Why can't we(Africans) set apart woman and motherhood.
Africa kama wewe ni mwanamke basi ni kama vile hujakamilika bila kuzaa.
Karibia kila mwanamke Africa anataka azae.
Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikitafuta mwanamke ambaye yeye hana mpango wa kuzaa wala kuwa na mtoto. Si jambo la ajabu katika nchi za nje ya Africa, nchi za wenzetu kuna idadi kubwa sana ya wanawake ambao wao wamefanya maamuzi ya kutokuwa na watoto na hakuna mtazamo wowote usiofaa ambao wamepokea kutoka kwa watu wengine. Kwanini ? Kwa sababu nchi za wenzetu kuwa mwanamke hakumaanishi kwamba lazima uwe mama.
Sina tatizo lolote na suala la uzazi na nawapenda sana watoto. Ila hili suala linapaswa kuwa maamuzi ya mtu na si sheria au kanuni kama ilivyo Africa.
Baadhi ya watu kuchagua kutozaa hakumaanishi binadamu wataisha. Kumbuka kuna watu wengi ambao wanapenda kuzaa. Kwahiyo watu wachache wakiamua kutozaa wala haiwezi kuwa tatizo.
Lakini kuzaa ni sehemu ya tamaduni ya Muafrica. Trust me, hata hapa kuna watu watakuja kunikashifu na kuhisi nna matatizo ya uzazi. Yaani kama vile hili suala la ndoa bila watoto ni mwiko Africa. Ukitaka kuoa mwanamke ambae hana mpango wa kuzaa basi utasubiri sana,
Niulize mimi, nimeanza kutafuta huyo mwanamke muda mrefu sana na nahisi kabisa kama hayupo. Nakutana na wanawake wagumba ambao nao wananiogopa KABISA eti wanahisi nimepewa masharti na mganga wa kishirikina nisiwe na mtoto au wanaogopa labda ntawatoa kafara, khaaa! Mimi na ushirikina ni ardhi na anga, viko mbali sana na havitakutana.
Yaani ukitaka ndoa bila watoto Africa basi utaishia kufunga ndoa na mwanamke mwenye umri mkubwa ambae ame-hit menopause au mwanamke mgumba ambae hatoacha kunywa mitishamba ili apate mtoto.
Kwa mwanamke wa Africa hili suala haliingii KABISA akilini eti awe amechagua kutokuwa na mtoto kama MIMI au watu katika nchi zilizoendelea ambao wanachagua.
Swali muhimu: Kwanini ni ngumu kuamua kutokuwa na mtoto Afrika? Labda nipate mawazo yenu pia.
Swali la msingi ni: Why can't we (Africans) set apart woman and motherhood.