Kwanini Mwigulu Nchemba anakuwa mkali watu wakisema Rais avunje Baraza la Mawaziri?

Kama namuona anavyousoma huu uzi🤣
huh.png
 
Wakuu salaam,

Mimi nimeingiwa na wasiwasi. Kwanini watu wakisema rais avunje baraza la Mawaziri ili aweze kuteua Mawaziri wapya na kuwaapisha, Mwigulu anatokwa povu sana? Katiba inamtaka Rais ateuwe Baraza la Mawaziri na Wale kiapo cha utii mbele yake.

Lakini Mwigulu anadai eti uongozi ni ule ule unaendelea. Kama ni uleule kwanini rais aliapa? Wewe Waziri ni nani usile kiapo cha Utii kwa rais? Au sababu ni Mwanamke?

Mawaziri hawawezi kumheshimu rais kwani hawajala kiapo cha kumtii rais na Katiba. Walioapa kumtii kashakufa, hatuwezi ongozwa kwa kivuli cha marehemu. Sasa ni Mambo mapya.

Watanzania tusitishwe na ovu la Mwigulu, lazima aape kumtiii Rais Samia Suluhu.

Ibara ya 42 (5) inasema Kila Rais mteule na kila mtu atakayeshikilia kiti cha Rais, kabla ya kushika madaraka ya Rais, ataapa mbele ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano kiapo cha uaminifu na kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.

Baada ya rais kuapa anatakiwa kuapisha Mawaziri. Uongozi wa hayati Magufuli uliiisha alipokufa ndo maana Samia akaapishwa haraka ili nchi isikae bila utawala.

Mawaziri waape pia.

Ibara ya 56 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatamka wazi kwamba “Waziri au Naibu Waziri hatashika madaraka yake ila mpaka awe ameapa kwanza mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.”

Ibara hii ya 68 inataka Mbunge aape kwanza kwa nafasi hiyo ndio aendelee na shughuli anazopewa kama Mbunge mojawapo ikiwa ni kuweza kuteuliwa kuwa Waziri. Na kifungu cha 56 cha Katiba hiyo hiyo kinatanabaisha kuwa mteule wa uwaziri si tu anapaswa kuapa kuwa Waziri bali awe amefanya viapo vingine, (ambavyo idadi yake haijaanishwa) kwa nafasi nyingine ya majukumu atakayokabidhiwa.

Hii inamaanisha kuwa kiapo kama hicho cha kumruhusu kuwa Mbunge ili aweze kushugulika na shughuli za kibunge au hata kuteuliwa kuwa Waziri.

Hata kama rais Samia ni Mwanamke, kuleni kiapo cha kumtii tena iwe live TBC

Nmemaliza na Sifuti.

View attachment 1738462
Dkt Mwigulu Nchemba ambaye ni Mbunge wa Iramba Mashariki Waziri wa Katiba na Sheria.
Huyu ni mpuuzi anaogopa kuachwa maana jamii haimtaki kabisa
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom