Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,786
Sijawahi kuelewa mpaka leo hii ni kwa nini Kiongozi wa kwanza wa Taifa hili Mlm.Nyerere anapendwa sana hapa kwetu, wkt kiukweli Nyerere anapaswa achukiwe sana siajabu klk Viongozi wote waliopita kama tulikuwa tunatafuta sababu ya kuchukuia Viongozi wetu kama baadhi yetu tufanyavyo leo hii, Nyerere alifanya social experiment Tanzania!
Kwa wasiofahamu maana ya social experiment ni kama vile kutengeneza dawa mpya ambayo hauna uhakika nayo kama inafaa kutumiwa na binadamu hivyo unaamua kuijaribu kwa baadhi ya binadamu na ukiona inafaa basi unaitumia ukiona haifai unaitupa!
Na hicho ndicho Mlm.Nyerere na utawala wake ulichofanya Tanzania, lkn cha ajabu Mtanzania kwa Mlm.Nyerere humwambii kitu ni kama vile unamuongelea Mungu!
Na cha ajabu zaidi labda kuliko vyote kuna watu wanaoichukia CCM kuliko kitu chochote Dunia hii lkn wanampenda Mlm.Nyerere na kumuondoa kwenye lawama zote wanazoipa CCM, tena wanakwenda mbali na kumuita kwamba alikuwa Mwana demokrasia, kwamba Utawala wake ulikuwa wa kidemokrasia, hivyo nashindwa kuelewa mtu anawezaje kuitenganisha CCM na Mlm.Nyerere? Unawezaje kutenganisha Umaskini na kudumaa kwa uchumi wa Tanzania na Mlm.Nyerere? Unawezaje kumlaumu, Mwinyi, Kikwete, au Mkapa na kumuacha Mlm.Nyerere?
Watu wanaongelea kila siku matatizo ya Zanziba na Muungano wetu lkn Mlm.Nyerere wanamtoa kwenye equation na kulaumu wengine, hili linawezekana vipi?
Watu wanalalamikia khs Elimu ya Tanzania kuwa Duni na wanalaumu Maraisi wote lkn Mlm.Nyerere wanamtoa kwenye lawama, hili linawezekana vipi wkt Mlm.Nyerere ameongoza TZ kwa miaka 24 na ndani ya hiyo miaka kwa mfano hapa Dar hakujenga Shule hata moja ukiacha zile alizotaifisha ktk Taasisi za kidini, watu wengi wamesoma Shule kwa shifti wiki hii asubuhi ijayo mchana, tena Wanafunzi walikuwa wanakaa chini hakuna madawati, lkn lawama wanapewa maraisi waliofuata, kwa nini?
Binafsi mpaka leo sielewi ni kwa nini Mlm.Nyerere hata anapendwa hapa Tanzania, hata nikianza kungalia sifa zote anazopewa na ukianza kuichambua moja baada ya nyingine utakuta wala siyo yeye anayestahili hiyo sifa!
Tukianza na Kiswahili, wengi wanafikiri TZ tunaongea Kiswahili shauri ya Nyerere, siyo kweli, Nyerere amezaliwa amekikuta Kiswahili kinatumiwa TZ nzima, ukija kwenye umoja wa Kitaifa, TZ ilikuwa moja kabla hata Nyerere hajazaliwa na ameikuta moja, tofauti tu TZ iliitwa majina tofauti vipindi mbali mbali lkn haijawahi kuwa na mtengano wala vita vya wenyewe kwa wenyewe kabla, sasa sielewi kwa nini umoja wa Taifa hili anapewa sifa yeye!
Binafsi kama kuna jambo Mlm.Nyerere alifanikiwa kama vile Wakoloni Waingereza ni brain washing, au kupumbaza watu kiakili, watu wamepumbazwa, na ndiyo maana hapa TZ hakuna anayeweza kumlaumu Mzungu kwa lolote, Mzungu anapendwa na kuabudiwa kama Mungu na haijalishi Mzungu atafanya nini atatetewa tu, Mzungu mmoja akivamiwa na majambazi hata Bunge litasimama na kuanza kujadilia kama hoja ya dharura, Mzungu hata akipiga Mwafrika risasi tutamteteta na kumlaumu Mwafrika mwenzetu aliyepigwa risasi na Mzungu kwamba ni kosa lake, hiyo ndiyo maana ya brain washing ...