Kwanini mwisho wa madikteta na wababe wa vita duniani kote huwa si mwisho mzuri?

Kuna watawala wengi wazuri tu wamefia ughaibuni na wengine kuuawa

Kwame Nkurumah

Samuel doe

Mahatma gandi

Milton Obote

Samora machel

John Kenedy

Anwar Saadat

Kuna wababe kadhaa pia mpaka mwisho wao wamefia kwao kwa heshma zote

Hugo shaves

Fidel Castro

Kim snr
Bush snr
Jomo Kenyata
Julius Nyerere
Omar Bongo
Bashar al assad

Meles zenawi

N.k

Zote ni coincidence tu, ukiwa mwema haimaanishi utakufa kwa namna fulan na ukiwa mbaya haimaanishi utakufa kwa namna fulan
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Savimbi alikuwa dikiteta wa nchi gani? Savimbi hakuwahi kutawala nchi yoyote Afrika licha ya kuwa kiongozi wa chama cha upinzani kama alivyo Maalim Seif Zanzibar.

Osama bin Laden alitawala Mafia!? Acha kutuletea nyimbo za halaiki za CCM, na hapo wengineo mbona hauwataji! Karumekenge!

Mkuu, savimbi amewahi kutawala sio wa kumfananisha na maalim seif, iliundwa coalition government ikaongozwa na savimbi pamoja na rais Holden Roberto kama co-presidents

( the Democratic People's Republic of Angola) iliyokua na makao makuu katika mji wa Huambo huku José Ndelé na Johnny Pinnock Eduardo wakiwa co-Prime Ministers.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda atuambie ni Sankara yupi anaemzungzia hapa!

Sent using Jamii Forums mobile app

mkuu, mleta mada yupo sahihi, someni maana ya neno DICTATOR. huko mitandaoni mtafahamu neno hilo humaanisha pia kiongozi anayeingia madarakani kwa nguvu , sankara na mwenzie Blaise Compaoré waliingia madarakani kwa mapinduzi, compaore akampa urais Sankara tarehe 4August 1983 sankara akiwa na umri wa miaka 33.

NENO DICTATOR HALIMAANISHI TU MTU ANAYETAWALA KWA NGUVU NA UNYANYASAJI WA WATU WAKE


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Savimbi hakuwa mbabe wa vita, alikuwa ni mpinzani mwenye mtazamo tofauti.

mkuu mpaka nimecheka aise hivi unamfahamu savimbi kweli ? nenda ukasome angolan civil war na angola war of independence (1961-1974), savimbi alikuwa war lord kama wakina joseph konny na pia alipigania uhuru wa nchi yake kabla ya yeye kuwa muasi, savimbi alikuwa mbabe wa vita alimiliki jeshi kabisa lenye askari zaidi ya 100000 , alikuwa hadi na ndege za kivita , au nikuletee screenshots na video umuone akiongoza vita kabisa ?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lucas Mobutu, Mkuu, malizia kwa nini Compaore aliyempa Urais Sankara baadaye alimgeuka na kumuua. Watu wanakaririshwa upande mmoja wa mtu bila kujua mtu huyo alikuwa na side B pia. Kwangu Thomas Sankara alikuwa dikteta kwa kuanza kuwaua alioshirikiana nao kwenye mapinduzi kwa hofu ya kupinduliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtu muuaji na mtesaji wa mwanadamu mwenzake kwa sababu yeyoye ile humaliza vibaya, mtu muonevu ambaye huonea mpk kutoa maisha ya mwenzake hawezi kumaliza vizuri.

Mleta maada hajafafanua tu, kuna mengi mabaya hufichwa wayatendayo watawala. Huua na kuonea wanadamu wenzao. Hunyima haki baadhi ya watu na kuwatesa watu, mtawala wa jinsi hiyo hamalizi vyema. Hupendelea baadhi ya marafiki, ndugu, kabila au koo zao, na kuwatesa wasiowapenda kamwe hawamalizi viziri.

Pia tutenge wema wanaouwawa kwa kuonewa wivu, kuhofiwa kuwa wakiwa watawala watalipa kisasi kwa waovu. Kama CCM hawa watawala wanahofu kuwa wakiingia watawala wengine watashitakiwa na kuhukumiwa hata kunyongwa.
Ndiyo maana hawaruhusu wengine licha ya wao kuishiwa plan na hata kuishiwa watendaji wazuri. Kurukia ajenda za wapinzani wao na kuzifanya zao.

Mtu muovu hawezi maliza vyema, kuna sifa kwa baadhi ya watawala lkn ukiwafuatilia ni wauaji na watesaji wa watu.
Mfano Lisu watawala hawa hawawezi kumuona anapata madaraka, wanahofu kubwa kuwa atawashitaki au hata atawaua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Assalaam walleikhum wanajamvi.

Nimejaribu kupitia historia za madiktekta wengi na wababe wa kivita duniani kote lakini sijaona mwisho mzuri kwa upande wao.

Nimepitia historia za wababe kama Adolf Hitler, Iddi Amin, Joseph Savimbi, Joseph Kone, Saddam Hussein, Sankara, Samuel Doo, Osama bin Laden, Mobutu Sseseseko, Laurent Gbagbo na wengineo, lakini sijaona mwisho wao ukiwa mzuri.

Wengi wao walimalizia maisha yao uhamishoni na wengine jela na wengine walipotea duniani "in a funny way".

Huwa najiuliza kama mtu akiamua kuwa mbabe wa vita au diktekta basi ajiandae kwa mwisho mbaya.

Au Mungu ndio anaanza kuwahukumu hapa hapa duniani?

Naomba kuwasilisha.

tukirudi kwenye mada, mwisho wetu sote hapa duniani sio mzuri kwa maana tunapokaribia kukata roho ni kipindi cha majonzi na wakati mwingine maumivu, hakuna binadamu mwenye mwisho mwema hata manabii hawakuwa na mwisho mwema, kikubwa ni kumuomba mungu tuishi maisha mema


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiwa dikteta unakuwa umeua watu wengi sana siku wakikupatia hakuachi, ndio maana madikteta wengi ni paranoid.
 
Back
Top Bottom