Kwanini ndoa za kizazi hiki zinabagua ndugu?

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Dondoo za kuzingatia katika mjadala:-

1. Ndoa nyingi zimeacha kufanyika baraka kwa ndugu (Charity that does not begin at home).

2. Ndugu za mwanamke akiishi katika ndoa anatoboa kimaisha kuliko ndugu wa mwanaume.

3. Mwanaume akifa jibu ni moja tu kwamba ameuawa na mwanamke, mwanamke akifa hajauawa na mwanaume kafa kwa kifo chake mwenyewe.

4. Semina nyingi za kufundisha ndoa mfumo wake ufumuliwe, usukwe upya. Haiwezekani uwafundishe watu wanaoenda kuishi kwa shida na raha hadi kifo kiwatenganishe; maisha ya ndoa kwa vipindi (lessons) 3-4 kwa mwezi mmoja tu alafu uwaambie mmefuzu chukuweni vyeti mkaishi.

5. Kuachana na nafasi ya Jando na Unyago (ambayo ilichukuwa kipindi kifupi cha miezi 6 na kirefu cha mwaka 1) kunaweza kuwa sababu ya dhoruba za ndoa za kizazi hiki?

6. Kwanini Mirathi inaamuliwa anapokufa mume tu lakini akifa mke hakuna habari ya Mirathi? Watu wa Gender na Feminists mnasemaje huu utaratibu huu ni mzuri? Mume hata kama siyo mtafutaji wa mali za familia lakini akifa tu Mirathi lazima iamuliwe, lakini mke hata kama ndiye aliyetafuta mali za familia siku akifa kabla ya mume hakuna Mirathi kuamuliwa!
Patrilineality.
Baghosha!
 
Usiingilie maisha ya watu, huo ni umbea unachunguza chunguza ndoa watu kwani yakwako imekunyookea?
 
Back
Top Bottom