Kwanini napinga mchakato wa Katiba Mpya ulivyo sasa na kwanini wewe pia yakupasa uupinge

mm ww ni mtu usiyeridhika hata siku moja,ni mwenye chuki ya asili na huna nia njema na watanzania kwa sababu ww una enjoy huko utumwani.tuache tupate katiba mpya plz

mkuu sio lazima kuchangia kila mada.inaonekana umekurupuka. wenzio wanakuja na hoja wewe unakuja na viroja jibu hoja sio kupinga bila sababu.!
 
Ni kipi cha Kikwete ambacho hujakipinga, wewe unaejiita "Mzee Mwanakijiji"?

Chuki zako kwa Kikwete ni dhahiri kabisa na sababu zinajulikana.

Pole sana, wewe baki na kupinga, sisi tunapeta na mchakato wa katiba mpya. Naona hata magwanda wamekukera sana walipoenda kupata juisi Ikulu na kutoka wakiwa wametulizwa munkar.

Another first and history in the making for Kikwete. Kudos Jakaya.
 
Vyovyote iwavyo haiwezekani CCM ikawa na wajumbe wachache mkuu mwanakijiji, kwa mujibu wa hiyo hiyo katiba wabunge ndio wawakilishi wa wananchi na kama ccm ina wajumbe wengi basi ndio yenye uwakilishi mkubwa wa wananchi na sioni kama kuna ishu kwa wawakilishi walio wengu kudominate bunge.

Hoja ya 50% instead ya 2/3 imetulia kiasi fulani na ninaiunga mkono, lakini nafikili kwa kuwa bado katika taifa letu tuna hali ya ushabiki na kukomoana zaidi kuliko kuangalia maslahi inawezekana hiyo 50% ni bora zaidi kuliko 2/3 ambayo ingewafanya wale mahasimu wa jadi kukomoana kama tunavyoona katika miswada mbali mbali.

Mwisho mfumo wa kisiasa wa kenya, wa kimaisha, na wa kitabaka uliopo kenya unatofautiana sana na tanzania, sikubaliani na wewe kuitumia kenya kama "model" kwa tanzania, mfano TZ tuna swala la muungano kenya hawana, Kenya ukabila ni asili yao TZ hatuna na mambo mengi. kwa hiyo TZ lazima itakuwa na mambo yake rasmi na yenye utofauti kuliko nchi kama ya kenya.

Naunga mkono tume na mchakato wa katiba kwa 70% kuliko kupinga kabisa.
 
Kila atachoandika mwanakijiji humu basi wafuasi wake hawachuji wao wanabeba tu kwa hilo hongera mzee.any way Bravo JK kwa kuwezesha uundaji wa tume ya katiba,we hope for the best.
 
Ni kipi cha Kikwete ambacho hujakipinga, wewe unaejiita "Mzee Mwanakijiji"?

Chuki zako kwa Kikwete ni dhahiri kabisa na sababu zinajulikana.

Pole sana, wewe baki na kupinga, sisi tunapeta na mchakato wa katiba mpya. Naona hata magwanda wamekukera sana walipoenda kupata juisi Ikulu na kutoka wakiwa wametulizwa munkar.

Another first and history in the making for Kikwete. Kudos Jakaya.

Wewe ni kipi ambacho Kikwete alifanya vibaya ukampinga?
Badala ya kuja na hoja, una-attack personalities.
Tuambie ni kwa nini wewe unaona ni bora kutengeneza katiba kwa kupitia tume badala ya baraza la katiba?

Kila atachoandika mwanakijiji humu basi wafuasi wake hawachuji wao wanabeba tu kwa hilo hongera mzee.any way Bravo JK kwa kuwezesha uundaji wa tume ya katiba,we hope for the best.

Tumbie basi wewe umechuja nini?
Mbona hamjibu hoja mnaishia kusema bravo tuu?


 
M. M. Mwanakijiji

Kuamua kushiriki mchakato huu wa "mabadiliko ya Katiba" kama ulivyoanzishwa na kusimamiwa na Chama cha Mapinduzi ni kukubali matokeo ya mchakato huo na hivyo kuupa uhalali ambao ninaamini kabisa hauna.

Ni kweli ukiangalia kidini au ki-muungano hii tume haijawiana lakini tujilulize kwa niini?
Kwanza hii ni tume na sio baraza la uwakilishi; Kazi yake ni kukusanya maoni, kufanya majumuisho na kutoa pendekezo kutokana na maoni yetu tutakayoyatoa. Si lazima tukubali mapendekezo hayo. Mfano tume ya vyama vingi maoni yetu wengi yalikuwa hapana lakini wakapendekeza tuende vyama vingi jambo ambalo lilikuwa likataliwe na utawala wa wakati huo lakini Mwalimu akatumia busara ikabidi wakubaliane nae.
Kwa misingi hiyo uwiano hapa si mahali pake


Pili: Swala la Muungano na uwiano Ni vizuri tukazingatia kuwa Tanzania ni muungano wa nchi mbili na si watu 9 na mmoja hivyo maamuzi ya kimuungano hayazingatii ukubwa wa nchi wala idadi ya watu bali ni nchi na kila upande una haki sawa. Ila swala kuu hapa ni kuwa Muungano wetu una mapungufu mengi ambayo ndio yanayotakiwa yaangaliwe kwa uwazi ili tuweze kuwa na muungano unaozingatia tofauti na mfanano wetu mambo ambayo hayakuzingatiwa wakati wa kuweka muungano huu pengine kutokana na mazingira ya wakati ule.


Swala La Uwiano ni la muhimu sana pale tunapokuja kwenye Baraza la kutunga katiba ambalo kutokana na sheria iliyopitishwa na wenye kutawala nchi kwa leo ndio kuna mapungufu makubwa ila kwa kuwa swala la katiba ni la Maslahi vile vile na tusisahau kwamba katiba nzuri ni tishio kwa maslahi ya wanaotawala sasa hivi na hilo wanalijua fika kwa hiyo huu mpambano hautaishia hapa Mwanakijiji amepambanua vizuri sana kuhusu mapungufu yaliyoko kwenye Baraza hili na kwa kweli ukiliangalia ni kuwa hii kwa kiasi kikubwa itakuwa katiba ya Chama na si ya watu. Na pia sijaona kama swala la Muungano linaguswa vipi maana kutokuliangalia kwa mapana yake ni kuendeleza ugonjwa.


Sasa nini jukumu letu sisi tunaoelewa fika kuwa mchakato huu una mapungufu makubwa na ni wazi mwisho wake katiba itakayopatikana itakuwa na mapungufu. Wajibu wetu ni kujitokeza kwa wingi, kujenga umoja na kuweka msukumo mkubwa kwa tume kuhakikisha maoni yanakusanywa kwa uhakika. Vile vile kutakuwa na haja ya kuweka msukumo mkubwa kwenye baraza na baadae tutapima Kama katiba itakayopendekezwa ni bora kiasi gani kuliko hii ya sasa na kama ikionekana ni ubabaishaji ndio tutapima nguvu mbadala kwenye kura ya maoni kwa kuipinga kama ODM walivyofanya Kenya. kTatizo lingine kubwa linalotusumbua hapa ni ile hali ya watawala wa sasa kujisikia "Wao ndio wao, na hawatingishiki" Kwa kimombo "A sense of Impunity".

Lakini nasisitiza nguvu ya kimasilahi ya wanaofaidika na katiba ya sasa ni kubwa hivyo mpambano huu ni mrefu na ninaamini hata hiyo katiba ikipita kesho yake tutaendelea kudai katiba ya kweli ya wananchi.

Hayo ndio maoni yangu kwa kuwa siamini kupinga kwa maana ya kupinga tu ni tija kama hatutajiuliza tutapinga vipi na tupime matokeo ya kupinga huko. Kwa kifupi Tupinge kwa kushiriki kikamilifu.
Mungu ibariki Tanzania na watu wake na utujalie muamko wa kutumia fikra zetu kwa manufaa ya nchi yetu!
Reply




 
MNzeee Mwanakijiji,

Nimekusoma na kukuelewa vema sana na nakupongeza sana kwa hili maana nilifikiri niko peke yangu hasa baada ya vyama na sijui asasi gani kukubaliana na muswada ule na kuupitisha kuwa sheria. Nilisikitika sana niliposikia Chadema walikubaliana kimsingi na mfumo mzima wa maandalizi isipokuwa vipengele vidogo ktk idadi ya wahusika na kadhalika, lakini binafsi yangu niliona ni muhimu zaidi kwanza kamati ya bunge ya kutunga katiba ichaguliwe mbele ya Tume ya kuratibu katiba, na wakapewa mamlaka yote ya kuchambua na kuhakikisha Katiba mpya inawagusa wananchi wote maana huko ndiko kwenye mzizi wetu. Hawa ndio wangeweza kuchagua tumew hata kama tume hiyo ingekluwa hii tunayoina leo, lakini wangekuwa answerable to Kamati ya Katiba ya bunge..

yawezekana kungekuwa na mvutano mkubwa kuipata hiyo kamati ya Bunge lakini nina hakika sura nzima ya kile kinachokuja kingeanza kujionyesha wazi baada ya kuundwa kwa kamati ya Bunge. Lakini ndio tumeshayavulia nguo maji haya hatuna budi kuyakoga yawe japokuwa naviona viwavi vikielea..
 
Mwanakijji,
Una hoja. Lakini ondoa hofu kwa sababu wananchi wengi wanaanza kuwa na mwelekeo mzuri wa elimu ya uraia, inawaingia na wameanza kutambua maslahi yao ya kisiasa. Kama utatokea uchakachuaji, uhai wa katiba mpya utakuwa mfupi sana - pengine siyo zaidi ya 2020 kama CCM itashinda uchaguzi wa 2015. Ikishindwa imekula kwao, chama chochote litakachoingia madarakani kitaanza siku ya kwanza na mchakato wa kuwapatia watz katiba ambayo itakidhi matarajio yao ya siku za usoni hususan vijana. Jaribu kuwa na subira. Sina wasiwasi Rais Kikwete ana dhamira ya kweli.
 
yale yale ya edwin mtei- "waislamu ni wengi kuliko wakiristo", Kama nikiunga mkono, naunga mkono aina ya tume itakayozingatia usawa wa haki na wajibu wa raia na si usawa wa idadi ilimradi idadi-tukianza kudai usawa wa kinamba namba basi sijaona mzanaki hata mmoja kwenye hiyo tume, je wazanaki maslahi yao yatawasilishwa na nani?

somalia baada ya kuwaliwa kimabavu na siadi bare sasa wameweka katiba ambayo inamnyan'ganya raisi madaraka na kugawa kwa bunge, mahakamakuu na raisi mwenyewe. Sisi hapa baada ya kutawaliwa na chama kimoja miaka mingi na kufanyiwa maamuzi ya kimaudhi na viongozi wa wakati huo, bado tunadanganyana kuhusu katiba.

Maamuzi ya kufuta kiingereza, kupelekwa vijini kinguvu, sogeza,kuvunjwa uhusiano wa kibalozi na Israel, hayo yalikuwa ya mtu binafsi na sio ya umma. Hivyo katiba yetu ni lazima ihakikishe raisi hafanyi maamuzi makubwa bila bunge na mahakam a kuu kushauliana nazo.

sasa ukiangalia katika wajumbe waliopo ktk katiba team karibia wote ni mashabiki wa azimio la arusha. wote wlitawala na kula raha ya chama kimoja. wote hawataki kuhusiana kibalozi na Israel.wote hawana habari na kupanua secta za usanii kama michezo, filamu na muziki. wote ni maadui wa western europe n, Israel na USA(anti west).wengine wamemkana mungu na hawa ndio hawajui haki za binadamu wala kusikia mahakama kuu ina kuwa huru.

wewe unategemea nini kutoka kwa watu kama hao?wameisha tengewa 40 billion za kutumia halafu mwisho wa siku hutasikia la maana. wewe ona tuu tume ya kumshtika Luhanjo na wenzake imeishia wapi? Tume ya richmond imeishia wapi?. somalia ndio hao watatuacha na sisi tutabakia pale pale pa chama chashika hatamu!
 
Kuna vitu kama :
waziri wa ulinzi, fedha na mambo ya nje lazima vyeo vyao vipigiwe kura bungeni ndipo raisi waapishe na kuwapa mikoba. sijui kamswla hili litawekwa ktk maoni ya watu.

halafu kuna :protective policy of our own local products. sijui kama nayo itawekwa ktk maoni. maana mikataba mingi sana imeua viwanda vyetu kama kilimanjaro na mang'ura mashine too kwa sababu ya kuagiza nchi za nje bidhaa ambazo hutengenezwa humu humu nchini.

siji katika hiyo team ya katiba kama kuna wachumi wa kutosha . wengi ni makada na mashabiki wa zidumu fikira sasa za mwenyekiti wa chama. jamani tusiige katiba ya Iran bali tuige ya Israel.
 
Yaani Tanzania nzima ni mtu mmoja tu ndiyo anakuja na hoja zinazoweza kutafsiriwa kama hoja za msingi au "zilizoenda shule" kupinga mchakato mzima wa katiba mpya hadi ulipofikia hivi sasa ambapo Wanatume au Wajumbe wanaapishwa waziwazi? Iweje Wasomi waliobobea kwenye masuala ya katiba na kisiasa kiujumla kama kina Shivji, Tundu Lissu, W. Slaa, Jenerali Ulimwengu, Baregu et al hawafurukuti kuhusiana na mchakato mzima? Watanzania ni taifa lenye watu wavivu wa kufikiri na ignorant wa masuala ambayo ni complex kisiasa na kisheria, na ndiyo maana wataendelea kudhulimiwa na kunyanyaswa milele na CCM. Nilitegemea angalau Watanzania wangejifunza kutokana na mazingira yaliyosababisha mabadiliko makubwa ya kikatiba na kisiasa yaliyotokea nchi jirani kama Kenya miaka ya karibuni.
 
Ni kipi cha Kikwete ambacho hujakipinga, wewe unaejiita "Mzee Mwanakijiji"?

Chuki zako kwa Kikwete ni dhahiri kabisa na sababu zinajulikana.

Pole sana, wewe baki na kupinga, sisi tunapeta na mchakato wa katiba mpya. Naona hata magwanda wamekukera sana walipoenda kupata juisi Ikulu na kutoka wakiwa wametulizwa munkar.

Another first and history in the making for Kikwete. Kudos Jakaya.

Yaani ww CDM walipoenda kumuona rais akili yako ilikuwa busy inawaza watakunywa nini badala ya watazungumza nini? Kwa hiyo upeo wako umeishia kwenye juice tu.
 
Kila atachoandika mwanakijiji humu basi wafuasi wake hawachuji wao wanabeba tu kwa hilo hongera mzee.any way Bravo JK kwa kuwezesha uundaji wa tume ya katiba,we hope for the best.

Ingekua heri ile sunami ingefanya tufani na wimbi lake lingekukumbatia na kukupa busu la kifo,
Dunia haihitaji watu wasioweza kujifikiria, wasioweza kujithamini tena wamelemewa na ujinga ni wajinga, MM umetupa changamoto kama tunajitambua ama la!!!!
 
Nimepata matumaini!!! Asante. Umeeleza kwa kifupi kabisa nilichotumia maneno mengi kukielezea.

Naunga mkono hoja ya mwanakijiji.

Mimi nataka kipengele kimoja tu kisiwekwe ktk katiba hiyo mpya, kuwa mabadiliko yoyote ya katiba hayatafanyika mpaka ipite miaka 50. Kipengele hicho kisipokuwepo serikali tarajiwa ya Chadema italeta katiba mpya baada ya 2015 kama ccm watachakachua mchakato huu kama dalili inavyoonekana wazi.
 
Hotuba ya Rais wetu JMK wakati amemaliza kuwaapisha wanaounda Tume hii imejibu baadhi ya hofu zetu hapa. Wateule wengi wa Tume hii ni watu ambao wako huru kiakili na kimawazo. Sielewi ni kwa namna gani unaweza kumburuza mtu kama Prof Baregu, Dr Mvungi, Ali Saleh,...Tukubali mchakato huu uendelee. Una ngazi na hatua nyingi. Tuwe karibu na Tume hii na kuifuatilia kwa karibu sana. Watu kama wewe Mwanakijiji, Profesa Issa Shivji, Jenerali Ulimwengu na wakali wengine wa humu JF na kwingineko mna mchango wenu mkubwa tu mkiamua kuwa WAZALENDO.
 
Hotuba ya Rais wetu JMK wakati amemaliza kuwaapisha wanaounda Tume hii imejibu baadhi ya hofu zetu hapa. Wateule wengi wa Tume hii ni watu ambao wako huru kiakili na kimawazo. Sielewi ni kwa namna gani unaweza kumburuza mtu kama Prof Baregu, Dr Mvungi, Ali Saleh,...Tukubali mchakato huu uendelee. Una ngazi na hatua nyingi. Tuwe karibu na Tume hii na kuifuatilia kwa karibu sana. Watu kama wewe Mwanakijiji, Profesa Issa Shivji, Jenerali Ulimwengu na wakali wengine wa humu JF na kwingineko mna mchango wenu mkubwa tu mkiamua kuwa WAZALENDO.

