NORTHERNIST
JF-Expert Member
- Feb 10, 2021
- 302
- 244
GOODAmina Victor wa happy
MSEZA MKULU
Bosi ninachoepuka hapa nikubishana na watu ambao wameambiwa hakuna Mungu. Hawana Hoja yoyote ya msingi watabisha bila hata point ya msingi. Tulichojaribu kuwajibu kwa kirefu sana humu jukwaani ni kwamba,
Maswali na hoja zoote zinazotolewa juu ya uwepo wa Mungu vinajibika kiurahisi mno kwa kujua tu Mungu ni nani ?!
Maana ya Neno Mungu:
Neno Mungu maana yake ni Muumbaji, Mungu sio jina la kawaida, ni jina ambalo limetokana na sifa ya uumbaji kama vile tunavyoona Muashi, Mhunzi, Sonara na kadharika.
Kinachofanya Jina hili liwe na title kubwa zaidi Ulimwenguni ni kwasababu ya ukweli kwamba Hakuna Mungu (Muumbaji) mwingine zaidi ya Yule muumba mbingu na nchi. Vitanda vipo vingi na watengenezaji ni wengi lakini Dunia ni moja Hakuna nyingine. Masonara wapo wengi na vito vya thamani vipo vya kila aina, lakini Binadamu ni wa aina moja na Uliyemuumba (Mungu) ni mmoja. Hii ndio sifa ambayo inafanya Mungu(Muumbaji) awe mwanataaluma wa kutisha zaidi katika historia.
Mungu ni Nani?
Ukishaelewa kuwa Mungu ni muumbaji, katika hali ya kawaida tu utataka kufahamu kuwa huyo muumbaji ni nani. Kwenye vitabu vya imani tunasoma kuwa Mungu ni Roho (Yoh 4:24).
Mungu yupoje ?
Ukielewa kuwa Mungu ni Roho kisha ukauliza Yupoje maana yake unataka kujua kuwa Roho ipoje! . Luka 24:39 "Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikenishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo"
Hapo elewa kuwa Mungu ni kama Upepo tu Hana Mwili wala umbile lolote.
Ndugu Deejay nasmile Tambua kwamba, Hatumjui mungu kwasababu ya Ukristo na Uisilamu, Mungu alitambuliwa tangu enzi za mababu zetu. Ukristo na Uislamu ni Taratibu tu wa Jinsi ya Kumfata Huyo Roho Aliyeumba mbingu na Nchi. Pia Tambua kwamba Fikra za kwanini mungu hajataka kujitokeza si fikra sahihi hata kidogo kwani yupo hata hapo ulipoandika hii post ya kumhoji.
Jaribu kuuliza maswali ya msingi, uliza kwanini tumtafute, uliza kwanini kunahukumu na kiama, uliza maswali mazito kuhusu mungu JF kuna wataalamu Watakudadavulia, acha kukaririshwa kuwa hakuna Mungu.
Summary:
Neno Mungu limetokana na sifa ya UUmbaji (Muumbaji)! Mungu ni Roho (Hana mwili wala mfupa), Hivyo yupo kila mahali.
Roho haina mwili wala mfupa lakini inaweza kuvaa umbo lolote lile,
mf: Mungu alivyotaka kuongea na mussa alijitokeza kwa njia ya kijiti, roho ilijidhihirisha kwa njia hiyo, Hivyo inawezekana Mababu zetu walikuwa sawa kuabudu milima.
Kama Mungu aliweza kujidhihirisha kupitia kijiti basi anaweza kupitia ngombe, anaweza kupitia mti, anaweza kupitia mlima, kwasababu vyote hivi vinathamani zaidi ya Kijiti alichotumia kipindi cha mussa,
na wakati mwingine anaweza kujidhihirisha kupitia Umbile la kibinadamu, Hatuna sababu ya kubishana na njia aliyotumia wala kile alichofanya alipojidhihirisha, ila kutafakari lengo lake na maagizo aliyoacha.
Muda unabana lakini kwa haya machache nadhani nimeeleweka na tutaendelea kubadilishana mawazo