Kwanini mwisho wa madikteta na wababe wa vita duniani kote huwa si mwisho mzuri?

korojani

JF-Expert Member
Dec 17, 2016
231
237
Assalaam walleikhum wanajamvi.

Nimejaribu kupitia historia za madiktekta wengi na wababe wa kivita duniani kote lakini sijaona mwisho mzuri kwa upande wao.

Nimepitia historia za wababe kama Adolf Hitler, Iddi Amin, Joseph Savimbi, Joseph Kone, Saddam Hussein, Sankara, Samuel Doo, Osama bin Laden, Mobutu Sseseseko, Laurent Gbagbo na wengineo, lakini sijaona mwisho wao ukiwa mzuri.

Wengi wao walimalizia maisha yao uhamishoni na wengine jela na wengine walipotea duniani "in a funny way".

Huwa najiuliza kama mtu akiamua kuwa mbabe wa vita au diktekta basi ajiandae kwa mwisho mbaya.

Au Mungu ndio anaanza kuwahukumu hapa hapa duniani?

Naomba kuwasilisha.
 
Savimbi alikuwa dikiteta wa nchi gani? Savimbi hakuwahi kutawala nchi yoyote Afrika licha ya kuwa kiongozi wa chama cha upinzani kama alivyo Maalim Seif Zanzibar.

Osama bin Laden alitawala Mafia!? Acha kutuletea nyimbo za halaiki za CCM, na hapo wengineo mbona hauwataji! Karumekenge!
 
Sankara unamjua au umehadithiwa? Tafuta historia yake ndio utajua alikua kiongozi wa aina gani.
 
Savimbi alikuwa dikiteta wa nchi gani? Savimbi hakuwahi kutawala nchi yoyote Afrika licha ya kuwa kiongozi wa chama cha upinzani kama alivyo Maalim Seif Zanzibar.

Osama bin Laden alitawala Mafia!? Acha kutuletea nyimbo za halaiki za CCM, na hapo wengineo mbona hauwataji! Karumekenge!
Soma uzi vizuri ulewe kabla ya kukurupuka kuhoji ujinga, nimesema madikteta na wababe wa vita.
 
Soma uzi vizuri ulewe kabla ya kukurupuka kuhoji ujinga, nimesema madikteta na wababe wa vita.
Wewe ndie unaekurupuka.. Thomas Sankara alikuwa dikteta au mbabe wa vita? Osama bin Laden kaongoza vita gani? Au yeye ni dikteta? Kukaa kimya kwa usivyovijua ni busara.

Unaweza ukapitia nyuzi mbalimbali ukasoma tu na kupitia coment nako ni kujifunza. Sio lazima kuanzisha nyuzi kwa usivyovijua!
 
San
Wewe ndie unaekurupuka.. thomas sankara alikuwa dikteta au mbabe wa vita? Osama bin Laden kaongoza vita gani? Au yeye ni dikteta? Kukaa kimya kwa usivyovijua ni busara. Unaweza ukapitia nyuzi mbalimbali ukasoma tu na kupitia coment nako ni kujifunza. Sio lazima kuanzisha nyuzi kwa usivyovijua!
Nipe maana ya vita, alafu endelee kubisha.
 
Thomas Sankara ndio the real African son, kiongozi aliyekuwa maono alitawala kipindi kifupi mpenda demokrasia na mpenda watu wake na mwenye dira ya maendeleo bahati mbaya akauwawa, inasemekana ndio Rais bora kuwahi kutokea katika bara la Africa kulingana na makala mbali mbali.
 
Kichwa cha habari kinatofautiana na hiyo mifano uliyotoa:

Next time unapozungumzia Madikteta usiwaache hawa

i) BENITO MUSOLINI
ii) MAO ZEDONG
iii) JOSEPH STALIN
iv) MOBUTU SESESEKO KUKU
Nakadhalika


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila umechanganya sana, Savimbi na Osama, hawapo kwenye kundi la madikteta.

Hawajawahi chukua uongozi wa nchi.

Janas Malhairo Savimbi, aliyezaliwa, 3 Agost 1934 huko Munhango Angola. Na aliwuwa 22 february 2002 Lucusse Angola.

Alikua kiongozi wa vita vya msituni, kupitia chama chake cha UNITA, na wakati wote aliishi vizuri na wale aliokua anawaongoza.

Osama bin Mohamed bin Awad bin Ladin, aliyezaliwa march 10 1957 huko Riadh, Saud Arabia, na aliuwawa, may 2, 2011 huko Pakistan,

Huyu alikua gaidi la kimataifa.
Hivyo hawa hawahebiki kama madikteta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom