Kwanini ndoa nyingi za watu waliopishana miaka michache (rika moja) huwa zinadumu muda mrefu na kuwa na changamoto ndogo ndogo sana?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
8,376
2,000
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Kwanini ndoa nyingi za watu waliopishana miaka michache (rika moja) huwa zinadumu muda mrefu na kuwa na changamoto ndogo ndogo sana?

Nimeamua kuuliza hivi kwa maana kwamba, hakuna ndoa inayokosa changamoto za hapa na pale, lakini hizi za watu waliopishana miaka michache (mwaka 1, miaka 2 au wanalingana umri), unakuwa wote mke na mume walizaliwa mwaka 1985 ila wametofautiana miezi tu, huwa nimeshirikishwa sana hususan classmates zangu waliokutana chuoni, waliosoma wote O level pamoja na A level lakini masuala yao yanatatulika kwa urahisi sana.

Na huu utafiti wangu sio kwa wanachuo wenzangu tu, bali mpaka kwa watu walionizidi umri ambao wana miaka mpaka 20 katika ndoa zao.

NB: Kamwe siwezi kueleza visa vya ndoa za watu humu kwa maana sio uungwana wala ustaarabu watu wakuamini na kukushirikisha katika masuala yao mazito kisha ukaja ukawaandika mitandaoni, hakika sio hekima hata kidogo.

Maoni ya Wadau;

=========

watu waliopishana umri kidogo wanadumu kwa sababu moja wanaendana kimitindo mwenendo na tabia yaan kwa mfano mtu wa 2000 amuoe mtu wa 2003 hawa wanaeza ishi vizur coz kila anachokifanya mwenzako sio kigeni kwako mfano mtindo wa mavazi na maisha mengine kama kutoka out mnajikuta wote ni waumimini wa hvo vitu hakuna atakaepata shida kuishi na mwenzie

Gap kubwa la miaka katika ndoa huwa linaondoa umuruwa, na hatushauriwi kuoana kwa wana ndoa kupishana miaka mingi sababu madhara yake ni makubwa kuliko manufaa.

Yale mengine ya kuimarisha ndoa hubakia kama yalivyo.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 

walitola

JF-Expert Member
Nov 28, 2014
3,899
2,000
Sio kwa wanachuo wenzangu tu mkuu, bali mpaka kwa watu walionizidi umri ambao wana miaka 20 katika ndoa.
Kikubwa ni kuheshimiana mkuu nafikiri kila mtu akitimiza wajibu wake ndoa itakuwa salama japo kupishana kauli hakuepukiki but vijana wengi wa sasa wanakitu inaitwa kujiamini sana sana kwa hawa dada zetu kigezo kuwa wamesoma jambo ambalo upulekea kuto kutambua wajibu wao kwenye ndoa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom