Kwanini ni muhimu kwa Baba kuonyesha upendo wa dhati binti yake?

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
1,863
2,000
Inaaminika huenda Baba mzazi akawa ndio Mwanaune pekeee atakaye mpatia binti wake upendo wa dhati kabisa na wa kutoka moyoni, na huenda Binti hatakuja kuupata upendo wa aina hiyo kutoka kwa mwanaune yoyote yule tena.

Hii ni kwa sababu mara nyingi kwenye maisha yake ataishia kuumizwa sana na Mwanaume, ataishia kunyanyasika na hata kama atapendwa basi ni ule upendo wa juu juu tu.

Hivyo Wababa jitahidini mno kuhakikisha kwamba kipindi binti yuko mikononi mwako nasi anapata upendo mkubwa mno, ili huo upendo uje ku compensate manyanyaso yanawo weza kuja kumpata mbeleni.
 

Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
6,689
2,000
Pamoja na upendo wa kutosha pia ni muhimu kumlea katika maadili sahihi na katika mazingira ya aina yoyote, sio kupendwa na kudekezwa pekee, maisha ni zaidi ya hayo
 

Agenda1

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
1,087
2,000
Nakubaliana na wewe mtoa mada, sambamba na upendo, pia tuwajengee mazingira mazuri ya kujitambua na kujiamini iwasaidie kufanya maamuzi sahihi huko mbeleni.
 

Agenda1

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
1,087
2,000
Wazazi wenye watoto wa kike, kujeni ktk uzi huu tuongezeane maarifa! maana changamoto za malezi ya mtoto wa kike zimeonekana kuongezeka sana zama hizi
 

Willard Jonnes

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
346
1,000
Watoto wa kike ni wakupenda sana na kuwajengea Confidence ili wajiamini kama unaweza toka nae out mpeleke sehemu za ghari, Au shopping na sehemu mbalimbali ili azoee mazingira sio leo anakutana na kijamaa kinaenda kumnunulia juice tu Sea cliff basi demu ananza kuona amepata, mfanye rafiki mkubwa na mfanye awe ghari mshirikishe baadhi ya vitu na umpe nafasi ya kufanya decision yani awe part of your advisor na Decision maker ukifanya hayo ña kumpa elimu nzuri hakika ni asset mana ukitoa upendo wa mama basi mtu anaefata kwa kukupenda ni Mwanao au wanao wa kike
 

Ramark

JF-Expert Member
May 19, 2015
1,809
2,000
Mkorinto
Yana uhalisia lkn kiburi ni nini? Je kwa kingereza kinaitwaje? Utakutana na maana ya neno lingine la kiswahili
Hivyo kiburi ni mtazamo wa watu kwa kubeza yaliyocheap kwake na kuonesha msimamo wenye mantiki dhidi ya mnayoamini ninyi mnaomuita ana kiburiSuala hili linakuja otomakiti kwani ni la kisaikolojia kuwa binti rafiki yake ni baba ndiye atakaye mpenda na kumfundisha kuhandle dunia ambayo kwake anaiona ni ngumu kwa uoga alionao naturally tofauti na wa kiume haoni umuhimu huo kwa kuwa hana uoga na anaweza kujitetea isipokuwa wanaficha maovu na siri zao migongano mwa mama zao
Binti anapomuona baba yake anajitengenezea taswira ya mwanaume anayemtaka
Pia wa kiume ataoa mwanamke anayefanana au aliyenasifa za juu kuliko mama yake kama anamapungu lkn vioo ni wazazi

Binti yangu tangu utoto utamuona akikimbilia miguuni kwangu, tukitembea yeye ndiyo anatakwa ashikwe lkn wa kiume hana mpango huku roho ikimuuma baba anampenda dada kumbe dada anamfuata baba kwanza
 

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
11,062
2,000
si kweli lakini kuwa watanyanyaswa na wanaume...kuna wengine wanawake waliopendwa na baba zao na wakabahatika kupata wanaume wanaowapenda kwa dhati,...ukimpata mwanaume aliyeonyeshwa upendo wa mama na pia kuona baba yake akimrespect mama yake wakati wa malezi yake,huwaga wana upendo sana na wake zao…...
 

supermarket

JF-Expert Member
Sep 10, 2016
7,286
2,000
Nature ya mtoto wa kike ni kupendwa, kudekezwa na kumjali na ndio furaha yake.

Ili kumkuza malkia wa nguvu kupambana na vishawishi vya wanaume na hata mapambano vyidi ya dunia na mfumo dume anahitajika apate upendo na ukaribu wa baba.

Japo kuwa mtoto wa kike anahitaji malezi sana ya mama, lakini pia anahitaji sana malezi ya baba, si unajua tena princess kwenye ufalme bora wa King & Queen.

Ukitaka mtoto wa kike aishi kwenye familia yake baadae na mwanaume bora kama baba yake, inabidi pia awe bora kama mama yake.
 

lliedie

JF-Expert Member
Apr 29, 2020
787
1,000
Watoto wa kike ni wakupenda sana na kuwajengea Confidence ili wajiamini kama unaweza toka nae out mpeleke sehemu za ghari, Au shopping na sehemu mbalimbali ili azoee mazingira sio leo anakutana na kijamaa kinaenda kumnunulia juice tu Sea cliff basi demu ananza kuona amepata, mfanye rafiki mkubwa na mfanye awe ghari mshirikishe baadhi ya vitu na umpe nafasi ya kufanya decision yani awe part of your advisor na Decision maker ukifanya hayo ña kumpa elimu nzuri hakika ni asset mana ukitoa upendo wa mama basi mtu anaefata kwa kukupenda ni Mwanao au wanao wa kike
👏👏👏
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom