Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,096
- 35,020
Kufuatia matamshi makali na vijembe vizito vilivyotolewa na Samia dhidi ya Ndugai kiasi cha kuleta sintofahamu na kutafsiriwa kama jambo lenye kufedhehesha na kukidhalilisha kiti cha spika wa bunge, nadhani kuna haja ya Ndugai kutumia yale mamlaka yake ya siku zote aliyonayo kikatiba ili kumtaka mara moja Samia kufika kwenye kamati ya kudumu ya kinga na haki za bunge ili kujieleza na kuchukuliwa hatua stahiki.
Kwa lengo la kulinda heshima na mamlaka ya bunge tukufu, jambo hili linapaswa kufanyika mara moja bila kusubiri. Sheria ni msumeno, kuwa rais sio kikwazo cha kukwepa kuitwa kwenye kamati hiyo. Mimi na watanzania wengine tutashangaa sana kama Ndugai atashindwa kufanya hivyo au atachelewa kufanya hivyo wakati jambo hilo ni genuine na liko ndani ya uwezo wake kikatiba kwa 100%.