Kwanini ndoa nyingi za watu waliopishana miaka michache (rika moja) huwa zinadumu muda mrefu na kuwa na changamoto ndogo ndogo sana?

Kosa lilifanyika ile nyakati ambapo mtoto wa kike aliachwa ajiamulie kuishi anavyojisikia. Mkutano wa Beijing ndio ulileta yote haya. Kimsingi mungu amemuumba mwanamke na roho ya uvumilivu wa hali ya juu na utiifu dhidi ya mamlaka.

Mamlaka kuu ya mtoto wa kike ni mwanaume, anzia chief, babu, baba mpaka mume! Hii ni hierachy ya mamlaka iliokuwepo tangu enzi na ililenga kutengeneza jamii yenye nidhamu na sio oppression kama ambavyo ilitafsiriwa.

Ofcourse hamna mfumo usio na faults ila huu mfumo ulionesha ku work efficently kwa asilimia kubwa sana kwa ku enforce wanawake kuwa submissive. Malalamiko yalikuwepo kwa wanaume waliokuwa wanazingua ila kulikuwa na namna ya kuya address.

Sasa baada ya kuja mambo ya gender balance ndio ikapelekea zile mila kutafsiriwa kama mfumo dume. Kwamba mke anatakiwa apewe nafasi ya kujiamulia atakalo na kuwa self reliable badala ya kuwa submissive kwa mwanaume. Hii ikiwa ni sehemu ya ku exercise haki zake za kijinsia kama ilivyo kwa mume.

Ndipo mwanamke akapewa mamlaka ya kushika madaraka na uchumi...The worst mistake to ever be done in this world. Mwanamke anachokifanya since then ni kushindana na mwanaume ikiwezekana kumu oppress kabisa akipata nafasi hio saa nyingine hata kwa kutumia sheria zile zile kwamba anaonewa ilihali yeye ndie anamkomoa mume.

Hii sumu imesambaa kwa vizazi kadhaa toka ilipoidhinishwa ila mpaka kufikia leo hii matokeo tunayaona. Ndoa zimekuwa hazidumu sababu mwanamke haoni sababu ya kuwa mvumilivu kusuluhisha migogoro ilio sehemu ya maisha katika ndoa. Sababu yuko free kujiamulia lolote atakalo ni ngumu kutii mamlaka ya mume endapo haoni ndoa ina favour matakwa yake. Especially kuishi maisha kama yuko single, achepuke anavyotaka afanye anayojiskia hata kama yanakarahisha na kukuondolea amani mumewe.

Kubwa kabisa, mwanamke kumiliki madaraka na uchumi. Hapo ndio balaa kabisa. Wote tunaenda kazini sasa kwanini anibabaishe. Hii ndio akili walionayo watoto wa kike 70% ambao baadhi wameolewa na wengine wanatarajia kuolewa. Ukimwambia basi acha kazi uhudumie familia pia ni ugomvi mkubwa unaambiwa kwani baba yangu alinisomesha ili iweje? Ndoa haiwezi kudumu pasipo na nidhamu na nidhamu ili iwepo lazma kuwe na mamlaka iliosimama ambayo ni mwanamume...Guess what?

Tafsiri ya mamlaka imegeuzwa tena na utandawazi kuwa sio mwanaume per se ila ni mwanaume mwenye hela!!! Kwa hali iliopo sasa mwanaume mwenye uwezo wa ku satisfy fantasies za mwanamke zaidi ndie mtu pekee ambaye wanamtafsiri kama anayestahili heshima. Wonders never cease!!!

Ndio maana kila baada ya kisa cha mahusiano kinachokuja jf moja ya suluhu utaskia "Tafuta hela mkuu!"
Huu mfumo wa "Beijing" umeleta madhara makubwa sana katika jamii yetu.

Hakika wazee wetu walikuwa na maono ya mbali sana ndio maana maisha yalikuwa yanaenda na hata waliweza kuwa na wake zaidi ya wawili lakini hakukuwa na shida kabisa. Leo mwanamke mmoja tu pasua kichwa ni kwa vipi utaweza kuwa nao wawili!?
 
Mwenzenu hata sifikiriahi mambo ya umri kwenye hiz habari
Ni vigezo na msharti tu ndio vinazingatiwa
 
Ngoja nikupe formula......
Screenshot_20180212-011319.jpeg
 
Ndoa nyingi za watu waliopishana miaka michache (rika moja) huwa zinakuwa na changamoto ndogo ndogo sana.
Mbona umeongea kinyume chake mkuu. Hivi unajua akili za wanawake?!

Mwanamke wa miaka 18 anawaza kuwa na mwanaume mwenye gari, na kazi na vitu vya thamani. Katika umri huo huo mtoto wa kiume anajifunza kunyoa kiduku na kugonga mademu hana hata moja analowaza juu ya maisha.
 
Mwanamke wa miaka 18 anawaza kuwa na mwanaume mwenye gari, na kazi na vitu vya thamani. Katika umri huo huo mtoto wa kiume anajifunza kunyoa kiduku na kugonga mademu hana hata moja analowaza juu ya maisha.
Mkuu, mimi ninaongelea watu walio katika umri wa kuingia katika ndoa na sio hawa vijana wa miaka 18 ambao bado ni kula kulala
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Kwanini ndoa nyingi za watu waliopishana miaka michache (rika moja) huwa zinadumu muda mrefu na kuwa na changamoto ndogo ndogo sana?

Nimeamua kuuliza hivi kwa maana kwamba, hakuna ndoa inayokosa changamoto za hapa na pale, lakini hizi za watu waliopishana miaka michache (mwaka 1, miaka 2 au wanalingana umri), unakuwa wote mke na mume walizaliwa mwaka 1985 ila wametofautiana miezi tu, huwa nimeshirikishwa sana hususan classmates zangu waliokutana chuoni, waliosoma wote O level pamoja na A level lakini masuala yao yanatatulika kwa urahisi sana.

Na huu utafiti wangu sio kwa wanachuo wenzangu tu, bali mpaka kwa watu walionizidi umri ambao wana miaka mpaka 20 katika ndoa zao.

NB: Kamwe siwezi kueleza visa vya ndoa za watu humu kwa maana sio uungwana wala ustaarabu watu wakuamini na kukushirikisha katika masuala yao mazito kisha ukaja ukawaandika mitandaoni, hakika sio hekima hata kidogo.

Maoni ya Wadau;

=========





USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Ndoa nzuri ni ile ambayo gap la umri ni kubwa,hasa ile ambayo mwanamke kamzidi umri mwanaume,mfano mimi nimuoe Dr.Tulia Akson,ndoa itadumu sana hii
 
Back
Top Bottom