtu yuko mwanza siku ya kupiga kura wakati siku ya kujiandikisha alikuwa songea. Hawa watu wapo wengi na hawakujitokeza kutangaza kutoridhishwa kama wanafunzi walivyofanya. Na chama CM kinajua kuwa hawa watu walio barabarani wanajua kero za nchi hii na wasingeweza kukipa kula. Haiingii akilini, kama mtu yuko songea na ana kitambulisho cha kupigia kula na tumewekeza kwenye mitambo ya kisasa ya kuchkcha kura na kura za urahisi zinakwenda makao makuu, kwa nini asipatiwe haki yake ya kupiga kura hata kama amejiandikisha mtwara? anyway chama cm na watoto wa maisha bora labda wanajua ukweli.
   
 4. M

  Msuruhishi Member

  #4
  Nov 7, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 95
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  Watu wote waliojiandikisha wasingeweza kupiga kura. Sina data kwa sasa lakini ninaamini huu ni uchaguzi mkuu wa kwanza tangu tuingie mfumo wa vyama vingi kwa wapiga kura kujitokeza wachache kiasi hicho! Sasa kama alivyoeleza Prof. Lipumba, Rais unayechaguliwa na asilimia 27 ya Watanzania wote wenye uwezo wa kupiga kura una jeuri yoyotee ya kufurahia ushindi? Hata hivyo nadhani CCM ndiyo inastahili kujilaumu kwa hali hiyo. Kwanza, kwa makusudi walitumia JW na pia Polisi kujenga hisia miongoni mwa WaTz kuwa siku ya uchaguzi hali ya usalama itakuwa tete. Kitendo cha JW kutoa tamko juu ya hatari ambayo waTZ wangejiingiza kwa kupinga matokeo ya kura ya urais iliashiria shari. Pamoja na kelele zote zilizopigwa juu ya tamko hilo la JW, CCM walisema lilikuwa halali. Lakini naomba tujiulize: Kama JW na CCM wangefikiri kuwa Dr. Slaa angeweza kuibuka mshindi, wangesema walivyosema kuwa asije akatokea mtu kupinga matokeo ya uchaguzi wa uraisi? sababu kubwa ya pili ya watu kutojitokeza kwa wingi kupiga kura ni vitisho kutoka kwa JESHI LA GREEN GUARDS. Kwanza ieleweke kuwa hao waliowekwa kwenye kambi za mafunzo maalumu HAWAKUWA VIJANA WA GREEN GUARDS BALI WAHITIMU WA JESHI LA MGAMBO. Hao waliwekwa kambini na kati ya kazi muhimu walizoagizwa ilikuwa kuwatambua wapiga kura waliokuwa na mwelekeo wa upinzani na kuwatisha wasiende kupiga kura. Na siyo Green guards tu. Watendaji wote wa chama na serikali kutoka ngazi ya wilaya hadi kwenye nyumba kumi walikuwa na maagizo mahususi ya kuhakikisha wale wenye sympathy na upinzani hawapigi kura na hili lilifanyika kwa njia nyingi ikiwa ni pamoja na kutoonyesha majina yao kwenye orodha za wapiga kura. Aidha dkatika kanda ya Ziwa hususan mikoa ya Mwanza na Kagera, hata wagombea wa Udiwani walionywa kuwa endapo katika kata zao wao wangepata kura zaidi kumzidi mgombea ubunge wa CCM au mgombea Urais wa CCM wangeweza kunyang'anywa kadi ya CCM na hivyo kupoteza udiwani walioushindia. Katika hali kama hiyo, tulitegemea nini?
   
Loading...