Kwanini Mwl Nyerere aliwauzia Waingereza Mgodi wa Almasi wa Mwadui Shinyanga?

humu JF kuna wengi wetu tunapenda kubeza ikiwa mtu ameleta mada inayohusu kitu muhimu
eti hii sio issue Nyerere alikuwa na makosa kama mtu yoyote yule kwanini tumlinde kama malaika? kwenye ukweli tukubali ndio demokrasia sio kila kitu tupinge,
Nyerere alifanya mambo mengi mazuri na mabaya kwenye nchi hii tokea vijiji vya ujamaa na azimio la Arusha mote amefanya makosa ingawa lengo lilikuwa zuri lakini mipango ilikuwa mibaya
Najuwa watu watapinga kila baya alilofanya Nyerere
Nachangia
 
[h=3]Tanzania[/h] Petra agreed to acquire the Williamson Mine in Tanzania in September 2008 from De Beers.[SUP][10][/SUP] The Williamson mine, which began production in 1940, has a reputation for the production of large, high value diamonds, with special stones (classified as larger than 10.8 carats (2.2 g)) produced regularly. The mine is also famed for its pink diamonds. In 1947, the mine's founder Dr. John Williamson presented Princess Elizabeth (later Elizabeth II) with a flawless 54-carat (11 g) pink diamond (the Williamson Pink Diamond) on her wedding day. The eventual 23.6-carat (4.7 g) cut diamond became the centre stone in the Williamson Diamond brooch and is supposedly the basis for the Pink Panther diamond in the film of the same name.
The Williamson Mine is currently thought to have a resource of 40,000,000 carats (8,000 kg) (995 million tonnes of kimberlite). It has a maximum mining depth of 205 metres and a very low stripping ratio. Energy and Minerals Minister William Ngeleja said Petra's entry is "an opportunity to breathe new life into Williamson Mine and Tanzania's diamond mining sector."

Wewe ni mburula tu, unaleta thread ambayo hata mwenyewe huielewi! sijui tatizo ni lugha au ukilaza wako uliozaliwa nao? sasa angalia hapo juu paragraph ya pili ya hiyo quote ambayo ni yako inasema production ilianza lini? hizi ndo akili za samaki alizowaambieni Aman Karume!shwain wahed!
 
Tabia ya viongozi kuficha Fedha walizokwapua ilianza Mwaka 1970 na Tafiti ya kimataifa ya masuala ya wizi wa kimamlaka imeonesha Awamu ya Nne inaongoza ikifuatiwa na awamu ya 3 then awamu ya kwanza lakini kuna Tumbili wanaamini wizi ulianzia awamu ya pili! Awamu ya kwanza ingekuwa na uwazi kama ulikuwepo kuanzia awamu ya pili tungejua mengi hata hivi sasa tungekuwa na RTD, mzalendo na uhuru pekee tungeomba mchakato wa kumtangaza Jakaya mwenye heri uanze sasa tunadanganywa elimu ilikuwa bure lakini wilaya nzima wanafaulu shule ya msingi watoto wawili, na kama elimu ilikuwa bwerere uhaba wa sasa wa wataalam kwenye kila tasnia umeanzia alipong'atuka?

Wakati Nyerere alipoona nguvu za Watanzania kudai serikali tatu inataka kumzidi nguvu, aliamua kuwatishia kwamba mtauana mtakapovunja muungano na kwamba yeye ataondoka na kuenda kuishi Uswiswi. Sasa kwa nini sehemu zote zilizopo duniani aamue kuenda Uswiswi? Uswiswi kuna biashara gani ambayo ingemuwezesha yeye kuishi huko?
 
wewe siyo raia wa Tz kama kinana na sheh ponda .... haya hayakuhusu

Nyie ndio wale vilaza mada inahusu mambo mengine wewe unadandia mkwaju kwa mbele Naamini kabisa nyie vimburu Nyerere enzi zake ingetokea siku akatangaza yeye ni Mungu au Nabii mgemuabudu kama Mao Tse Tung lakini alikuwa binadamu tu wakawaida tena saana tu ache ushamba Nyerere kakosea mambo mengi saana Enzi zake kuna waziri mmoja alikuwa anaiitwa Bhonke Munanka sasa hivi nae ni Marehemu alikuwa waziri wa Biashara na viwanda jamaa alikuwa Fisadi ila kwa kuwa alikuwa wa kwao huko mara hakujaribu kumkemea hata mara moja alioa mpaka waziri mmoja wa serikali ya Guinea alikuja na msafara wa Rais Ahmed sekou toure akamjengea bonge la kasri pale msasani ili hali yeye kafa kaacha nyu ba kama 60 pale kimara
 
Nyerere angekuwa hai wa kwanza kumfungulia mashtaka ningekuwa mimi alitutesa saana huyu kuanzia Elimu katunyima kabisa elimu huyu katupotezea fursa nyingi kiuchumi leo Kenya kutuacha mbali ni makosa ya huyu mzee alituvalisha tairi za gari chai tukaweka peremende nyeupe badala ya sukari viwanda alijenga havikuzalisha hata siku mmoja watu tukaishia kuvaa kaniki wakati viwanda vya Textile alijenga vikafika vitano kuna kiwanda alijenga shinyanga mpaka leo hakijafunguliwa Tanzania meat pakers
 
Mkuu wangu Ritz, ufisadi ndani ya nchi hii unaratibiwa na kufanikishwa vilivyo na wenzetu wa Roman Empire...Wengine tunabezwa na kuitwa majina kibao kama wazee wa gahwa, pekos, magaidi nk... Naamini iposiku wafuata upepo wanaoitumikia Roman Empire kwa kujua ama kutokujua soon watapata ufunuo. Nchi hii ni yetu sote, Mkwawa kule Iringa alistahili maziko ya heshima kama ya Rugambwa kule kagera, Bakwata inastahili kufanyakazi za waasisi wake! chombo cha waislam kiko wapi?, Jembe na Nyundo vyote ni silaha ya maangamizi kwetu sisi walala hoi...(loading...confusing?)... Mbege, Komon, Kangara, Wanzuki, Dengelua, ulanzi, babu lao gongo lapatikana karagwe mpaka kiboroloni, lapatikana nangurukuru mpaka mchamba wima, swali la msingi kwanini GONGO linakatwazwa? TBS? Ikelege?...Loading...confusing...OOoh my GOD wazungu wazuri sana, hawajamaa ni marafiki zetu wanatupa RV, wanatusaidia bajeti yetu, Kidumu CCM! WAARABU aaah grrrrrr hawa jamaa kwanza ni mabasha sana, Hata Gordon Brown si anatoka uarabuni? hawa jamaa laana kum eti wanataka ndoa za jinsia moja!...Grrrrr....NDUGU ZANGU GT, TANZANIA ni yetu! Hakuna wa kumlilia ili ukombozi kamili upatikane, kila mmoja wetu asaidie kuidhoofisha na hatimae tuizike CCM rasmi 2015 regardless dini yako, kabila lako, shule yako, status yako ya kimaisha..."Kunyoa zivuma si ujinga bali ni usafi"
 
Bahati alitoka madarakani kwa hiari angeendelea kun'gan'gania madaraka wangemulia mbali mungu nawaapieni watu walishamchoka watu humu JF Wanafiki sana Nyerere hakupendwa na Mtu yoyote Labda Kawawa na Kingunge Sozigwa butiku na wengine lakini Watu tulimchukia sana hatukumpenda acheni undumilakuwili huyu Mzee hakupendwa kabisa sababu ya Roho yake ilikuwa Mbaya Hasidi mkubwa Mbona Baraza lake la mawiziri wizara nyeti aliwaweka Wahindi Wizara ya Fedha Dr. Amir Jamal Leo wanae ndio wameliki wa J MAIL Pale Samora Wizara ya Nishati na Madini Alnoor Kassum Leo uliza leo familia yake wanamiliki Makampuni gani huko Canada lakini leo hii mbunge tu akiwa muasia watanzania wanapiga kelele Gabachori Kwani Mwalimu aliwapa wizara nyeti kama hakuwa Fisadi?
 
Nilisikitika Ngeleja aliposema mgodi unajiendesha kwa hasara! CCM wezi wakubwa.
Kuendesha mgodi siyo sawasawa na biashara ya machinga au fremu ya duka kama ilivyozoeleka nchini.

Kwa ulinganishi tu hebu anzisha uchimbaji na usagaji wa kokoto, na pengine utaelewa mambo makuu mawili, uwekezaji unaotakiwa na technolojia inanotakiwa.

Utaalamu wa kupiga domo tuwaachie wanasiasa, si thinkers.
 
Nimewahi kufanya kazi katika mgodi huu kwa miaka kadhaa hivyo historia inayozungumzwa hapa kiasi fulani ninaijua vizuri sana, ni kweli mwaka huo uliotajwa na bwana Riz1 ndipo ulipoanzishwa mgodi huu, mmiliki huyu bwana Williamson alifariki mwaka 1958 kwa ugonjwa ambao inasadikiwa ulisababishwa na mapenzi, ilikua amuoe huyu malikia wa sasa wa Uingereza, yaani Queen Elizabeth, baada ya jopo la wakuu wa Ikulu ya Uingereza kumkataa jamaa kwamba hafai kuoa kwenye Royal Family aliaanza kunywa pombe mfurulizo bila kula na afya yake ilianza kudhoofika hadi baadae mauti kumkuta, kwakua hakuacha familia hapa duniani (kwa Uraia jamaa alikua ni wa Canada) dada yake alirithi mikoba, sister wake huyu hakua na ujuzi na masuala ya madini ndipo aliamua kuuza kampuni hiyo kwa kampuni kubwa duniani ya Almas iitwayo De beers (Anglo America ilikua inaimiliki kwa asilimia 50 hiyo kampuni ya De Beers) viongozi wa De Beers walikua ni familia ya Waingereza fulani waliohamia South Africa iitwayo Openhammer (hawa jamaa wamewahi kua Billionaires No 1 Africa kwa miaka kadhaa mfululizo).

Mwaka 1967 wakati wa Azimio la Arusha, sote tunakumbuka Mwalim Nyerere (siku hizi tunamwita mzee Nyerere) alibinafsisha makapuni yote ya mabepari, Mgodi huu haukupona lakini hakuchukua share zote, aliwanyang'anya asilimia 75 na wao wakabaki na 25 tu hadi mwaka 1994 mzee mwinyi alipoamaua kuwarudishia tena De Beers, mambo yamekwenda hivyo na De beers nao wameamua kuuza tena kwa kampuni ya Petra, nachotaka kusema hapa, sio kweli kwamba Nyerere aliwahi kuuza mgodi kwa wawekezaji, yeye ndiye aliyewanyang'anya, ni kiongozi pekee aliyethubutu, swali linaweza kua, kwanini aliacha baadhi ya share na sio zote?

Kumbuka miaka hiyo tunapata Uhuru, hatukua kabisa na wataalam wa madini hasa fani za Geology, Mets, yaani mineral Processing na Mining Engineers, so ilikua busara kuacha baadhi ya share ili watalaam hao waendelee kuwepo, hata hivyo wazalendo waliendelea kuendesha mgodi huu kwa miaka mingi huku pia vinaja waliomaliza Form 6 wakichukulia na kufanya kazi pale then baada ya muda fulani walipelekwa nje ya nchi kusoma, hasa Urusi, Canada n.k, mifano yao ipo hadi leo, watu kama Mzee Mseluka, Philbert Rweyemam, familia ya akina Tesha, Shoo n.k wapo hadi sasa katika fani hizi za madini, huu ndio mgodi ambao ulikua na chuo chake, enzi hizo za mwalimu, tembelea migodi yote hapa nchini, product za Mwadui zinatamba hadi sasa, chuo kile kinachoitwa TES wawekezaji wapya walipokuja walikitosa na sasa Kanisa la Anglicana ndio linakimiliki baada ya kushinda zabuni ya ununuzi.

Niishie hapo though uandishi wangu leo sio mzuri kabisa, i am very sorry but get the idea.
 
Diamond is forever Ritz, vimigodi vya juzi vishaishiwa madini. Mwadui haziishi, pia huduma za mgodini muda huo zilikuwa 'half London' sababu ya uimara wa Nyerere (R. I. P). Je wajua baba Mwanaisha ana kamgodi kake pembeni in venture with Hillary Soud? Open your eyes
 
Last edited by a moderator:
Dah...hapo ndo "sorting" kwenye hilo jengo...nimezaliwa,kukulia na kusoma humu ndani!Mwadui Mine homie...enzi hzo tuliish kama Ulaya,maziwa unaweka chupa mlangoni na token unanunua duka kubwa,unaletewa maziwa mpaka mlangoni..upo kazini lakn unayakuta maziwa nje,huduma nzuri n.k!nilipotoka nje ya mgodi nilipata shida sana...Wakati haupo tena..enzi za Phantom,Meneja Silvanus Mipawa n.k!I wish maeneo yote ya Migodi Tz wangeish maisha ka ya mwadui ya miaka ya '90
 
masopakyindi Naujua mgodi wa Mwadui 'in-out' na kama swala ni kukosa faida, serikali ingewaachia wachimbaji wadogo wadogo (wabeshi) ili wajichimbie! Maganzo, Utemini, Idukilo, Magagi, Buchambi, Songwa, Zanziba, New Alamasi n.k.
 
Last edited by a moderator:
Nadhani unaandika ambacho hujakisoma vizuri.....Mgodi ulizinduliwa mapema 1940 na ulimilikiwa na de boers chini ya utawala wa kikoloni....mwaka 1971 mgodi ulitaifishwa....lakini ulipata hasara chini ya uongozi wa watanzania waliokuwa na weledi mdogo katika mambo hayo....hivyo serikali iliamua kuuza share kwa wawekezaji mwaka 1994 ambapo Rais alikuwa Ally Hassan Mwinyi!
 
Nyerere angekuwa hai wa kwanza kumfungulia mashtaka ningekuwa mimi alitutesa saana huyu kuanzia Elimu katunyima kabisa elimu huyu katupotezea fursa nyingi kiuchumi leo Kenya kutuacha mbali ni makosa ya huyu mzee alituvalisha tairi za gari chai tukaweka peremende nyeupe badala ya sukari viwanda alijenga havikuzalisha hata siku mmoja watu tukaishia kuvaa kaniki wakati viwanda vya Textile alijenga vikafika vitano kuna kiwanda alijenga shinyanga mpaka leo hakijafunguliwa Tanzania meat pakers

wahi shule usome mambo ya Stages of Development. Kosa la Nyerere ni kujaribu kuleta usawa katika ukuaji wa miji ili kuondoa ukabila. Mfano kiwanda cha kukata almasi alikiweka Iringa badala ya Shinyanga. Kwa namna fulani alikuwa visionary. Look at what is happening in Dar, 'horrible and chaotic' as if nchi ni Dar. Viwanda 90%, vyuo vya elimu ya juu 60% Dar. Upuuzi wa wapuuzi wa CCM
 
Hili ndo tatizo kubwa la jamii forum, imegeuzwa sehemu ku-discuss mambo ya udaku. It is well said enzi ya Nyerere at least we had 25% ya maslahi kwenye migodi na leo tupo 3% or 4%. Halafu watu wanaponda sera zake, stupid kabisa. We need to improve from where he left the country at na pia tumuache mzee wetu apumzike mahali pema peponi.!
 
Hujui chochote naona umekurupuka kujibu kitu amabacho hujui. Mwaka 1940 ndio wamegundua kuwa Mwadui kuna almasi ulivyokuwa mpuuzi unadhani mgodi ndio umeanza kazi huo mwaka 1940.

Mgodi wa Mwadui umeanza kazi mwaka 1960...ulivyokuwa kauzu ebu jiulize wakati mgodi unafanya kazi Nyerere alikuwa nani.

Ok kwa hiyo we una maoni gani?
 
Hujui chochote naona umekurupuka kujibu kitu amabacho hujui. Mwaka 1940 ndio wamegundua kuwa Mwadui kuna almasi ulivyokuwa mpuuzi unadhani mgodi ndio umeanza kazi huo mwaka 1940.

Mgodi wa Mwadui umeanza kazi mwaka 1960...ulivyokuwa kauzu ebu jiulize wakati mgodi unafanya kazi Nyerere alikuwa nani.

Ha ha haaa, kweli umeamua kumfanyizia ukauzu huyu jamaa!
 
Back
Top Bottom