Wildcard, hivi unajua aliwateua bila hata kuwauliza kama wanataka kuwemo kwenye tume?
 
Wildcard, hivi unajua aliwateua bila hata kuwauliza kama wanataka kuwemo kwenye tume?
Najua. Mzee wangu Butiko alikuwa hana taarifa kabisa. JMK alisema majina alooteua ni yale yaliyopendekezwa na watu na asasi mbalimbali. Kwa maana hiyo alizingatia maoni ya wengi. Ukiangalia majina haya, hasa yale ya Bara kama angelazimika kuiunda Tume hii mwaka 2006 asingeyakubali. Hili ni "advantage" kwa WATANZANIA na ndio maana hayajapingwa hadharani. Kumbuka Mwalimu alivyounda Tume kama hii mwaka 1977 ya "WATIIFU" watupu akina Sheikh Thabiti Kombo, Pius Msekwa,...
 
Rais kwa mfano amechaguliwa na asilimia 61 ta wapiga kura ambao ni karibu milioni 6 hivi kati ya watu miliioni 42! Sasa kama kiwango kingekuwa ni asilimia 50 ina maana watu kama milioni 4 hivi ndio wanaweza kumchagua Rais. Lakini je watu milioni 4 kwenye chama chenye wanachama milioni 5 hivi haiwezekani kwamba wenye chama kuwa ni wengi zaidi na wakapitisha katiba ambayo itaungwa mkono na chama chao?
Ukiweka kiwango cha katiba mpya lazima ipite kwa zaidi ya asilimia 70 ya wapiga kura manake ni kuwa lazima kutakuwa namazungumzo, compromises n.k. Kwa sasa hivi, CCM haiitaji kabisa wapinzani kwenye suala hili zaidi ya 'token participation' ambayo wamepatiwa hadi hivi sasa.

Hapa nimekufahamu sana Mwanakijiji. Ukiangalia hizo takwimu ulizoweka, kuna uwezekano katiba kupitishwa hata na watu milioni tu na ikawa KATIBA YA WANANCHI, kwa kuzingatia kuwa idadi inayotakiwa ni asilimia 50 ya kura zilizopigwa na sio asilimia 50 ya idadi ya watu wenye haki ya kupiga kura. Baya zaidi, kura ya katiba mpya haipigwi na wananchi wote bali na watu 602 kuwakilisha watu si chini ya milioni 20 wenye haki ya kupiga kura. Matokeo yatakayopatikana kuhalalisha Katiba Mpya NI MSIBA KWA WATANZANIA, NI MSIBA WA TAIFA.

Mada yako ni "Kwanini napinga mchakato wa Katiba Mpya ulivyo sasa na kwanini wewe pia yakupasa uupinge."
Mmoja amesema hapo juu kuwa wazo lako ni zuri sana lakini ni sawa na kufunga banda la kuku wakati wote wameshatoka nje, lakini mimi badala ya kuwa na mawazo hasi, ningependa tuwaelekeze wananchi juu ya namna gani waupinge huu mchakato. Kijuu juu kupinga kwa Watanzania itakuwa tu kutoshiriki katika kura ya maoni na hilo halitaathiri matokeo.

Ningelishauri, kwa kuwa wanaharakati na vikundi wa kuweka shinikizo kwa kupitia wanasheria, waishitaki serikali na kusimamisha mchakato huu. Katika maelezo yako, kipengele kimoja tu cha tafsiri potofu ya "Soveignty/Hakimiya" kinatosha kama pahali pa kuanzia.

"Mtu hawezi kukupandia mgongoni ikiwa wewe hukuinama". Kuuruhusu mchakato kuendelea ni sawa na Watanzania kuinama na kuiruhusu CCM kuendelea kutupandia mgongoni, mabegani, kichwani au vyoyote tukavyoita.

Mzee Mwanakijiji, ni sasa au sasa. Tuwaongoze Watanzania sio tu kuupinga mchakato kwenye majukwaa bali mahakamani, Mahakama ya Katiba.
 
Back
Top Bottom