Kwanini mwalimu aliyemchapa mtoto hadi kufa amehukumiwa kunyongwa?

Sema Tanzania

JF-Expert Member
May 18, 2016
251
465
Marehemu alikuwa anasoma wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Kibeta iliyoko Manispaa ya Bukoba, jina lake ni Sperius Eradius amefariki akiwa na miaka 13, baada ya kipigwa na mwalimu wake akituhumiwa kuiba pochi ya mwalimu.

Siku ya tukio marehemu Sperius Eradius alikwenda kumpokea mizigo mwalimu wake aliyefika shuleni hapo kwa usafiri wa bodaboda, lakini baada ya mwalimu kuingia ofisini alianza kulalamika kutoiona pochi yake.

Mtoto huyu aliitwa na kuanza kuhojiwa kuhusu kupotea kwa pochi hiyo na akakana kuichukua, hali iliyosababisha kuanza kupigwa akitakiwa kuirejesha. Wanafunzi wenzake walihimizwa kuitafuta pochi hiyo mpaka chooni, lakini hawakuiona huku Sperius Eradius akiendelea kuadhibiwa.

Pochi ilipatikana. Cha kusikitisha ni kwamba wakati marehemu akiendelea kupigwa, dereva bodaboda alifika shuleni hapo akimtafuta mwalimu aliyepoteza pochi na kumkabidhi pochi aliyokuwa ameisahau kwenye pikipiki yake. Baada ya pochi hiyo kupatikana, mmoja wa walimu aliagiza Sperius Eradius apatiwe juisi na bagia, chakula ambacho hakuweza kukila kutokana na maumivu.

Kesi dhidi ya walimu hao (yaai ‘alopoteza’ pochi na alotoa adhabu) imeendeshwa ndani ya siku thelathini na kutolewa hukumu na Jaji Lameck Mlacha. Mwalimu Heriet Gerald ‘alieibiwa’ pochi ameachiwa na Mahakama Kuu. Wakati mwalimu Respicius Mtazangira akianguka kizimbani baada ya kuhukumiwa kifo kwa mauaji ya mwanafunzi.

Washtakiwa wote walishtakiwa kwa kosa la mauaji ya makusudi ya mwanafunzi Sperius Eradius. Katika hukumu iliyosomwa kwa saa mbili, Jaji Mlacha amesema upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha ushiriki wa Heriet kwenye kifo cha Sperius, huku Respicius akitiwa hatiani na kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Kuhusu nia ya kuua, Jaji Mlacha amesema Mwalimu Respicius ambaye alikuwa akisimamia nidhamu, alimpiga kwa fimbo ya kawaida mwanafunzi huyo na baadaye kutumia kuni, jambo lililosababisha majeraha kwenye mwili wa mwanafunzi huyo na ni ushahidi kuwa alipigwa mara nyingi.

Ushahidi wa daktari. Mahakama imezingatia ushahidi wa daktari wa magonjwa na vifo kutoka Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza, Dr. Kahima Jackson ambaye alisema kifo kilisababishwa na mshtuko uliotokana na kipigo.

Tunapenda kuwakumbusha wazazi, wanafunzi, walimu, washika dau pamoja na wananchi wote kuwa mnamo mwaka 2002, Serikali ya JMT kupitia Wizara ya Elimu ilitoa Waraka wa Elimu (Na.24) Kuhusu Adhabu ya Viboko na kuweka utaratibu mahususi wa utolewaji wa adhabu ya viboko. Adhabu hiyo inaweza kutolewa endapo kutatokea utovu wa nidhamu uliokithiri ama kwa makosa ya jinai yaliyotendeka ndani ama nje ya shule yenye muelekeo wa kuishushia shule heshima. Waraka huu pia unaongeza kuwa adhabu ya viboko itakayotolewa sharti izingatie ukubwa wa kosa, umri, jinsi na afya ya mtoto na isizidi viboko vinne kwa wakati mmoja.

Kwa maoni na ushauri tupigie simu namba 116 ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile unaweza kutupata kupitia ukurasa wetu wa Facebook: Sema Tanzania; Twitter: @SemaTanzania na www.sematanzania.org.

Aisee inasikitisha sana, RIP kijana!! Waraka wa kumchapa mtoto ulishatolewa!! Mtoto hapigwi mpaka kibali cha maandishi kitoke kwa Mwalimu Mkuu!! Na Mwl Mkuu akitoa kibali ni lazima kuwa na sababu maalum ya kumchapa. Nafikiri hukumu ni kali ila kama ipo sawa tu, jino kwa jino!!
 
Walimu wazingatie hili;
tapatalk_1551868204801.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. Walimu wapendeni wanafunzi wenu.
2.Mwalimu umekua na kupata elimu ya kotosha kupewa majukumu ya kuelimisha umma, 3. Unawekaji bifu na kijana mdogo asiyejua chochote ?
Hivi kweli mlisoma maadili ya ufundishaji ?
4. Mnapenda sana kupiga watoto, ivi ni kwanini ?
5. Wewe ni mlezi au mpigaji ?
6. Ivi msipowapiga watoto mtapunguziwa mishahara yenu ?
7. Kama mnataka fani ya mapigano kwanini Msijiandikishe kwenye UBONDIA ?
8. Hivi huko chuoni kwenu mlisomeaga mambo ya kuwachapa bakora wanafinzi ?
9. Hivi unapomchapa mtoto unaijua afya yake ?
10. Sasa mchapaji mwenzenu kahukumiwa Kunyongwa, hii ndio furaha yenu ?
11. Yaani walimu wa Primary wengi wenu ni Zero na masikini wa kutupwa, mnataka umaarufu kupitia viboko.
12. Na baadhi ya walimu wa sekondari
13. Hivi mda wote huu, mmeshinda kuwaiga waalimu wa vyuo ?
14. Kweli ninyi ni Zero IQ
15. Mtoto wa mwenzio, hata akiwa mtundu, kwanza mjue ni mtoto. Haijui dunia na kanumi zake.
16. Ndio kwanza kazaliwa mwaka uliopita
17. Hivi wewe mwalimu muhenga unashindwa hata kujua hilo ?
18 l. Huo UPUMBAVU WAKO uliusomea cbuo gani ?
19.UPIMBAVU wa kutokujua nanitoto na nani mkubwa.
20. Huyo mwalimu aliyeua mwanafunzi nakuomba Raisi Magufuli " myonge haraka sana aana.
21. Tumechoshwa na UPUMBAVU WA WALIMU.
22.Jitu limesoma hadi chuo linakuja kuweka bifu mtoto mchanga...!
23. Tanzania ya saaa haihitaji kuwa na watu kama hilo Li mwalimu.
24. Baadhi ya Walimu ni WAPUBAVU KUZIDI wengine
25. Baba Magufuli Linyonge hilo linalojiita Limwalimu.
26. Haraka sana
27. Hatuhitaji kuishi na WAPUMBAVU.
28. Yaani Serikali inakulipa mshahara ili ulee watoto wake
29. Wewe unageuka TERMINATOR...!
30. RAISI WETU MPENDWA, JOHN POMBE MAGUFULI. TAFADHALI, MUUE HUYO, MPUMBAVU.
31. TENA HARAKA SANA.

😂😂punguza hasira mkuu
 
Haujui ulichokiandika, Nonsense!!! Umeandika kwa chuki zaidi bila kuzingatia uhalisia

Hapa swali la kujiuliza ni nia ya mwalimu kupiga.

Je mwalimu alikusudia kuua?
Pengine kuna ushahidi wowote uliothibitisha kwamba mwalimu alipiga akiwa na kusudio la kuua?

Binafsi naona mwalimu hakuua kwa kukusudia, hivyo hukumu ya kunyongwa hadi kufa ni nzito sana. Angehukumiwa kwa kuua bila kukusudia, nadhani Jaji ameingiza hisia zaidi kama sisi watu wa kawaida.

Muhimu ni walimu wajifunze wanapoadhibu watoto wasipige kama wanaua mwizi wa kawaida huko mitaani.
 
Sijafurahi kwa hukumu hiyo kwa kweli.
Kesi imeendeshwa mwezi tu na hukumu just? Huyo jaji Hana vinasaba, family friend ama utani kujuana na wazazi was mtoto kweli?
Au jaji ana historia ya mtoto wake kupitia/kutendewa ubaya na watu wazima labda?

Kosa ni kubwa na baya kweli kumuua mtoto kwa kumchapa bila utaratibu(kuwa na machungu na hasira yenye mlengo was kuonya kwa dhati)

Wadau
Unaweza ukawa na nia njema, mfano ukampiga mtu aliyekukosea Kofi lisilo la nguvu na na huyo mtu akaanguka akafa. Ukaishia kupata kesi ya kuua.

Ualimu versus nidhamu za wanafunzi.

Wanafunzi was shule za msingi ni watoto wasiojielewa. Hupiga kelele sana, hawafanyi kazi zozote pasipo kusukumwa, wanatokea kwenye mazingira tofauti na familia tofauti sana. Yaweza ikawa ya wazazi walevi, wazazi wagombanao usiku kucha, wazazi wa kishua, wazazi wa chumba kimoja pamoja na watoto. Kiujumla ni shida sana ktk jamii za shule ku handle hiyo circumstances ukubali ukatae.

Then mwl anapewa wajibu wa kuhakikisha elimu na nidhamu vinamkaa vyema mtoto wa mazingira hayo tofauti tofauti. Chukua viatu vyake viwe vyako wengi wetu tungeua kwa ukatiri mkubwa kuliko huyo.

Idadi kubwa ya wanafunzi darasani versus idadi ya waalimu inachangia waalimu ku handle nidhamu za wanafunzi kwa ukali zaidi kuliko nasaha. Utawapa wangapi ufundishe saa ngapi?

Kuna mwl alipelekewa kesi na binti wa std 5 kuwa ametukanwa na dogo mtukutu wa darasani lake. Ilikuwa hivi ndo dogo mtukutu alitengeneza vinyago vya Bibi na bwana vya vijiti vyenye viungo vya uzazi. Kisha akawa anavifanyisha mbele ya yule binti na akisema ndivyo wazazi wake binti huwa wanafanya hivyo.

Kuna mwalimu wa waalimu alikuwa akimsimamia mwanafunzi wake ufundishe wa vitendo akiwa nyuma ya darasani. Ghafla dawati la pembeni kaona vurugu mara binti akapigwa kichwa na dogo wa kiume hadi jino likang'oka la yule bint. Yule mwl wa waalimu alipandwa na mori kiasi. Alimrukia yule dogo na kuanza kumng'ata yule dogo shingoni na kipindi kiliishia pale pale.

Aise acheni hiyo mambo ya vitoto vya primary. Ni havina hatia kweli kutokana na kutojielewa. Hivyo hivyo na wale wanaowafundisha tuwaache wafundishe kwa kutojielewa hivyo hivyo

Nenda na child psychology yako utaisahau tu baada ya muda na kufuata natural psychology itakayo wafaa watoto na isiyokuwepo kwenye vitabu.

Nirudi kwa mwl aliyehukumiwa.

Kwa kawaida naona huyu mwalimu ni mtu wa papara na hamaki asiyeweza kuwa na muda wa kusikia hisia za maekezo za marehemu mwanafunzi

Kwa nn nasema hivi?
Mtu akisema kitu Cha kweli hata km hukuwepo wakati kinatokea, nafsi ya msikilizaji huridhika na kuamini. Papara na hamaki huondoa hali hii ya usikivu na nafsini. Ndicho kilichomponza mwl, kwani naamini asingekuwa na papara asingempiga dogo kiasi cha kutaka kuisuuza nafsi yake. Pengine mwl aliyehukumiwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwl aliyepoteza pochi, hivyo ili kutaka kuonyesha kujali ilitakiwa amwadhibu dogo ipasavyo.
(Ni kuigegedua mada tu hapa, simaanishi km inavyosomeka)

Kwanza kitendo cha mwalimu huyu kuua tu kwake ni adhabu tosha.

Natamani mahakama kupitia jopo la majaji linge review hiyo kesi na hukumu na kuamuru vingenevyo. Maana naona sheria aliyoitumia jaji kuhumu haina macho ya kutosha.

Ualimu ni changamoto sana.

Poleni waalimu na wote mlioguswa na kuumizwa na hukumu hiyo km pia mimi ilivyoniumiza
 
Hapa swali la kujiuliza ni nia ya mwalimu kupiga.

Je mwalimu alikusudia kuua?
Pengine kuna ushahidi wowote uliothibitisha kwamba mwalimu alipiga akiwa na kusudio la kuua?

Binafsi naona mwalimu hakuua kwa kukusudia, hivyo hukumu ya kunyongwa hadi kufa ni nzito sana. Angehukumiwa kwa kuua bila kukusudia, nadhani Jaji ameingiza hisia zaidi kama sisi watu wa kawaida.

Muhimu ni walimu wajifunze wanapoadhibu watoto wasipige kama wanaua mwizi wa kawaida huko mitaani.
Mkuu, naungana na wewe! Hiyo adhabu ni kubwa sana, ukizingatia mazingira ya tukio lenyewe! Kwangu, hata kufungwa kwa zaidi ya miaka mitano, ningeiona ni adhabu iliyozidi kiwango!
Naiona inafanana na wale waliohukumiwa hivi karibuni kwa kuchoma moto kituo cha polisi
 
Kwa hiyo yule mtoto alikufa kwa mapenzi ya Mungu eti,hivi nyie unampigaje mtoto na kuni kisa pochi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom