Wewe ni kipi ambacho Kikwete alifanya vibaya ukampinga?
Badala ya kuja na hoja, una-attack personalities.
Tuambie ni kwa nini wewe unaona ni bora kutengeneza katiba kwa kupitia tume badala ya baraza la katiba?
Tumbie basi wewe umechuja nini?
Mbona hamjibu hoja mnaishia kusema bravo tuu?
Sijui watu wetu wana matatizo gani!? Sote tulikuwa tunajua sheria iliyotungwa inatakataza watu kuzungumzia muungano au hata kutaka kuuvunja. Sasa watu wakashabikia lakini leo wanataka 'watu waruhusiwe kujadili Muungano". Hivi wakati inakatazwa kwanini hawakuchukua msimamo huo? Nilivyosema awali bado ni kweli - wale waliounga mkono na wenye kukubali mchakato huu hawana haki ya kulalamikia matokeo yake kwani matokeo yalikuwa dhahiri toka mwanzo.
Sijui watu wetu wana matatizo gani!? Sote tulikuwa tunajua sheria iliyotungwa inatakataza watu kuzungumzia muungano au hata kutaka kuuvunja. Sasa watu wakashabikia lakini leo wanataka 'watu waruhusiwe kujadili Muungano". Hivi wakati inakatazwa kwanini hawakuchukua msimamo huo? Nilivyosema awali bado ni kweli - wale waliounga mkono na wenye kukubali mchakato huu hawana haki ya kulalamikia matokeo yake kwani matokeo yalikuwa dhahiri toka mwanzo.
Wewe utaje kipi kizuri alichofanya Rais yeyote kabla ya Kikwete ambacho Kikwete hajakifanya zaidi. Nakwambia hutopata, mtabaki kutafuta vya kutafuta, ooh mara kofia, mara picha, hamna cha maana hata kimoja. Mnajua ndani ya roho zenu kuwa Kikwete ni Rais bora kwa Tanzania kuliko yeyote wa kabla yake.
Ya kutoka usingizini ukataja ni kama haya;
1. Kudhibiti Mfumko wa bei
2. Kuchujuka kwa wapiga kura
3. Kuimarisha thamani ya Shilingi
4. Kushindwa kusimamia ilani ya chama chake
5. Hata chama kimemshinda!.
Sijakaa kuhorodhesha ni mengi mno.
Hatukutaka ashindwe kama wenzake walivyoshinwa ila aweze waliyoshindwa.
Watu tulikuwa na matumaini kuwa ataweza lakini wapi ndiyo maana kura zilishuka mno!.
Ajabu hata kutazamia hawezi!.
Ukitaka aliyoweza uliza utajiwe pia.
Nahisi umeakisi ID yako1. Mfumko wa bei si tatizo kubwa sana, ni tatizo la dunia nzima kwa sasa, hujasikia Ethiopia na Ugiriki. Tatizo kukiwa na mfumko wa bei halafu ukashindwa kununua unachokihitaji.
2. Sijakuelewa, kwani wao magwanda (nguo) hata yachujuke?
3. Thamani ya Shillingi, ikiwa imeshuka, kwanini hutumii fursa hiyo kuuza mahindi yako nje ya Tanzania? au huna?
4. Ilani ya chama chake unaijuwa weyee? Chama kimemshinda?
5. wakati chama hicho hicho ndio wanaongoza nchi, au hilo hulijui? Utachekwa!
kuna mambo ya awali ya yote ambayo Mzee Mwanakijiji umeyaacha na hapo ndipo mushkeli wote unakoanzia. Huwezi kutumia sheria za kawaida kuanzisha machakato wa kubadilisha katiba. Sheria za kawaida zahitaji simple majority ya wabunge kulingana na koram tu wakati marekebisho ya katiba huhitaji zaidi ya 2/3 ya wabunge wote bila ya kujali mahudhurio yao.
Kwa lugha nyingine sheria ambayo AG alikwenda nayo ya mchakato wa kurekebisha katiba inakiuka katiba...it is unconstitutional.period hakuna kifungu chochote kwenye katiba yetu ambacho kinaruhusu sheria za kawaida ktumika kunyambulisha katiba iliyopo bali sheria iliyopo ya kikatiba ni kupitia 2/3 ya Bunge lote.
Pili, utaratibu wa kukiuka katiba ni wa makusudi kwa sababu waliona iakuwa kupata idadi ya wabunge wa 2/3 kuweza kupitisha marekebisho ya kikatiba na kwa kufanya hivyo waliunda utaratibu wa ukwiukwaji wa katiba ili kulinda masilahi yao wenyewe.
Tatu, kutokana na mapungufu makubwa ya kikatiba ya sheria ya kurekebisha katiba basi tume aliyoiunda JK kusimamia mchakato wa kukusanya maoni ni batili, na hayo mabunge yote mawili ni batili bila ya kuangalia kama wanayo mamalka ya kikatiba ya kufanya hivyo. katika hukumu ya Mahakama Kuu ya Kenya dhidi ya mkutano wa Boma mahakama kuu ya Kenya ilitumia hoja hizo hizo kujibu ya kuwa mkutano wa Boma uliojumuisha wabunge, wanaharakati na warasimu ulikua batili kwa sababu wamiliki wa kenya ni raia na nafasi sawa hazikutolewa katika kuchagua tume na wananchi walipaswa washirikishwe....................hii kwa mahakama zetu ni hoja ambayo itatupwa kwa sababu kama huhoji uhalali wa sheria ya kurekebisha katiba kama imekiukakatiba utashindwa kuwashawishi kwa hoja ulizozibandika kule kwa sababu watesema demokrasia yetu ni ya kiuwakilishi tu.................kwa hiyo hao ni wawakilishi wa wananchi ingawaje hawakutumwa kwa minajili ya kurekebisha katiba..........
Ruta, hayo yote unayoyasema nilishayasema huko nyuma. Ndio maana miye kwa dhamira yangu siamini kabisa kuwa mchakato huu una uhalali wowote na ninawabeza wale wote ambao wameukubali na kuukumbatia kwa vile "Rais kasema"!
Mojawapo ya vitu ambavyo huwa navikwepa sana ni kujaribu kuwawazia watu wengine; tayari tumeonesha tatizo wengine wafikirie nini cha kufanya
Mzee Mwanakijiji I see where you are driving at....."not my cup of tea"....Are you not running away from our journalistic onus............to educate, inform and where relevant to entertain the society?
[MENTION]unajua mojawapo ya vitu vibaya sana ni kujaribu kuwaza kila kitu. Kuna tabia siku hizi utaiona sana ambapo utakuta watu wanasema "nyie mnaandika kukosoa tu andikeni basi na nini kifanyike". Kimsingi wanaosema hivi hawataki kufikiria nini kifanyike; wanataka watu waaambie tatizo, wawafikiria namna ya kulitatua na usipoangalia hata kupanga bajeti ya jinsi ya kulitatua.