Kwanini nayaunga mkono mabadiliko nje ya CCM

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,602
5,569
Wanajamvi, hebu tutazame mfano huu (kwa umakini)

Kidimbwi cha maji kinakuwepo, mbu anataga mayai yake humo, yanakuwa viluwiluwi mpaka wanaanza kuota mabawa, wanakuwa mbu kamili, wanaruka... Wanatuuma njiani, kwenye magari, sebuleni, chumbani, na kwingine kokote wanakotupatia nafasi!! Mwisho wa siku tunaletewa neti ati mbu asituume??????

Na watu walewale wenye kidimbwi kilekile na bado wanatuambia wao ndio wanaofaa!!!!

Kwangu mimi kwa mfano huo wa mbu. Ccm hawana jipya wala hawawezi kuja na jipya wataendelea kufuga mbu na tutaugua maralia (mfumo ovyo, sera zisizotekelezeka, umaskini na huduma mbovu za jamii) mpaka tukome kama wanavyosema wenyewe

Mwenye macho aone na mwenye masikio na asikie.

Mwisho: Binafsi nikimuona mtu anaeikimbia nyumba aliyoishiriki kujenga msingi na kufanya juhudi za kuibomoa kwa sababu aidha kuna mgeni ana kisasi nae au ni kukumbwa na tamaa mbaya ama kujiona yu mwenye haki kuliko alioshirikiana nao kama si ushawishi mbaya toka kwa marafiki wabaya.

Mzee mmoja alipata kuniambia jihadhari na mtu aliyewahi kupata ajali ya kichwa.


 
Sawa mkuu
Wanajamvi, hebu tutazame mfano huu (kwa umakini)
KIDIMBWI CHA MAJI KINAKUWEPO, MBU ANATAGA MAYAI YAKE HUMO, YANAKUWA VILUWILUWI MPAKA WANAANZA KUOTA MABAWA, WANAKUWA MBU KAMILI, WANARUKA... WANATUUMA NJIANI, KWENYE MAGARI, SEBULENI, CHUMBANI, NA KWINGINE KOKOTE WANAKOTUPATIA NAFASI!! MWISHO WA SIKU TUNALETEWA NETI ATI MBU ASITUUME?????? NA WATU WALEWALE WENYE KIDIMBWI KILEKILE NA BADO WANATUAMBIA WAO NDIO WANAOFAA!!!!

Kwangu mimi kwa mfano huo wa mbu. CCM hawana jipya wala hawawezi kuja na jipya wataendelea kufuga mbu na tutaugua maralia (mfumo ovyo, sera zisizotekelezeka, umaskini na huduma mbovu za jamii) mpaka TUKOME kama wanavyosema wenyewe

MWENYE MACHO AONE NA MWENYE MASIKIO NA ASIKIE.

MWISHO: Binafsi nikimuona mtu anaeikimbia nyumba aliyoishiriki kujenga msingi na kufanya juhudi za kuibomoa kwa sababu aidha kuna mgeni ana kisasi nae au ni kukumbwa na tamaa mbaya ama kujiona yu mwenye haki kuliko alioshirikiana nao kama si ushawishi mbaya toka kwa marafiki WABAYA...
Mzee mmoja alipata kuniambia JIHADHARI NA MTU ALIYEWAHI KUPATA AJALI YA KICHWA.
 
Mfano huo ni sawa kabisa na ule maarufu wa kuweka dereva mpya kwenye gari bovu halafu utegemee hilo gari kufanya kazi vizuri eti kwa kuwa umebadilisha dereva!
 
Mfano huo ni sawa kabisa na ule maarufu wa kuweka dereva mpya kwenye gari bovu halafu utegemee hilo gari kufanya kazi vizuri eti kwa kuwa umebadilisha dereva!

Tunaaminishwa na wanataka tuamini kuwa mchana ndio usiku na usiku tuuite mchana.
 
Umenena vyema mkuu, acha tuyamalize mazalia ya mbu ili mbu wabaki historia...kura yangu ni ya mabadiliko, over.
 
Umenena vyema mkuu, acha tuyamalize mazalia ya mbu ili mbu wabaki historia...kura yangu ni ya mabadiliko, over.
Mbu sasa wameota pembe si mbu wale wa kwenye kidimbwi! Sasa ni mbu wa milimani hawatishwi na upepo wala baridi! Mbu wenye meno wanauma pasi simile bila kujali watoto wala wazee!!!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom