Kwanini NHIF imeondoa dawa za bei ya juu kwenye Orodha, Watumishi Octoba 28 Mnajambo lenu

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
6,620
2,000
Kitendo cha shirika la BIMA ya Afya NHIF kuondoa dawa zenye bei juu kwenye orodha imenisikitisha sana, tulitegemea sana ule wimbo kuwa NHIF wameboresha huduma basi ingeenda sambamba na kuongeza dawa zinazotolewa.

Haina maana na wala haingii akili kumpatia mtu vipimo halafu suala la dawa linakuwa kizungumkuti, laziama tufike mahali tusema si lazima NHIF ijiendeshe kibiashara lengo ni kutoa nafuu kwa nanchi kupata matibabu hasa wale amabo hawawezi kumudu gharama za matibabu.

Mfano kuna dawa nyingi za wagonjwa wa Cancer zimeondolewa kwenye orodha tunajua dawa hizi ni ghali sana si wengi wanamudu kuzinunua, ukienda pale ocean road utakuta watu wengi wapo pale wanalalmika sana baati mbaya hawana mtu wa kuwasaidia.
 

Msingida

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
7,605
2,000
Lissu ataboresha bima ya Afya itoe huduma nyingi na adhimu.
Ipo kwenye ilani.Kura zote kwake.
 

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
2,544
2,000
Lissu ataboresha bima ya Afya itoe huduma nyingi na adhimu.
Ipo kwenye ilani.Kura zote kwake.
huyu huyu anaye kusanya michango yetu sisi walala hoi, Duh!! kweli watanzania bado tuna uvivu wa kufikiria...umewahi kujiuliza watoto wake wana soma na kutibiwa wapi? ulayaaa!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom