Kwanini ni vigumu kuisambaratisha Chadema kwa Mizengwe?

STEIN

JF-Expert Member
Aug 29, 2010
1,765
2,000
Ndugu Zangu wanaJF, wapenda mabadiliko, Wasomi, waliochoka na Uongozi mbovu wa CCM toka Uhuru wa nchi hii miaka 49 iliyopita, naomba niwasilishe kisehemu tu ya utafiti mdogo nilioufanya baada ya matokeo ya uchaguzi.

Kwanza nianze na jamii ya waTZ waliokiunga mkono chadema wakati wa kampeni hadi siku ya kupiga kura ni wa aina kuu tano.

Aina ya kwanza ni vijana ambao waliahidiwa na CCM toka mwaka 2005 kuwa wangeishi maisha Bora ambayo waliamini mara tu baada ya JK kushinda angeweza kuwasaidia wakapata kazi nzuru yenye ujira mzuri, lakini wamekuwa mashahidi wakati huu wa kampeni wakiwa wamechoka na maisha kuzidi kuwa magumu na hata kazi zimekuwa ngumu kupatikana mtaani kwahiyo wakapoteza imani na CCM pamoja na JK wake na kuanza kazi ya kuipigia CDM debbe hata bila malipo yeyote.

Pili ni Vijana ambao ni wasomi wa nchi hii kwa ngazi ya Form Six, Diploma, Degree, Masters, PHD ambao kila moja ana sababu zake za kutoikubali CCM na uongozi wake kwa mfano Form six ana matatizo ya ajira na maisha kuwa magumu, Wengine wamesoma lakini kazi hakuna na sehemu nyingi wanakosa nafasi ya kufanya kazi kutokana na Wageni wengi kuchukua nafasi zao huku waTZ wakihaha huku nakule huku bodi ya mikopo ikiwavutia punzi warudishi mikopo waliyopewa. Kwa hiyo utaona ni vigumu kuwabadilisha watu hawa na kuanza kuishabikia CCM mwaka 2015. Kwa upande wa vijana wenye masters na PhD kwa kweli hawa huwa si watu wa kubadilika maana wanafahamu jinsi hali yao kimaisha ilivyo mbaya kwani mshahara wanayopewa ni midogo mno hata haitoshi.

Tatu ni Wafanyakazi ambao kimsingi ndo wanaifanya CDM ing'ae kutokana na sera zake nzuri na CCM kuonyesha kutowajali ambao wanaamini kwamba hata mabadiliko yeyote yatakayofanywa na CCM kwenye maslahi yao ni kutokana na shinikizo kutoka vyama vyao kama TUCTA, CWT etc na si serikali ya CCM. Na hawa ndio wanatumikia taifa hili na ndo wanakatwa kodi kubwa na kupewa mshahara mdogo. Hawa kimsingi si watu wa kuwahonga kirahisi maana kila utakacho wapa watasema ni haki yao.


Kundi la nne ni wazee ambao wameasi kutoka CCM kwa manyanyaso mbali mbali kama wale wa EAC wanaohangaika siku zote mpaka sasa, kundi hili ni dogo lakini si lakudharau maana ina watoto na wajukuu. hawa kuwabadilisha ni kazi ngumu.

Kundi la mwishi ni watoto wa shule za msingi ambao ni taifa la 2015, hawa waelewa na wanafuatilia sana mambo yanayoendelea kwenye siasa za nchi hii, wanapenda sana wata wanaoshughulikia mafisadi ambao ni Wapinzani wa kweli. Kundi hili kulibadilisha mawazo ni kitu ambacho hakiwezekani kabisa maana huamini kwa asilimia mia moja wanacho ambiwa na wakubwa zao.


Kwa ujumla ilikuwabadilisha watu hawa mawazo kabla ya 2015 itabidi CCM wafanye yale ambayo CDM na mgombea wake wa Uras wameyahubiri wakati wa kampeni. Kwa kweli waTZ wameielewa CDM na sera yake ya Elimu Bure, Afya Bure, Makazi Bora na kushughulikia mafisadi. Kwa sasa waTZ wanaamini yote haya yanawezekana.

Ukitaka kuhakikisha angalia Coments za watu kwa Zito kupitia mitandao mbali mbali na magazeti.

Kwa watu wengi wa mjini wanafikiri ni kama CCM watafanikiwa kama ilivyo kwa NCCR na CUF, ukweli ni kwamba hizi propaganda za magazetini yanaishia Mjini hapa.

Walioko mikoani ni mashahidi wataendelea kutupa data za kutosha.

Naomba kuwasilisha.
 

DENYO

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
698
195
UMENENA UKWELI MKUU CHADEMA HAISAMBARATIKI, HII KWA SASA NI TAASISI INA HAZINA KUBWA NA NGUVU YA UMMA. Kwa faida ya wale ambao hawakuipata TAARIFA KAMILI YA CHADEMA
Najua kuna wengi huenda hawakuipata hii. Nimeitafuta sijaiona jamvini baada ya rafiki kuniambia niitafute. Ila nimeikuta feacebook yake. Wanaoitafuta kama mimi, hii hapa

Msimamo wa Chadema haujabadilika

by Dr. Wilbrod Slaa on Tuesday, December 14, 2010 at 7:29pmKuna taarifa ambazo zimekuwa zikiandikwa na kuripotiwa na vyombo vya habari ambavyo zinaashiria kuwa Chadema tumebadili msimamo wetu kuhusu masuala ya uchaguzi.

Hakuna mahali popote Chadema imebadili msimamo wake na kusema kuwa Kura hazijaibiwa au kuchakachuliwa. Taarifa niliyotoa jana kwa TBC ilieleza wazi kuwa Kamati Kuu, ilipokea na kujadili na kuridhia mapendekezo yote yaliyowasilishwa na Sekretariat ya Chama kuwa Chadema imekataa matokeo ya Uchaguzi kutokana na irregularities 15. Chadema inaamini kuwa iwapo Katiba ya nchi isingelikuwa imezuia kuhoji matokeo ya uchaguzi Mkuu wa Rais mahakamani, matokeo hayo yangeliweza kubatilishwa. Kwa vile Katiba inakataza kuhoji matokeo kuhojiwa mahakamani, basi japo Kikwete's Presidency ni Lawful it is Illegitimate.

Chadema ilitumia maneno ya kiingereza kuonyesha tofuati kubwa kati ya maneno hayo mawili. Huo ndio msimamo wa Chadema toka mwanzo na haijawahi kuyumba, japo maneno ya kiswahili yamekuwa yakipewa tafsiri tofauti na watu mbalimbali. Ni kwa msingi huo, Kamati Kuu ikasisitiza " Kuundwa kwa Tume Huru" kuchunguza Dosari " Irregularities" hizo kubwa katika uchaguzi. Nasisitiza, Chadema ni Chama ambacho toka mwanzo ilisisitiza kuwa "Haiko Tayari kuingia Ikulu kwa kumwaga Damu ya Watanzania".

Inawezekana wanaopenda na kufurahia vurugu, Chadema haiko tayari kwa hali hiyo. Tunasukumwa sana na wapenzi na wanachame wetu kutoka mitaani na kuandamana, na ndicho pia wanachotaka ndugu zetu akina Mwanakijiji. Maandamano, (ya amani au ya kushinikiza), kwa watu wanaojua mchakato wa demokrasia ni hatua ya mwisho kabisa baada ya njia zingine zote kushindikana. Pili, ili Tanzania isiingie katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015 kwa Katiba na Sheria mbovu kama tuliyonayo leo, Chadema inasisitiza upatikanaji wa Katiba mpya, Shirikishi na ya Wananchi.

Upatakanaji wa Katiba hii utakuwa na mchakato, na kama Serikali haitaki, basi Chadema kwa kushirikiana na wadau na watu mbalimbali wakiwemo wananchi itatutumia njia zote zinazoweza kuipatia nchi Katiba ya Wananchi. Yote haya ni mchakato, na kwa mtu yeyote anayoamini kuwa mchakato huchukua muda, basi atakuwa mvumilivu. Hakuna sababu ya kutumia lugha kali, kukashifiana na kutukanana japo jamvi letu ni mahali ambapo "we dare to speak". Tukivumiliana na kuheshimiana tutafika salama bandarini.

Tukikurupuka tunaweza pia tusifikie lengo tunalotaka. Hekima na busara vikitawala na kuongoza matunda yatakuwa mazuri kwa Taifa letu. Taifa ni letu tukilibomoa hatuna pengine pa kwenda, labda tukiamua kulowea penginepo. Tukikurupuka tunaweza kuwaumiza wanaohusika na wasiohusika. Uvumilivu na Busara daima huvuta heri.
Source: Gonga hapa Msimamo wa Chadema haujabadilika | Facebook


NYONGEZA: Kuna thread imewekwa hapa chini na Mwanajamii mmoja (Chapakazi) anauliza tofauti ya maneno haya mawili (Lawful na Legitimate). Kwa uelewa wangu. Naomba niiongeze hapa kwa mtiririko sahihi. Unaweza toa usahihi zaidi


Moja ya tafsiri za legitimate zilizoko kwenye link hii define: legitimate - Google Search


Zinasema kitu
legitimate ni kile ambacho kiko affirmed to be just na in accordance with recognized or accepted standards or principles.


Na kitu
lawful ni kitu ambacho kiko recognized or sanctioned by law(lawful: meaning and definitions — Infoplease.com.


Kwa upeo wangu hii inamanishaa kitu kinaweza kuwa recognize na sheria lakini kisiwe just kwa sababu hakikiendana na accepted principlesTukitumia mfano wa tukio lenyewe naweza kusema hivi,

Sheria inasema Raisi ni Raisi kwa kutangazwa na tume (lawful) lakini ili atangazwe lazima kanuni (principle) kadhaa zifuatwe.


Hivyo kama kanuni hazikufuatwa lakini katangazwa (kama sheria inavyotaka) na tume ya uchaguzi basi ni lawful kwa sababu katangazwa kisheria na tume yenye mamlaka ya kisheria kutangaza lakini kama kanuni za kufuatwa ili atangazwe zimevunjwa tunasema ni illegitimate kwa sababu principle s zimekiukwa.


Kwa msaada zaidi gonga hili link uone mfano kule Georgia

http://georgiandaily.com/index.php?o...2829&Itemid=68
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom