Kwanini ndoa huwa zinaua ndoto zenu za maisha?

Liverpool VPN

JF-Expert Member
Aug 29, 2020
5,767
12,982
Wajumbe Wazima?

Ni yuleyule Mr. Liverpool from Anfield.

Baada ya salamu hebu twende direct kwenye mada.

Kwanini mkishaoa huwa ndoto zenu zina kufa?

Scenario 01:-
Walimu wa2 from Songwe. Hawa jamaa nilikutana nao 2012 Tunduma, tukawa marafiki. Kwenye maongezi yetu nikagundua waliajiriwa 2011 wakiwa na certificate.

Waliniambia 2012 lazima warudi Shule kusoma ili waitafute Bachelor. Muda ukaenda na tukapotezana. Nilikuja kuwaona 2018 wakiwa na mke na ile ile certificate na Chuo walishindwa kurudi baada ya kuoa. Ila dip down wanatamani sanaa Shule.

Scenario 02:-
Bwana mifugo wa2 from Morogoro. Kuna kipindi nilishawahi ishi Morogoro ndani ndani hukohuko kwenye kulima mpunga. Nikakutana na hawa jamaa.

Kipindi hicho nafikiria kurudi chuo. Kwa story za kipindi tofauti waliniambia na wao lazima warudi kuongeza elimu ili kazini mambo yapande. 2019 nikiwa na MSc. nilienda tena Moro kulima mpunga nikapokewa na mmoja wao.

Alinipa hongera ya kurudi Shule akaniambia "ungeoa na wewe ungekuwa kama mimi (kushindwa kurudi shule)"". Ila ukimsikiliza vizuri ni kama mtu anayejutia kutorudi shule. Na wa pili nae kaoa zile ndoto zake zikafa.

Scenario 03.
Binamu yangu. Form six 2008, akiwa mtoto wa nje ya ndoa ya baba ake, mama wa ndoa ya baba ake aligoma mumewe asimsomeshe bro Bachelor.

Bro akiwa ni mtoto wa nje ya ndoa ya baba ake alitamani sanaa kusoma Law. Alifanya applications zote akapata chuo Tumaini. Kupeleka join instruction kwa baba ake, mama wa ndoa ya baba ake akaweka zuio. Basi bana ndugu wakamtia moyo akatafutiwa chuo cha Dip ya ualimu.

Kasoma, kamaliza na kuajiriwa mwalimu DSM. Siku anaenda kwenye ajira aliniambia "mdogo wangu siwezi acha ndoto zangu za kusimama mbele ya mahakama kufa, lazima nirudi Tumaini kusoma law. Sasa hivi si Nina ajira basi nitajisomesha tu"

Akaingia kazini na kuoa. Leo hii 2021 ana ile ile Diploma of Education. Baada ya kuoa ndoa zake chaliiiiiiiii

Scenario 04:-
Bwanashamba Mbeya. Nilikutana nae 2014. Akiwa na Diploma of Gen. Agr. Kwenye story aliniambia "nataka niwe Bwana Shamba wa wilaya, lazima nirudi chuo nitafute Bachelor" Nimekutana nae wiki iliyopita mjini huko akiwa na Diploma yake + Kaoa.

Scenario 05.
Mtoto wa mama mdogo. Huyu alivyosikia naenda Masters aliniambia "Hongera mdogo angu umenipa motisha na Mimi nakuja"

Nimeenda Shule, nikamaliza, nishasahau kama nilishawahi enda Shule ila yeye yupo tu certificate yake na kasahau kabisaa zile ndoto zake.

Scenario 06.
Marafiki niliomaliza nao Bachelor. Tulikua na plan za kusoma MSc. Ila baada ya kuoa wotee chaliiiiiiiii. Tuliosoma ni wawili tu ambao tupo single.

Scenario 07.
Work mate. Nilivyo hamishiwa ofisi yao na kuwa mkuu wa kitengo Chao aliitamani sanaa elimu yangu. Kuja kuuliza naambiwa huyo kelele zake za kurudi Shule ni tokea 2017 ila Kashindwa kurudi. Kuchunguza naambiwa pia alio 2017.

Scenario 08.
Mtoto wa baba mkubwa. Tulivyomaliza form 4 alienda certificate nikaenda Advance. Alivyomaliza cert yake akaoa. Wajumbe zile ndoto za kuwa PROFFESIONAL fulani zilikufa na Shule iliishia hapo.

Scenario 09.
Ni wengi sanaa nawaona aisee, Baada ya kuoa zile "Dream Chasing Rasing" nazo ziliishiwa mafuta zikafa..!!!

1. Kwanini mnaruhusu hao wake zenu ambao mlikutana tu ukubwani kuua ndoto zetu ?

2. Kwani ni lazima kuoa ili kuua ndoto zenu?

Ewe kijana wa kiume ACHA KUOA.

UKIOA NDOTO zako zotee nazo UNAZIKA.

Tuendelee kutafuta hela ili tuzifukuzie ndoto zetu za maisha.

Ndoa NGUMU
Ndoa NDOANO
Ndoa KIFURUSHI CHA SHIDA

"If you think money can't buy your happiness then go and ask the homeless and Jobless"

#YNWA
 
Mmh..! Hebu fanya utafiti kwanza maana mimi wakati naanza kazi nilianza na cert. na pengine wazo la kujiendeleza halikuwepo lakini nilienda kukutana na watu wawili ambao ndiyo walikuwa viongozi wangu.sitawasahau kwa ushauri wao mzuri ambao mpaka leo umenipa mafanikio na kunivusha mpaka hapa nilipo sasa

Walioa mara baada tu ya kuingia kazini baadae ndipo wakajiendeleza na mimi nilipofika walinishauri hivyo hivyo nioe ila nisisahau kwenda kusoma na kweli nilifanya hivyo ingawa nilihisi ugumu na changamoto lakini nilipambana mwishowe nikafanikiwa

Kikubwa ni malengo na kuweka dhamira ya dhati.
 
Familia nyingi za Kitanzana ni duni. Ukipata ajira ndugu na wazazi kama wapo watakutegemea. Ukioa mke, wazazi wa mke na ndugu zake nao watakutegemea japo siyo kwa 100%. Kinachofuata ni wewe kuzika ndoto zako za kiuchumi na kielimu. A bitter truth 😅
 
Wanaotafuta usahihi ni wao.
Kinsingi ndoa haijawai kukamilika, na kikubwa ni kuvumilina kwasababu sisi sote si wakamilifu.
Wasio wakamilifu 2 wanapoamua kuishi pamoja wanazaa shida/taabu.

Asiye mkamilifu+ asiye amkamilifu= shida/taabu
 
Familia nyingi za Kitanzana ni duni. Ukipata ajira ndugu na wazazi kama wapo watakutegemea. Ukioa mke, wazazi wa mke na ndugu zake nao watakutegemea japo siyo kwa 100%. Kinachofuata ni wewe kuzika ndoto zako za kiuchumi na kielimu. A bitter truth
Hili Jambo linanitatiza mnoo
 
Back
Top Bottom