Besta Mlagila
Senior Member
- May 29, 2018
- 101
- 191
Tangu kuingia kwa Virusi vya Corona wataalamu wa Afya wamepambana kutafuta dawa na chanjo kukabiliana na gonjwa hili hatari bila mafanikio.
Hivi karibuni ziligundulika chanjo mbalimbali ikiwemo ASTRAZENECA ambayo ilipitishwa na Shirika la Afya Duniani kuanza kutumika kwa binadamu ili kupunguza na kuzuia vifo vilivyokuwa vikiendelea kutokea.
Katika siku za karibuni Nchi mbalimbali zimezuia matumizi ya CHANJO hiyo kwa madai kuwa ina madhara yanayoweza kupelekea kifo ambapo baadhi ya Nchi zimeripoti vifo vya watu vilivyojitokeza baada ya wao kupata CHANJO, japokuwa hawakuhusisha moja kwa moja vifo hivyo ni Chanjo ya AstraZeneca.
Kati ya Nchi zilizopiga marufuku matumizi ya CHANJO ya AstraZeneca ni Indonesia, Congo DRC, Norway, Denmark, Iceland, Bulgaria, Ireland, the Netherlands, France, Italy, Germany, Austria, Venezuela.
Sisi ambao bado Serikali yetu haijaamua kutumia CHANJO yoyote tunapaswa kujifunza nini?