Kwanini neno haki ni gumu sana kutendeka kuliko amani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini neno haki ni gumu sana kutendeka kuliko amani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jethro, Nov 8, 2010.

 1. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Wana JF,

  Huwa nashangazwa sana na kauli nyingi za viongozi kukimbilia kuhubiri neno AMANI esp wakati kama huu uliopita wa uchaguzi.

  Huwa najiuliza kwanini viongozi walioko kwenye madaraka hukimbilia kuhubiri neno AMANI huku fika wanajua hawatendi HAKI, Kwanini wasi hubiri neno HAKI kwanza then AMANI huja haraka kabisa ukisha itenda HAKI kwa rai wako.

  sasa tuchukulie mfano wa mgombea ubunge ( CUF jimbo la Tandahimba Mr. Katani Ahamed Katani) kwa yale yaliyo mkuta Mheshimiwa mbuge huyu aliye nyang'anywa tonge mdomoni na kichapo akakipata toka kwa nguvu za Dola (Police).

  Na sasa anakimbilia mahakamani kwani HAKI hapa inge tendeka AMANI ingevurugika na kumfika yaliyo mpata na kujikuta na POP.

  Hiyo yote ni kuwa HAKI haikutendeka na AMANI ikapotea. sasa siwaelewi hawa viongozi ni kitu gani kinawasibu kuhubiri neno AMANI badara ya kuhubiri HAKI kwanza?

  Karibuni Wana JF kuchangia mada hii mbele yenu
   
 2. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Bila HAKI hakuna AMANI na hata ikiwapo inakuwa siyo halisi kutoka moyoni...huwa ni amani ya WOGA, UKONDOO, UNAFIKI ambayo kwa kawaida huwa sio ya mda mrefu kwani hufika wakati kiwango cha uvumilivu hufikia kikomo na kinachofuata hapo ni BOMU!
   
 3. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #3
  Nov 8, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Wanabomoa amani kisha wanahubiri sasa tukubali matokeo ili kuponya vidonda walivyosababisha.
   
 4. Sanja

  Sanja JF-Expert Member

  #4
  Nov 8, 2010
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 60
  Hawajui/hawakumbuki msemo huu MJUSI UKIUKIMBIZA SANA MWISHO HUGEUKA NYOKA. Siku zote na mahali popote duniani panapotendeka na ikaonekana machoni pa raia hapahitajiki mahubiri ya amani miongoni labda awe mwanasiasa aliyeishiwa hoja. Sisi badala ya kushughurikia suala linarosababisha hiyo haki iwepo tunaihubiri majukwaani kama mazuzu wakati raia wakizurumiwa haki zao huku serikali ikishuhudia hata muda mwingine ikishiriki bila aibu wala kuchukua hatua. UTAJIRI WAKO NDO SHERIA ZAKO
   
 5. sensa

  sensa JF-Expert Member

  #5
  Nov 8, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hakuna Amani bila haki,hivyo hiyo amani inayohubiriwa haipo ni porojo tu za siasa.Haitoshelezi kusema kuna amani kwa vile hakuna vita.
   
 6. Utotole

  Utotole JF-Expert Member

  #6
  Nov 8, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 6,344
  Likes Received: 3,178
  Trophy Points: 280
  Hawa watu hawajui kuwa haki huinua taifa, na amani ni furaha ya wengi. Wanatakiwa wajue kuwa " Amani itakuwepo ikiwa haki itaheshimiwa, haki ya MUNGU ni kweli na mwenye haki hababaishwi!". Suala la amani kuja baada ya haki kutendeka limeandikwa hata katika vitabu vya MUngu (angalau kwa kile kitabu cha MUNGU nitumiacho mimi). Watu hawa wanatulazimisha kuwa wavumilivu pale tunaponyanyaswa na kunyimwa haki zetu huku wakihubiri amani. Wanataka amani ilindwe na anayenyanyaswa huku wao wanaonyanyasa wakichelea kutenda haki. Na sisi tunakubali na kusema "kuliko tupoteze amani yetu bora tuwaachie tu". Matokeo yake tunapoteza haki zetu na uhuru wetu, tunanunua 'amani' feki. Benjamin Franklin alisema: "Those who would give up essential liberty to purchase a little temporary safety deserve neither liberty nor safety"

  Lazima tutafakari!
   
 7. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #7
  Nov 8, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Kuna tabia au utamaduni katika nchi hii umejengwa na viongozi mbali mbali wakiwepo wa dini. Mfano mzuri ni viongozi wa dini wakati haki watu wanadhulumiwa haki zao huwa wako kimya, baada ya watu kudhulumiwa haki zao viongozi hao wa dini hujitokeza kuwasihi watu wasivunje amani. nafikiri ni makosa kutumia neno amani vibaya.
   
 8. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #8
  Nov 8, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Say it again
   
 9. T

  Tanzania Senior Member

  #9
  Nov 8, 2010
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 114
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ndugu yangu, nafikiri unatakiwa kwanza ku define Amani kabla hujaendelea. Nijua mimi amani huanzia moyoni na si vinginevyo. Na hakuna amani bila Haki. Hii tunayoifikiri ni amani ni rubber stamp tu siyo sustainable. Unapoona telaban wanajiripuwa na kuuwa mamia ya watu, shida ni haki. Mioyo ya watanzania imesha jeruhiwa muda wa kutosha kwa kukosa haki zao, kifupi hakuna amani. Ni neema ya Mungu italinda, ikitoweka ni dhiki kubwa sana. Mungu na aendelee kuturehemu na kuirejesha haki ili tuishi kwa amani.
   
Loading...