Kwanini nasema na kutetea kwamba Taasisi tunayoihisi haihusiani na Vifo pamoja na Ukatili unaoendelea nchini?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,548
108,860
Nitakuwa wa mwisho kabisa kuamini kwamba eti haya mauaji yote yanayotokea na ukatili wote tunaoushuhudia kwa sasa nchini Tanzania unatekelezwa / unaratibiwa na ' Taasisi ' fulani kutokana na sababu zangu kadhaa ambazo nimezipata baada ya kufanya ' Kautafiti ' kadogo kutoka katika ' Taasisi ' zingine huko duniani.

Kamwe ' Taasisi ' haiwezi kumuondoa / kumuua Mtu kwa mapanga au risasi za hovyo hovyo bali nijuavyo ' Taasisi ' hutumia njia nyepesi tu na ' murua ' kama ikihitaji kumuondoa Mtu ambaye labda wanadhani ni ' tishio ' kwa ustawi wa Taifa husika.

Nimegundua ya kwamba kuna uwezekano mkubwa sana haya mauaji, ukatili na mambo yote ya ajabu yanafanywa na Watu kwa ' interests ' zao ila kwa kutumia mgongo wa ' Taasisi ' ambayo kwa sasa inaonekana ni adui na wale wanaotaka mabadiliko nchini.

Hivi kwa mfano ukishajua kuwa GENTAMYCINE ni mpenda ' Mbunye ' au ana udhaifu mkubwa wa ' Mbunye ' halafu hapo hapo labda ' Taasisi ' inataka kummaliza hivi kuna haja ya wao ( Taasisi ) kupoteza muda kunitumia Watu na Mapanga au Risasi 38 waje wanimalize wakati ipo njia rahisi tu ya Wao kunisakizia Demu mwenye Dally Kimoko / UKIMWI kisha akaniambukiza na nikawa nakufa taratibu tu?

Kuna siku tunaoilaumu ' Taasisi ' tutaumbuka baada ya ukweli kujulikana na ni vyema Sisi sote ambao kutwa tunailaumu ' Taasisi ' na kuihusisha na haya yanayoendelea tukatubu kwa Mwenyezi Mungu kwani nina uhakika kabisa kwamba 100% hawahusiki isipokuwa tu tunawaangushia Jumba Bovu.

Nawasilisha.
 
Kwa muktadha huo ulioeleza basi Na ionekane wazi kwamba mkuu mwenye mamlaka na taasis hiyo akikemea 38 ,kutekwa,mauaji na wasiojulikana nk..akikaa kimya ni maon yangu kwamba ndipo wasiwas na taharuki inazunga kwa watu wake anaowaongoza
 
Chief Genta,

Kuhusishwa kwa taasisi kupo kwa aina mbili. Moja nimojawapo ya taasisi yenye nguvu ya kujua nani anafanya nini au anataka kufanya nini. Hivyo wanauwezo na nyenzo ua kuzuia uhalifu usitokee.

Pia tunatambua sio kila uhalifu unaweza kuzuilika lakini pale unapojitokeza kwa style ile ile kwa kundi fulani la watu unapata shaka. Human thonking lazima itakuambia wanahusika kwa maana wanawajua na wamekaa kimya.

Namna ya pili inawezekana ndani ya taasisi hiyo kuna kikundi kidogo chenye weledi wa mambo kimeamua kutekeleza uhalifu nahawajulikani. Kwa sababu maisha yetu na usalama wetu teweka mikononi mwao na hatuoni jitihada za makusudi kutokomeza uovu huo, again ubinadamu unatuambia wanahusika.

Pale uhalifu unapomlenga mtu mkubwa wa upande ule hatua za haraka huchukuliwa na tunaona wahusika wanakamatwa. Kulikoni wakifa upande wa wanyonge?

Double standards kwenye mambo ndio kigezo kikuu kusema taasisi ile inahusika.
 
Duhhh hili nalo neno

Amini maneno yangu Mkuu hiyo ' Taasisi ' tunaisingizia na kuionea mno na hivi huwa haina tabia ya kupenda Kuropoka / Kuzoza basi ndiyo inasukumiziwa kila aina ya dhambi / ubaya. Ninavyojua kutokana na Mafunzo yao tena ya Kimataifa kabisa kutoka nchi mbalimbali zilizotukuka ' Kitaasisi ' ni kwamba siku zote ' Njagu / Jasusi ' aliyeiva kabisa huwa hamdhuru Mtu kwa Mapanga au sijui Risasi 38 bali atatumia vitu tu vyepesi na hata usivyovitegemea na utashtuka tu ' Mlengwa ' ameshadhurika.

CIA, MOSSAD, KGB na MI5 pamoja MI6 huitumia hii sana na hata wana ' Taasisi ' wengi wa nchi zingine wakienda ' Kujiendeleza ' katika hizo nchi nao hupewa mbinu hizi za Kisasa kabisa na ambazo hata hazihitaji sijui nguvu kubwa wala gharama nyingi isipokuwa anayetekeleza anatakiwa awe tu na Kiwango kikubwa kama siyo cha juu cha ' akili ' nikimaanisha IQ.

Taasisi ya Tanzania inasingiziwa na kuonewa mno ni vyema tukatubu na hata ikiwezekana basi tukaiomba radhi kwani tunawavunja nguvu na wanaweza sasa ' wakasusa ' kweli kutekeleza wajibu wao hala tukashangaa huku juu Rwanda imeshakamata sehemu ya ardhi ya Tanzania na kule chini napo Malawi imehodhi Ziwa Tanganyika lote.

Hebu tuadilike na tuwatie moyo wana ' Taasisi ' kwani wanafanya Kazi ngumu na nzito pengine hata kuhatarisha maisha yao kwa ajili tu ya Kunilinda Mimi, Kukulinda Wewe na Kuwalinda wale. Hata hii amani iliyopo nchini nadhani ' Tuzo ' kubwa iende kwa ' Taasisi '.
 
Kama taasiasisi imeshiwa mbinu je

Mkuu hili ni ' Tusi ' kubwa sana Kwao. Unaweza kutengua hii Kauli Mkuu? Hivi kweli kuna ' Taasisi ' yoyote duniani inayoweza kuishiwa nguvu? Hakuna mahala ambapo hufanyika a thorough vetting ya kuwapata wana ' Taasisi ' kama huko ' Taasisini ' na wengi waliopo huko Kwanza wana IQ kubwa na za hatari na wako very talented na hiyo Fani.
 
Chief Genta,

Kuhusishwa kwa taasisi kupo kwa aina mbili. Moja nimojawapo ya taasisi yenye nguvu ya kujua nani anafanya nini au anataka kufanya nini. Hivyo wanauwezo na nyenzo ua kuzuia uhalifu usitokee.

Pia tunatambua sio kila uhalifu unaweza kuzuilika lakini pale unapojitokeza kwa style ile ile kwa kundi fulani la watu unapata shaka. Human thonking lazima itakuambia wanahusika kwa maana wanawajua na wamekaa kimya.

Namna ya pili inawezekana ndani ya taasisi hiyo kuna kikundi kidogo chenye weledi wa mambo kimeamua kutekeleza uhalifu nahawajulikani. Kwa sababu maisha yetu na usalama wetu teweka mikononi mwao na hatuoni jitihada za makusudi kutokomeza uovu huo, again ubinadamu unatuambia wanahusika.

Pale uhalifu unapomlenga mtu mkubwa wa upande ule hatua za haraka huchukuliwa na tunaona wahusika wanakamatwa. Kulikoni wakifa upande wa wanyonge?

Double standards kwenye mambo ndio kigezo kikuu kusema taasisi ile inahusika.

Naweza kukubalina nawe tena kwa 100% katika maelezo yako hayo ya aya ( paragraph ) ya Tatu kwani hata huku ' Kitaani ' nimeshawahi kuwasikia Watu fulani fulani Wabobezi Wastaafu ' Kitaasisi ' wakiihusisha kwa namna moja au nyingine. Tena Wao wakaenda mbele zaidi kwamba ' aliyeteuliwa ' hakutegemewa na badala yake wapo ambao walikuwa wameshajiaminisha kuwa watakuwa ma DG na ma DDG ili waendelee ' Kutumbua ' lakini Mwanamume wa Shoka kutoka Mkoani Geita akawafanyia bonge la ' Sapraizi ' kwa kuwaletea Bonge aliyekuwa NIDA hivyo ni kama vile walioachwa wamekasirika na kwakuwa wanajua mifumo yote ya ' Kitaasisi ' wameunganisha nguvu na wale ' Maadui ' zetu wa ndani na nje kufanya haya tunayoyaona ili kumuharibia Mwanamume wa Geita pamoja na Bonge wa aliyekuwa NIDA kisha nchi ichafuke mbele ya macho ya wengi duniani.
 
Sasa hapo nashindwa kukuelewa.

Kama hilo chaguo ndio sahihi kwa maana weledi alipaswa kuwa ahead of time. Intel community siku zote suppposed kuwa mbele ya muda na sio nyuma ya muda.

Pili kama wewe umeweza kujia hayo yote umeshondwaje kushauri hatua stahiki zichukulie hujuma zikome?

Ngoja niingie kazini kubeba box. Na wanaeast Africa good nite.
 
Unajichosha sijui kama yupo anayekusikiliza zaidi ya lumum...

Hapa nawasilisha mtazamo wangu tu ambao hata hivyo sijamlazimisha Mtu yoyote akubaliane nao ila nakushangaa Wewe ulivyoweza Kujichosha kuja Kuufuata uzi ambao umeshauona utawachosheni wana Ufipa na Biafra. Sasa kama pia umejua kuwa huu uzi ni wa Mimi na wana Lumumba wenzangu kilichokufanya ' ushoboke ' kwa Kiherehere ni nini?
 
Mkuu hili ni ' Tusi ' kubwa sana Kwao. Unaweza kutengua hii Kauli Mkuu? Hivi kweli kuna ' Taasisi ' yoyote duniani inayoweza kuishiwa nguvu? Hakuna mahala ambapo hufanyika a thorough vetting ya kuwapata wana ' Taasisi ' kama huko ' Taasisini ' na wengi waliopo huko Kwanza wana IQ kubwa na za hatari na wako very talented na hiyo Fani.
mtazamo wako utaheshimiwa ila utabakia kuwa mtazamo wako, nawe ukubali kuheshimu mtazamo wa wanao amini tofauti na unacho kiamini.
 
1.Rais ni mwongo maana aliongea tarehe 14/10/2017 kuwa kuna Watumishi wa Umma 59,000+ watapandishwa madaraja mwezi Novemba lakini hadi sasa hajapanda hata mmoja.

2.Rais alisema baada ya uhakiki kumalizika kutakuwa na maslahi bora kwa Watumishi wa Umma lakini hadi sasa wamepewa za uso.

Waandishi wa habari hizi hazifai kupamba kwenye front page maana sijawahi kuziona.

Kutoka hifadhi ya misitu ya Madihani
Mwanachama wa CCM.
 
Nimeipenda

Nasubiri siku watu watakapoumbuka na kulia wakishajua ukweli wa kinachoendelea
 
Back
Top Bottom