Jacobus
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 4,700
- 1,721
Wakuu, mie ni mtoto wa zamani. Nimeona nifunguke baada ya kusangazwa na wengine kunistaajabu kusikiliza vipindi vya radio TBC Taifa.
Ukweli huwa nafarijika hasa usiku kuisikiliza radio hii (ya Taifa) kwani vipindi vyake huburudisha na kuelimisha vema.
Vipindi takriban vyote vinabebwa kwa kiswahili hata kipindi cha burudani cha 'Muziki wa kantri' ni kiswahili tofauti radio nyengine kwa kukiita kipindi hicho 'Country music'.
Muziki unaopigwa ni ule wa bendi zetu kama Juwata, Maquis n.k. na hata za nje kama T.P. Ok jazz Lipua Lipua n.k.
Lugha wanayotumia watangazaji wake ni ya STAHA mno na nyepesi huwezi kumsikia mtangazaji akisema 'sasa nasoma meseji zenu.........' ila utamsikia 'sasa nasoma ujumbe wenu wasikilizaji.......', au 'sasa tunawaletea matangazo live na siku hizi tunaambiwa Kiarabu-mubashara', TBC watakuambi 'sasa tunajiunga kwa matangazo ya moja kwa moja toka.......'. Kwa kweli ni mengi sana radio hii inayadumisha.
Keep UP TBC Taifa.