Kwanini ndege za kivita zina kasi kuliko za abiria?

lukelo sakafu

JF-Expert Member
Feb 19, 2015
2,939
517
jamani hivi kwa nini za kivita zinakimbia sana kuliko ndege za abiria?

je ni kweli kuwa ndege za kivita ndio zina uwezo wa kubeba mizigo mizito zaidi kwa sababu mabomu na makombora mazito zaidi na yenye tani kibao kama ma nyuklia, scud.

je ni kweli chopa za kivita ndio zenye nguvu zaidi kuliko machopa mengine yote na ukimbia zaidi. halafu ni kweli kuwa ndege za kawaida hazina kasi kama za kivita?

pia kuna tetesi kwamba ndege ya kivita zina uwezo wa kutembea fasta kutoka bongo mpaka marekani kwa muda mfupi tu. wenye utaalamu na mambo ya vita watujuze hapa
 
NDEGE ya kivita kama F-16,f-35,mig zina limit ya umbali hauzidi km 2000,Kwahiyo haziwezi toka mfano marekani hadi irag ,ndo maana zinabebwa katika yale mameli kuzisogeza karibu na uwanja wa vita.

ndege long range bomba kama B-52,B-1,ama T-160 ndo inaweza toka marekan mpaka irag bila kutua sehemu.
mpaka sasa ndege ya mrusi T-160 blackjack ndo ndege kubwa kuliko zote za kivita na inayoweza kubeba payload kubwa.
na pia inaspeed kubwa.

ndege inayobeba mzigo mkubwa,kwamaana ya ndege ya mizigo ni Antonov An-225 ya Ukraine.
 
Ni kweli inaweza kwenda 1000KM\H normal speed. ndege yenyewe ina tani 3-5 lakini mzigo inabeba tani 7-12 mabomu.
 
Sidhani kama ni kweli ndege za kivita zinakimbia kuliko zote, sema zina acceleration (thrust) kubwa kutokana na kwamba zina umbo jepesi, ambalo liko stream lined zaidi na vile vile zina engine kubwa ukilinganisha na umbile lake yani ni sawa sawa na starlet uifunge engine ya vogue! Ndege za kawaida ni nzito na huchukua mda mrefu zaidi mpaka ziweze kuchangaya. Pia huku karibu na ardhini (low attitude) kuna high wind resistance hivyo haziwezi kukimbia sana. Ni mpaka zifike kilometa kumi kutoka usawa wa bahari ambapo kuna poor wind resistance ndio zinafika kati ya speed 800km/hr hadi kwenye 1050Km/hr, speed ambayo ni kubwa ajabu. Ndege zilizowahi kuongoza kwa speed zinaitwa Concord ambazo zilikuwa zinafika nafikiri ni karibu na km 2000 kwa saa!
 
ni kweli ndege vita zinakasi zaidi kuliko ndege za abiria...zinatakiwa kuwa na kasi kukabiliana na makombora yenye kasi kwa adui
 
Mwenyewe ushaiita vita na vita unajua kuwa ni hatari, nadhan hata vifaa vitumikavyo nivya hatari pandezote
 
Technologia zote advanced huanzia majeshini (military). Wakigundua technologia zaidi ile iliyopitwa na wakati ndio hutolewa kwa matumizi ya kiraia. Kwa maana hiyo ndege za kivita kweli zina speed kubwa kuliko za kiraia. Zingine hazina rubani (drones). Pia hata simu za mkononi zilianzia jeshini, mgari yenye uwezo wa juu yako jeshini, silaha za uwezo wa juu hupewi raia, komputer high speed wanao wao japokuwa kuna mgunduzi wa internet nasikia ndio yake ya kwanza.
 
Zipo ndege za abiria zina speed sana, kumbaka supersonic zilikuwa zina speed kuliko sauti.
 
Akijibiwa atakuja na swali jingine.....Kam a lifuaavyo:
Kwanini kifaru cha kivita kina speed ndogo??????????
 
Mimi si mtaalamu wa mambo ya kijeshi lakini nina upenzi na ninafuatilia teknolojia za namna hii. Hivyo nitaongea kwa uzoefu wa mfuatiliaji tu.

Ni kweli kuwa ndege zenye kasi zaidi ni za kijeshi ila si ndege zote za kijeshi zina kasi kubwa kupindukia. Ndege za kijeshi zina makundi kadhaa na kimsingi ni haya:


  1. Fighter Jets: Hizi ndizo zenye kasi zaidi kwa sababu ya matumizi yake kama nitakavyojadili chini. Zina uwezo mkubwa wa kushambulia na kujilinda zenyewe.
  2. Bombers: Hizi hubeba mzigo zaidi (mabomu mazito zaidi) kuliko Fighters na aghalabu huwa na kasi ndogo kuliko Fighters. Zina uwezo mdogo wa kujilinda.
  3. Cargo carriers: Hizi ni za mizigo. Hubeba vifaa kama chakula, silaha, mavazi nk toka sehemu moja ama nyingine lakini hazishiriki katika uwanja wa mapambano. Hazitegemewi kuwa na uwezo wowote/mkubwa wa kujilinda.

FIGHTER JETS

Kama nilivyokwishasema awali hizi ndizo zenye kasi zaidi. Ndizo hutumika kujibu mashambulizi ya dharura dhidi ya adui kwa sababu zinatumia muda mfupi kufika eneo alipo adui. Pia ni salama zaidi kwa kuwa zinashambulia na kutoka eneo la adui haraka iwezekanavyo. Adui mkubwa wa ndege hizi ni makombora ya kutoka Ardhini kwenda Angani kwa kiingereza Surface to Air Missiles (SAMs). Ili kombora la SAM liitungue ndege hii ni lazima liwe na kasi kuliko ndege.. hivyo ndege ikiwa na kasi kuliko kombora haitotunguliwa ikiwa itafanya juhudi za kukimbia. Kwa kawaida makombora yana kasi sana na bidii hufanyika kila uchao kuyaboresha tegemeana na ndege zinavyoboreshwa pia.

TEKNOLOJIA/SUPERSONIC/SUPERCRUISE
Ndege zinazoweza kwenda kasi zaidi kuliko sauti huitwa Supersonic Aircraft.. fighters nyingi za kisasa ni supersonic. Kimsingi supersonic aircrafts hutumia injini ya jeti (si ya pangaboi/propeller la nje) na ndege hizi husaidiwa kufika kasi kuliko sauti kwa kurudia kuichoma gesi kwenye injini kwa kutumia After-Burners. Ndege zinazoweza kubeba silaha na zikaenda kwa kasi ya sauti bila msaada wa After-Burners hutajwa kama Supercruise.. Fighters za kisasa zaidi ni supercruise (angalau baadhi).

REKODI YA LOCKHEED SR-71 BLACKBIRD (Viwanja 10 vya soka kwa sekunde moja!!)
Pamoja na kuwa kuna takwimu zinazokinzana lakini ndege inayotajwa bila shaka kuweka rekodi ya kasi zaidi ni Lockheed SR-71 Blackbird iliyokimbia kwa kasi ya kipimo cha Mach 3.3 ama 3,529.6 km/saa hii ni sawa na kasi mara tatu ya sauti! ama karibu na urefu wa viwanja 10 vya mpira wa miguu kwa sekunde moja!!

CONCORDE/TUPOLEV TU-144
Ndege maarufu kabisa ya abiria ambayo ni supersonic ilikuwa ni Concorde. Iliweka rekodi ya kasi ya Mach 2.04 (Mara mbili ya sauti). Ilitengenezwa kwa ushirikiano wa Uingereza na Ufaransa. Imepumzishwa baada ya kufanya kazi miaka 27. nyingine ni Tupolev Tu-144 ya Urusi ambayo ndiyo ya kwanza kuwa supersonic kwa abiria ila haikufanya kazi muda mrefu wa la haikuwa maarufu kama Concorde.

GHARAMA
Ni gharama sana kuiendesha ndege ambayo ni supersonic maana mafuta pia yanatumika sana pamoja na kero ya sauti kubwa hivyo kibiashara hailipi sana. Hii ni mojawapo ya sababu Concorde ilipumzishwa. Hailipi. Ila kijeshi gharama inaweza ikavumiliwa kwa kuwa ndege hizi zinaweza kuiokoa nchi isiangamie ama ikasaidia kufupisha vita kwa kumpa adui kichapo haraka.

MWISHO
Burudika na rubani wa Fighter Jet iliyotengenezwa Sweden, Saab Gripen NG JAS 39. Ndege inakimbi kama kombora wakati mwingine juu-chini. Video ya chini ni makombora ya SAMs ya Urusi S-400. Enjoy!!





 
Last edited by a moderator:
Lukelo hili swali la akili umelitoa wapi? Au umeulizwa na watoto wadadisi? Nimeshangaa sana, maana hili lipo juu ya uwezo wako wa kufikiri.

Tehehe. ...na wewe kweli umefikiria
"Utani wa kupendeza lakini...."
 
Back
Top Bottom