Kwanini ndoa zisisajiliwe kwa njia ya Mtandao (Digital)

Lihove2

JF-Expert Member
Mar 23, 2018
3,117
5,584
Niende moja kwa moja kwenye maada

Nilikuwa naangalia jinsi mama, dada, shangazi zetu wanavyotelekezwa na wanaume kuhama miji na kwenda kuoa tena wake wengine. Pia hao wake wengine bila kujua kwamba jamaa ana mke wa ndoa tayari. Mwisho wa siku kutengeneza sintofahamu.

Wazo langu ni kwa nini serikali hasa wizara ya sheria isibuni cheti cha ndoa cha kimtandao.Ambapo mnapooana inabidi kwanza muwe na kitambulisho cha NIDA,halafu mnasajiri ndoa yenu kwa njia ya vidole. Kiasi kama mmoja wenu alishaoa basi pale pale wakati wa usajili ijulikane kwa kuonyesha majina ya mke au mme ambaye tayari yuko naye na tarehe ndoa ilipofungwa.Ili kuendelea na process inabidi iwe digitally approved na mke aliyoko kwenye ndoa

Najua kuna ndoa za wake wengi,basi wakati wa usajili paonyeshe wazi jamaa tayari ana ndoa gani,na hao wanawake wakubali kwa kuaprove jamaa kuongeza mke.Pia iwe inawezekana mke au mme kila wakati kuperuzi ile profile ya mwenzake kuona idadi ya wake walioolewa na mme wake.

Pia iongeze kidogo gharama za kulipia hiyo huduma hasa hiyo ya kuperuzi profile ya hali ya ndoa kwa mwenzako.njia iwe ile ile ya control namba.

Najua kuna wale wenzetu wanao oaga leo kesho taraka.mahakama ndiyo iwe na uwezo wa kusajili taraka kwenye mtandao,lakini isiondoe majina ya watalikiwa, yabaki humo humo ili anayeingia kwenye hiyo ndoa ajue wameshaachwa wangapi na huyo jamaa.pili gharama ya kusajili taraka iwe kubwa kuliko ile ya kusajili ndoa.

Nadhani tutapunguza kwa kiasi fulani udanganyifu kwenye ndoa.

Nasema uongo ndugu zangu?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom