Kwanini Mwanamke asipojua kuosha Mwiko, Sufuria na Mchi huwa anadharaulika?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,542
108,858
Kuna Siri gani iliyojificha ambayo naiona sana huku Uswahilini / Uswazinyo Kwetu kwamba endapo Mtoto wa Kike ( Binti ) au Mwanamke akiwa hajui kuosha vizuri Mwiko, Sufuria na Mchi ule wa Kutwangia huwa anadharaulika sana na kuonekana kwamba hatoweza pia kuishi vizuri na Mwanaume na kwamba atawatia aibu Wazazi / Walezi wake?

Nayasubiri majibu yenu kwa hamu sana hivyo karibuni mtiririke na mserereke ili nami nijifunze na nianze kumshikia bango ' Binti ' yangu Charlotte mapema nae aanze sasa Kujifunza kuosha vizuri Mwiko, Sufuria na Mchi baadae huko Baba yake GENTAMYCINE nisije kuadhirika na wale watakaomuoa.

Nawasilisha.
 
Uzungu mwingi ndio maana
 
Mie nilikuwa naambiwa na Bibi yake Emmy kuwa hiyo ya kutokuosha mwiko hasa ule uliopikiwa ugali ukiachwa unazagaa na uchafu pasi kuoshwa huwa anasema mwanamke mwenye mazowea hayo huwa anahesabika hata kuosha maeneo yake vizuri huko kwa bibi au kunyoa zile naniliu hajui.

Saa nyingine nadhani walitupa mifano ya aina hiyo ili tupate kuwa wanawake wenye kujali usafi hasa huko maeneo yaliyojificha kwamba utakapokuwa mchafu huna tofauti na mwiko uliopikiwa pasi kuoshwa.
 
Mkuu yaani jibu jepesi sana tu kama jinsi unavoweza kufikitia

Mchi wa kutwangia unafananishwa na mtaimnooo

Sufuria unafananishwa na papuchiiiik

Ndo maana kama hajui usafi huu hata akiambiwa jinsi ya kusafisha mtaimbo hataweza wala yeye mwenyewe hataweza kujisafisha

Ujue

Waliongea kwa mafumbo ili ikifika unyago inakuwa nyepesi kufunda

Teh
 
Kweli hizi mambo za uswahilini. Maana kwenye kusafisha sufuria napo kuna masharti mara sijui uanzie nje sijui ndani. Aagh
 
Mie nilikuwa naambiwa na Bibi yake Emmy kuwa hiyo ya kutokuosha mwiko hasa ule uliopikiwa ugali ukiachwa unazagaa na uchafu pasi kuoshwa huwa anasema mwanamke mwenye mazowea hayo huwa anahesabika hata kuosha maeneo yake vizuri huko kwa bibi au kunyoa zile naniliu hajui.

Saa nyingine nadhani walitupa mifano ya aina hiyo ili tupate kuwa wanawake wenye kujali usafi hasa huko maeneo yaliyojificha kwamba utakapokuwa mchafu huna tofauti na mwiko uliopikiwa pasi kuoshwa.
Ewaaah, kazia hapohapo bint.
Hasa ni mafumbo ya kufundishia wakubwa.
Kwamba hayo mamiiko na masufuria hayajalengwa, kulikolengwa ni kulekule ulikokusemea.
 
Mie nilikuwa naambiwa na Bibi yake Emmy kuwa hiyo ya kutokuosha mwiko hasa ule uliopikiwa ugali ukiachwa unazagaa na uchafu pasi kuoshwa huwa anasema mwanamke mwenye mazowea hayo huwa anahesabika hata kuosha maeneo yake vizuri huko kwa bibi au kunyoa zile naniliu hajui.

Saa nyingine nadhani walitupa mifano ya aina hiyo ili tupate kuwa wanawake wenye kujali usafi hasa huko maeneo yaliyojificha kwamba utakapokuwa mchafu huna tofauti na mwiko uliopikiwa pasi kuoshwa.
Uko sahihi lkn pia kuna zaidi ya hayo unaambiwa siku ukifundwa (kitchen party) wakati ukijiandaa kuolewa. Haya ni maalum kwa wanawake na wanaume hayawahusu.

Mtoa uzi hayo hayakuhusu kabisa wewe mwanaume na hata kama una binti yako sio wewe utakayewajibika kumfundisha bali ni mama/bibi/shangazi zake..
 
Mie nilikuwa naambiwa na Bibi yake Emmy kuwa hiyo ya kutokuosha mwiko hasa ule uliopikiwa ugali ukiachwa unazagaa na uchafu pasi kuoshwa huwa anasema mwanamke mwenye mazowea hayo huwa anahesabika hata kuosha maeneo yake vizuri huko kwa bibi au kunyoa zile naniliu hajui.

Saa nyingine nadhani walitupa mifano ya aina hiyo ili tupate kuwa wanawake wenye kujali usafi hasa huko maeneo yaliyojificha kwamba utakapokuwa mchafu huna tofauti na mwiko uliopikiwa pasi kuoshwa.
Shida ya mwiko usipouosha baada tu ya kupika unaweza kukaa hata wiki huoshi.

Emmy umenikumbusha siku za ujana wangu.
 
Mwiko usipouosha pale unapotoka kusonga ugali unang'ang'ania uchafu unakuwa kazi kutoka, sufuria ukimaliza kusonga ugali Yale makoko ya juu yanang'ang'ania Kutoka ni shida mwanamke ambaye ana tabia hiyo ni Dalili ya uchafu na uchafu siyo sifa ya mwanamke.
 
Mchi kuosha ni rahisi Sana hata mtoto anakuoshea Sasa wewe mwanamke mtumzima uliyekomaa hedhi ushindwe kuosha Mchi huo ni uchafu uliyotukuka.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom