Kwanini mwenge unalindwa Kama Benki kuu?

Ciprofloxacin.

JF-Expert Member
Apr 15, 2015
1,583
2,696
Zamani nilidhani mwenge ni dhahabu tupu, baadae nilipokuja kuijua dhahabu vizuri ndo nikabaini kuwa wala si dhahabu hata kidogo, maana dhahabu yenye ukubwa wa mwenge huwezi kuibeba Kama mwenge unavyobebwa.
Ni lazima iwe nzito kupindukia kiasi cha kufikia kilo 200,hiyo ndo nature ya dhahabu.
Sasa mwenge unalindwa utadhani benk kuu, askari zaidi ya 20 wenye silaha nzito wanalinda mwenge, ni nani wa kuuiba hata ukiachwa bila ulinzi? uuibe mwenge utauuza wapi au itakusaidia nini?
Karibuni Lumumba Kwa ufafanuzi maana nyie ndo mnaijua hiyo siri.
 
Ukijaribu kuuiba mwenge wa uhuru utapatwa na maluhani na mapepo yote
 
Kwa ufupi
Licha ya kuteketeza mamilioni
unapokimbizwa yeye analipwa
sh250,000, sasa ni mlemavu.
Habari
MONDAY, SEPTEMBER 14, 2015
'Anayeunda
Mwenge wa
Uhuru' huyu hapa
 0   0  0
 0  0  0  0
Shaban Mwinchumu akiwa na
mkewe Asha Abbas, walipofika ofisi
za gazeti hili Tabata Relini, Barabara
ya Mandela Dar es Salaam wiki
iliyopita na kutoa malalamiko yake.
Picha ndogo ni Mwenge wa Uhuru
unavyoonekana baada ya kuwashwa.
Picha na Venance Nestory.
Mbio za Mwenge wa Uhuru zina
historia kubwa katika Taifa letu
tangu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere alipozianzisha
Desemba 9, 1961 akisema;
... tunataka kuwasha Mwenge na
kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro,
umulike hata nje ya mipaka yetu;
ulete tumaini pale ambapo hakuna
matumaini, upendo mahali palipo na
chuki na heshima palipojaa dharau.”
Mwenge huo uliwekwa juu ya Mlima
Kilimanjaro na shujaa Luteni Kanali
Alexander Nyirenda(marehemu),
huku baba wa Taifa akisisitiza kuwa
una umuhimu mkubwa katika
kuijenga Tanzania yenye umoja,
mshikamano na upendo miongoni
mwa wananchi wake na kusababisha
nchi kuwa miongoni mwa
zinanzosifika kwa amani na utulivu
duniani kote.
Ndiyo sababu, kila wakati Taifa
liawajibika kujikumbusha bila ya
kuchoka juu ya dhana na falsafa hiyo
kupitia maneno ya busara, hekima,
uzalendo na upendo yaliyotamkwa
na Mwalimu Nyerere kabla na baada
ya Uhuru.
Maneno ya Mwalimu yalikuwa na
maana kubwa na yanaendelea kuwa
na maana hata kwa sasa. Mwenge
umekuwa ukikimbizwa nchi nzima
ukipita kwenye mitaa, vijiji, wilaya
na mikoa na umeendelea
kuwakumbusha Watanzania wajibu
wa kufanya kazi kwa bidii ili kuleta
maendeleo huku ukitumika kuzindua
miradi mbalimbali kila mwaka
kwenye maeneo unakopita.
Hata hivyo licha ya heshima
unaopata mwenge huo, huku
ukichangiwa mamilioni ya fedha
kwa ajili ya mafuta yake
unapokimbizwa, mamilioni mengine
ya Serikali yakitumika kwa posho za
wakimbiza mwenge kuzunguka nchi
nzima huku ukiacha maswali
yanayokosa majibu.
Je, umewahi kujiuliza mwenge huo
unatengezwa wapi na nani?
Je, unatengezwa kwa thamani gani?
Anayetengeneza analipwa kiasi gani
cha fedha licha ya thamani kubwa
iliyopo?
Mtengenezaji alonga
Gazeti hili limefanikiwa kumnasa
fundi anayetengeneza Mwenge huo,
akifanya kazi hiyo kwa miaka 25
sasa baada ya kuirithi kutoka kwa
mwasisi aliyeifanya tangu mwaka
1961.
Shaban Mwinchumu (46) mkazi wa
Gongolamboto jijini Dar es Salaam
anasema ndiye fundi
anayetengeneza Mwenge wa Uhuru
tangu mwaka 1990 hadi sasa.
Anasema alianza kazi hiyo akiwa
mwajiriwa na Kampuni ya Recco
Engineering company Ltd, iliyopo
Chang’ombe, Wilaya ya Temeke,
ambayo hufanya kazi za kihandisi.
Anasema baada ya kuajiriwa na
kampuni hiyo mwaka 1990,
alifundishwa kutengeneza mwenge
huo na mfanyakazi mwenzake
wakati huo, Athuman Ali kabla ya
kufariki mwaka 1993.
“Baada ya mzee Athumani kufariki,
jukumu la kutengeza Mwenge wa
Uhuru nikaachiwa kwani hapakuwa
na mtu mwingine mwenye uwezo
huo,” anasema.
Anasema tangu mwaka 1993
amekuwa mkuu wa kazi hiyo, akiwa
mwajiriwa wa kampuni hiyo hadi
alipoacha kazi mwaka 2008.
Anasema kutokana na shughuli zake
za kutumia moto kuyayusha vyuma,
jicho lake moja likapoteza uwezo wa
kuona na daktari akamshauri
apumzike kufanya kazi hiyo.
“Niliueleza utawala wa kampuni,
ukanishauri niandike barua ya
kuacha kazi na kuahidi wangenilipa,
lakini hawakufanya hivyo,”
anasema.
Anasema tangu kipindi hicho,
amekuwa akiitwa na uongozi wa
kampuni hiyo kutengeneza Mwenge
kila wanapopewa kazi hiyo kutoka
Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo
ya Vijana.
“Serikali inaipa Kampuni ya Recco
kazi ya kutengeneza Mwenge, lakini
mimi ndiye mtengenezaji kwa
sababu ndiye wanayonitegemea hadi
sasa na mwaka huu niliutengeneza,”
anabainisha.
Analipwa kiasi gani?
Anasema amekuwa akilipwa Sh
250,000 kwa kila Mwenge
anaotengeneza na wakati mwingine
hutakiwa kutengeneza miwili mpaka
mitatu kwa mwaka.
Recco wazungumza
Uongozi wa kampuni hiyo
unathibitisha kupewa kazi ya
kutengeza Mwenge na Serikali tangu
enzi za utawala wa awamu ya
kwanza wa Mwalimu Julius Nyerere.
Mhasibu wa kampuni hiyo, Akida
Sheffa anasema: “Ni kweli Mwenge
wa Uhuru unatengenezwa katika
kampuni yetu.”
Hata hivyo, mmoja wa viongozi
ambaye alikataa jina lake lisitajwe
anasema: “Masuala mengine kuhusu
Mwenge wa Uhuru, hatuwezi
kukuambia kwa sababu yanahusu
Usalama wa Taifa.”
Mwenge unavyotengenezwa
Mwinchumu anasema Mwenge
hutengenezwa kwa kutumia madini
ya chuma, shaba, bati na mti aina ya
mpingo au mninga.
Anasema mti wa mninga au mpingo
hutumika kwa ajili ya kuushikilia
mwenge wakati wa kuukimbiza.
Anasema tenki la kuhifadhia mafuta
ya mwenge, hutengenezwa kwa
chuma na huunganishwa na ndimi
za utambi kwa ajili ya kuwaka.
Uzito wa Mwenge
Mwinchumu anabainisha kuwa
Mwenge ukitengenezwa, kabla ya
kuwekwa mafuta huwa na uzito wa
kilogramu tano.
Anafafanua kuwa kazi ya
kuutengeneza Mwenge huo,
huchukua wastani wa wiki moja.
“Nikiitwa na Recco nakwenda
kwenye karakana yao na
kuutengeneza na kulipwa baada ya
kufanya kazi hiyo,” anasema.
Anajisikiaje unapokimbizwa?
Mwinchumu anasema akiona
mwenge unapokimbizwa maeneo
mbalimbali ya nchi, hupata faraja na
kuona kwamba ametoa mchango
mkubwa kwa Taifa.
Lakini anasikitika akiona miradi ya
mamilioni ya shilingi inazinduliwa
wakati wa mbio za Mwenge huku
aliyeutengeneza akishamiri kwa
umasikini wa kipato na ajira.
Amwandikia barua Rais Kikwete
Kutokana na ukali wa maisha, licha
ya kufanya kazi inayostahili
kutambulika kitaifa Mwinchumu,
anasema aliamua kuandika barua
kwa Rais Jakaya Kikwete kuomba
msaada kwa imani kuwa kwa nafasi
aliyonayo ya urais na Mwenyekiti wa
Chama cha Mapinduzi(CCM)
kilichoasisi mwenge huo na haiba
yake anaweza kumsaidia.
Katika barua aliyoiandika kwenda
kwa Rais Kikwete Oktoba 9, 2008,
Mwinchumu anasema ingawa
anafanya kazi ya kitaifa lakini hana
ajira ya kudumu, pia hatambuliki
kitaifa.
Anasema hajui kama aliyemfundisha
kazi hiyo ndiye mbunifu, bali
anaamini ni yeye pekee mwenye
utaalamu huo na kuiomba Serikali
impe ajira ya kazi hiyo badala ya
kuipa kampuni.
Mwenge umempa ulemavu
Anasema kazi ya kutengeneza
Mwenge ndiyo iliyompa ulemavu wa
jicho alionao, hivyo anamwomba
Rais Kikwete amsaidie kupata kazi
hiyo ya kudumu ili aweze kuendesha
maisha yake.
“Sina ajira, lakini kazi ninayoifanya
ina faida kubwa kwa taifa. Lakini
tangu nimeanza sijawahi kupewa
tuzo wala cheti cha kutambua
mchango wangu kwa taifa, badala
yake wanafaidi wakubwa(Kampuni
ya Recco),” anasema.
Anasem:, “Nina watoto watano,
miongoni mwao ni yatima
nilioachiwa na ndugu zangu
waliofariki. Wote ninawalea tangu
mwaka 1995.”
“Nimekuwa naona watu wanapewa
Nishani za Mwenge na Rais kwa
michango waliyotoa katika jamii,
ingawa nishani haiombwi, lakini
nadhani nami nastahili kwa kazi
ninayofanya,” anasema Mwinchumu.
Anasema kwa sasa anaishi kwa kazi
ya kuchomea vyuma, ingawa ni kwa
`kujishikiza’ kwenye karakana za
mafundi wengine.
“Nina fani ya uchomeaji wa vyuma,
lakini sitachagua kazi
nitakayopewa,” anasema.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom