Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,864
- 155,822
KWA NINI NI RAHISI MWANAMKE KUGUNDULIKA ATOKAPO NJE YA NDOA?
Hakika mwanamke ni rahisi sana kugundulika endapo anatoka nje ya ndoa, kwa sababu Mwenyezi Mungu amemuumba mwanamke aishi na mwanamme mmoja tu, na hakumpa kabisa uwezo wa kuonyesha mapenzi kwa watu wawili tofauti kwa kiwango sawa, hivyo mwanamke akiamuwa kutoka nje ya ndoa ni muda mchache mumewe hugundua na kama mume ni mjanja kidogo tu, basi anaweza kumgundua mke wake siku ya kwanza anayopata mwanamme mwengine nje ya ndoa. Inawezekana zipo sababu za ziada zinazowafanya wanawake kugundulika kiurahisi pindi atokapo nje ya ndoa yake, lakini mimi nitazionyesha sababu tatu pekee, ambazo kwangu mimi hizo ndizo kuu, na nyenginezo zilizopo nitawaachia ukumbi wengine na wao waziorodheshe kwa mujibu wa uzoefu wao.
Kwanza, ni ‘Jaala’ ya Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu ameiumba nafsi ya mwanamke ipende mwanamme mmoja kwa wakati mmoja, halikadhalika ameuumba mwili wa mwanamke umridhishe na kumburudisha mwanamme mmoja. Kisheria, hakuna rukhsa ya kidini mwanamke aliyoamriwa kuolewa na wanaume zaidi ya mmoja, kwa sababu moyo wake hauwezi kugawika kupenda zaidi ya mmoja na akaonyesha uwiano sawa, ingawa hali hii pia hutokea kwa wanaume wenye wake zaidi ya mmoja. Lakini wanaume angalau wamepewa uwezo wa kuficha mapenzi yao, hivyo kitu hicho huwasaidia. Hivyo mwanamke akichepuka lazima adharau kumoja apende kwa dhati kwengine, sasa kwa kitendo hicho ndio maana huwa ni rahisi kugundulika, kadhalika endapo akiutumia mwili wake kuburudisha mchepuko wake basi maumbile yake hayatakaa kimya, yatamshitaki tu kwa mumewe ikiwa mume huyo si ‘mume bwege’.
Pili, mwanamke ni mtu wa fakhari ya mapenzi, maana yake nini? Hii ina maana mwanamke siku zote hutaka kuona yeye ndiye anaependa zaidi kuliko mwenza wake, iwe kwa kutamka, ishara na hata kwa vitendo, hivyo hata kama itakuwa wako mbali mbali na mchepuko wake, yeye hupenda wawe wanawasiliana kila wakati, hasa kwa zile siku za awali za mahusiano, sasa hapa ndipo mara jungu hulikoroga kwa kujisahau kwamba pale alipo amemilikiwa na kuanza huonyesha ishara kwa mchepuko wake bila kuzingatia kwamba labda mumewe atagundua, aidha humuacha mumewe chumbani yeye akabaki sebuleni kwa kisingizio cha kuangalia TV, huku akichati na huo mchepuko wake au hata kumpigia simu kuzungumza nae, na huu ni udhaifu maalum wa kimaumbile ambao Mwenyezi Mungu amewaumbia wanawake na maisha hawataweza kubadili hili.
Tatu, jambo jengine ambalo kwa Makala hii ni la mwisho, ni yale maumbile ya mwanamke kupenda sana vitu vipya, sina maana kwamba mwanamme hapendi, hapana, lakini kimaumbile hasaa, wanawake hupenda zaidi vitu vipya, pindi mwanamke anapo pata kitu kipya, basi anaweza hata kukisahau kile cha zamani, sasa kwa muktadha huu, pindi mwanamke anapoamua kuwa na mtu nje ya ndoa ambaye kwake ni mpya, hapo huweza hata kumdharau mume wake na kuwa tayari kwa lolote, alimuradi amridhishe yule mpya zaidi kuonyesha kwamba anampenda sana, ili na yeye arejeshewe mapenzi kama yale na mtu huyo, sasa hapo ndio mara mambo yaliyofichika hupata mwanya wa kufichuka.
HITIMISHO;
Kama nilivyoeleza katika ufunguzi wa makala hii kwamba si lengo lagu kuonyesha ujabari wa mwanamme kwa mkewe au udhaifu wa mwanammke kwa mumewe, lengo ni kufikisha mawazo yangu kwa wenzangu ili tuokoe maisha yetu ya ndoa, ndoa ambayo huzaa watoto, watoto ambao kutegemea malezi, malezi yanayoaminika kuwa ni bora ni yale ya pande mbili, yaani Baba na Mama, ambapo tafiti zinaonyesha watoto wengi wananyanyasika na kuathirika kisaikolojia pale wazazi wao wanapoachana na kuambulia malezi ya upande mmoja.
Na nirudie tena kusema, licha ya sababu nyenginezo zinazotajwa za ndoa kukatika ambazo hizi mimi sizikubali, lakini sababu kuu na ya msingi ninayoiamini na kuikubali kuwa ni ya kweli ni pale wanandoa mmoja wapo anapoiacha ndoa yake na kuanzisha mahusiano na mtu mwengine.
Nitoe nasaha tudumu kwa uaminifu katika ndoa zetu, tuwe waaminifu, kila mmoja atekeleze wajibu wake wa msingi na wajibu mwengine ili kunusuru hii hali, ambayo kwa sasa imekuwa mtango unaotambaa, kila kona unayopita habari ndio hio mambo yamekuwa ‘shaghala baghala’.